Na Woinde Shizza Michuzi Tv,Arusha
MWANAFUNZI wa darasa la nne katika Shule ya Msingi Osunyai Elibariki Lekine (12)ambaye ni Mkazi wa Muriet jijini Arusha amejinyonga hadi kufa kwa kutumia kamba ya katani.
Akizungumza leo Agosti 23,2019 Kamanda wa Polisi mkoani hapa Jonathan Shana amesema mwanafunzi huyo amekutwa amejinyonga jana saa 11 jioni katika mtaa wa FFU uliopo Kata hiyo ya Muriet jijini hapa.
Kamanda Shana amesema mwili huo ulikutwa kwenye nyumba ambayo ujenzi wake unaendelea mali ya Emmanuel Thomas ambaye ni mkazi wa eneo hilo.
Aidha amesema mwili huo ulikutwa unaning'inia juu huku kamba iliyotumika iliyokuwa imefungwa kwenye mbao ya jukwaa linalotumiwa na mafundi ujenzi.
Amesema kwa sasa Jeshi la Polisi linaendelea kufanya upelelezi kuhusu tukio hilo ili kufahamu chanzo halisi cha tukio hilo na mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali ya Mount Meru kwa uchunguzi zaidi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...