NA MWAMVUA MWINYI,PWANI
MKUU
wa Mkoa wa Pwani ,Mhandisi Evaristi Ndikilo amepokea msaada wa mifuko
40 ya sabuni kwa ajili ya kituo cha matibabu ya Wagojwa wa COVID 19
ambayo ni Hospitali ya Wilaya ya Kibaha Mjini.
Msaada
huo umetolewa na kampuni ya KEDS Group Limited ,ikiwa ni jitihada za
kuunga mkono juhudi za serikali kuendelea kupambana na ugonjwa wa corona
.
Akipokea Msaada huo
,Mhandisi Ndikilo aliishukuru Kampuni ya KEDS Group Limited na kusema
kwani sabuni hizo zitatumika kusafishia majengo na kufulia nguo za
madaktari.
Aidha
aliwataka wawekezaji wengine ndani ya Mkoa kuiga mfano wa KEDS,kwa
kujitoa kusaidia vitakasa mkono, barakoa kwani mahitaji bado ni makubwa.
"Viwanda
tunavyo vingi ,wawekezaji na wadau wengi tuendelee kujitoa kusaidia
maeneo muhimu ambayo yanauhitaji wa tahadhali ya huu ugonjwa"
";Ninawaomba
pia wananchi waendelee kufuata maelekezo ya wataalamu wetu kujikinga na
kujilinda na ugonjwa wa corona kwa kuepuka mikusanyiko ,kushikana
mikono " alisisitiza Ndikilo.
Akikabidhi
msaada huo ,mkurugenzi wa Kampuni ya KEDS Group Limited Ben Song
alisema wametoa mchango huo kuunga mkono jitihada za Serikali katika
mapambano dhidi ya COVID 19 na wanatarajia kutoa msaada wa Barakoa
(Masks)na Vitakasa Mikono (Sanitizer).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...