Kamanda Saimon Sirro akitoa pole kwa wananchi na Viongozi Mara baada ya kuwasili eneo la Tukio Wilayani Kyerwa

Kamanda Sirro akizungumza na Wanachi wa Kyerwa Mara baada ya kuwasili eneo la Tukio Wilayani Kyerwa

Kamanda Sirro akiongea na Vyombo Vya Habari Mara baada ya kukagua jengo liliteketea kwa Moto na Kusababisha maafa makubwa

Baadhi ya Masalia ya Vifaa vilivyoteketea kwa Moto ikiwemo Vitanda na Masanduku ya Wanafunzi.
Na Abdullatif Yunus MichuziTv
KUFUATIA Tukio la Ajali ya Moto lililotokea Wilayani Kyerwa na Kusababisha maafa makubwa yakiwemo Vifo vya Watoto Kumi na wengine kadhaa kujeruhiwa, Viongozi mbalimbali wamefika eneo la Tukio kujionea hali halisi na kutoa pole kwa Wafiwa.
Mapema Mkuu wa Mkoa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti akiambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama amefika Kijiji Cha Itera na kushudia maafa hayo, ambapo kwa niaba Serikali Gaguti ametoa pole hizo na salaam za Rambi Rambi kutoka kwa Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli na kuahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Familia za Ndugu waliopatwa na maafa, ikiwa Ni pamoja na kupima Vinasaba Vya miili ya Marehemu, ikiwa pamoja na kugharamia shughuli zote za mazishi.
Aidha miongoni mwa Viongozi waliofika eneo Hilo ni pamoja na Mbunge Mteule Jumuiya ya Wanawake Tanzania Regina Zachwa ambae amekutana na Baadhi ya Wafiwa wakiwemo Viongozi wa Dini na Serikali na kutoa Pole na rambi rambi zake.
Kwa nyakati tofauti wamefika pia Afisa Elimu Mkoa Kagera, Mwenyekiti CCM Mkoa Kagera Bi. Costancia Buhiye, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Mkoa Kagera Wilbroad Mutabuzi pamoja na Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi Kamanda Saimon Sirro.
Kwa Upande wa Jeshi la Polisi, Kamanda Sirro amewaomba Wananchi kuwa wavumilivu na kutoa ushirikiano ili kubaini chanzo cha Moto huo, na kwamba ikiwa chanzo Cha ajali ikibainika kuwa ni kutokana na uzembe au miundo mbinu mbovu, hatua Kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao. Aidha Kamanda Sirro ameongeza kuwa Wamiliki wa Shule wanatakiwa kuwa na Kamati ya Usalama kuhakikisha Usalama wa Wanafunzi kuanzia majengo madhubuti na Imara, Ulinzi wa kutosha muda wote na kubaini wanafunzi watukutu ambao wengine hutumiwa katika matendo ya kiharifu.
Kufuatia Ajali hiyo na Msiba huo kitaifa, Rais Dkt. John Pombe Magufuli na Mwenyekiti wa CCM Taifa ameahirisha Mkutano wake wa Kampeini aliopanga kufanya Mkoani Kagera Manispaa ya Bukoba Septemba 15, na Sasa Mkutano huo utafanyika Tarehe 16 Septemba katika Viwanja vya Gymkhana.

Regina Zachwa Mbunge Mteule UWT Kagera akiwafariji Wafiwa Ndugu jamaa pamoja na waombolezaji Mara baada ya kuwasili Itera eneo la Tukio.
Regina Zachwa Mbunge Mteule UWT Kagera akiongea na Wakazi wa Kyerwa wakati akiwasilisha salaam zake za pole na rambi rambi kufuatia Ajali mbaya ya Moto.
Mapema Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Kyerwa Rashid Mwaimu akizungumza na Wanahabari Juu ya Tukio hilo

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Mkoa Kagera Wilbroad Mutabuzi akitoa salaam zake za pole kwa Wananchi Wilayani Kyerwa

Mwenyekiti wa CCM Mkoa Kagera Bi Costancia Buhiye akitoa salaam zake za pole kwa Wananchi na Wafiwa kufuatia Tukio la Ajali ya Moto Wilayani Kyerwa

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...