Hatimae Safari za ndege za ATCL kutoka Tanzania kuelekea Guanzou Nchini China zinatarajiwa kuanza May 08,2021 mara moja kila baada ya wiki mbili licha ya kuendelea kuwepo janga la corona.

 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula ameyasema hayo wakati wa mazungumzo yake na Balozi wa China hapa Nchini Mhe Wang Ken a kuongeza kuwa safari hizo zitaongeza kwa kuzingatia muenendo wa maradhi ya COVID 19.

 

Kwa upande wake Balozi wa China hapa Nchini Mhe Wang Ke amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan kwa hatua yake ya kukutana na Jumuiya ya wafanyabiashara kutoka China na kuongeza kuwa hatua ya uwepo wa safari za ndege za moja kwa moja kutoka Tanzania hadi China ni fursa ya kukuza biashara na uwekezaji na kwamba China itaendelea kuunga mkono dhana ya diplomasia ya Uchumi isiyoingilia masuala ya ndani ya kwa faida ya pande zote mbili.

 

Pia Balozi Liberata Mulamula kwa nyakati tofauti amekutana na kufanya mazungumzo na Mabalozi kutoka Ujerumani,Ubelgiji na Israel ambapo masuala makubwa yaliyojadiliwa ni pamoja na mashirikiano yatakayokuza uchumi na biashara lakini pia miradi mbalimbali itakayochochea ustawi wa jamii ikiwa ni pamoja na elimu,afya na miundombinu.

 

Balozi anayeiwakilisha Israel hapa Nchini Mhe Oded Joseph amesema Israel itaendelea kushirikiana na Tanzania katika masuala mbalimbali hususani katika kukuza ujuzi wa kilimo chenye tija kwa vijana ambapo kwa sasa Israel inawapokea vijana kutoka Tanzania waliohitimu katika vyuo vya kilimo kwa lengo la kujifunza kwa vitendo Nchini humo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...