Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV

*Walisema wanasikia Joto wakiwa kileleni!

BAADA ya ushindi wa Simba SC dhidi ya Gwambina FC ya Mwanza, swali la kujiuliza ni moja tu, Yanga SC wao wenyewe wanasemaje? baada ya kushushwa kileleni mwa Msimamo wa Ligi Kuu Soka Tanzania bara wakiongoza katika nafasi hiyo kwa muda mrefu tangu kuanza kwa Ligi.

Simba SC wamefikisha alama 58 wakiwa na michezo 24 katika msimamo huo baada ya ushindi wa bao 0-1 dhidi ya Gwambina ya Misungwi, Mwanza katika dimba la Gwambina Complex, Wekundu wa Msimbazi licha ya kuongoza Ligi bado wana michezo miwili mkononi ili kuwa sambamba na wapinzani Yanga SC wenye alama 57 na michezo 26.

Nahodha wa Simba SC na Mfungaji wa bao pekee katika mchezo huo, Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’ amesema wamepata alama tatu na kufika kileleni mwa Msimamo wa Ligi Kuu Soka Tanzania, Zimbwe Jr amesema uwanja wa Gwambina haukuwa rafiki kucheza pambano hilo hivyo wamejitahidi kupata alama tatu.

Simba SC wakiwa Kanda ya Ziwa katika Mikoa ya Shinyanga, Kagera na Mwanza wamejikusanyia alama tisa na wanarejea Dar es Salaam kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya Yanga SC utakaopigwa kwenye dimba la Benjamin Mkapa May 8, 2021 ikiwa ni mchezo wa marudiano katika mzunguko wa pili.

Yanga SC wao watacheza na Azam FC ikiwa ni mchezo wa 27 katika muendelezo wa Ligi hiyo ya Tanzania siku ya Jumapili majira ya 2:15 usiku katika dimba la Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Endapo Yanga SC watashinda mchezo huo dhidi ya Azam FC watarejea tena kileleni mwa msimamo wa VPL wakitikisha alama 60 wakiizidi Simba SC michezo.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...