
***********************************
NA MWAMVUA MWINYI,CHALINZE
MKUU wa mkoa wa Pwani,Mhandisi Evarist Ndikilo, ametimiza agizo la Waziri Mkuu kwa kukabidhi
Madawati 305,Viti na meza 221 kwa shule mbalimbali za Halmashauri ya Chalinze .
Hatua hiyo ni
Utekelezaji wa Maagizo ya Waziri Mkuu ,Kassim Majaliwa aliyoyatoa
Desemba 7,mwaka huu kwa Wakuu wa Mikoa la Kusimamia ujenzi wa
Miundombinu ya Madarasa na Madawati ili Wanafunzi wote waliofaulu
kujiunga na kidato Cha kwanza kuingia Mashuleni ifikapo Februari 28
mwaka 2021.
Akizungumza wakati
akiwa Kikaro Sekondari -Miono, mhandisi Ndikilo alieleza ,Halmashauri
hiyo ilikuwa inakabiliwa na upungufu wa Viti na Meza 650, vyumba vya
Madarasa 13.
“Tatizo la Viti na
Meza 650 na Uhaba wa vyumba 13 vya madarasa limekwisha kwenye
Halmashauri hii, Mmeweka Mikakati Mizuri ya kukamilisha ujenzi wa
madarasa hapa, ;Hadi sasa mna upungufu wa Viti na Meza 61 huku Mbunge
Ridhiwani Kikwete ametoa fedha Sh. Milioni 3.6 kumaliza Upungufu huu,
Ujenzi wa Maboma 17 unaendelea na utakamilika mapema”
Pamoja na
hayo,Ndikilo alitoa Wito kwa Wakuu wa Wilaya kuendelea kusimamia ujenzi
wa Madarasa kwenye Wilaya zao na Amewataka wataalamu kutoka
Sekretarieti ya Mkoa kutoka maofisini kwenda kusimamia ujenzi wa
Miundombinu hiyo.
Aidha alifafanua,
mkoa huo umefaulisha wanafunzi 30,212 sawa na asilimia 86.9,
Halmashauri ya Chalinze pekee imefaulisha wanafunzi 4,965 kwa mwaka huu
na wote watapaswa Kuingia shuleni Januari 2021.
Akisoma Taarifa Mkuu wa Wilaya hiyo, Zainabu Kawawa alifafanua,
Wilaya hiyo
imejipanga kumalizia ujenzi wa Maboma 17 kupitia Sh. Milioni 100
zilizotolewa na Halmashauri ya Chalinze na wamepanga kuanza ujenzi wa
Vyumba vya madarasa 21 kwa ajili ya mwaka 2022 .
Ridhiwani
alibainisha, Maelekezo ya Waziri Mkuu wameyasimamia na kuyatekeleza
chini ya Uongozi wa Ndikilo na Zainab Kawawa na kudai Chalinze ya Sasa
Hakuna Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari na Msingi atakayekaa chini.
Ridhiwani alielezea, Umaliziaji wa Madarasa 17 yanayohitajika kuwa tayari kabla Shule hazijafunguliwa nao unaendelea.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...