Na Hamida Kamchalla, TANGA.
WAJASIRIAMALI nchini na Zanzibar wameiomba serikali kuangalia kero wanayoipata kupitia vifungashio ambavyo vimepigwa marufuku kutumika ambavyo baadhi yao wamekuwa wakipata hasara kwa kuviagizia kutoka nchini China hasa kwa upande wa Zanzibar.Akiongea
mbele ya Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Exaud Kigahe kwa niaba ya
wengine mjasiriamali kutoka Zanzibar Dadi Ahmedi Dadi alisema Tanzania
Bara kuna viwanda vidogo vidogo vingi na vinatambulika lakini kikwazo
kikubwa ni upatikanaji wa vifungashio nchini.
"Kwanza
niseme salamu za wajasiriamali katika maonyesho ya biashara ya nane
hapa Tanga, kitu cha kwanza kinachotukwamisha wajasiriamali ni
vifungashio, jambo hili mimi binafsi katika kiwanda changu cha
usindikaji wa matunda na mbogamboga toka nilivyoanza nilikuwa naweka oda
kule China, tuna viwanda vingi Tanzania Bara lakini tunakuwa na vikwazo
kwa kiwango kikubwa cha kwenda kulipia ili kupata vifungashio" alisema.
"Muheshimiwa
Naibu Waziri naomba hili mliangalie kwa macho mawili, tunapata shida
Wanzazibar, tunapata shida Watanzania kwa ujumla, kwa ushahidi nilionao,
niliagiza mzigo wa vifungashio vya bidhaa tatu nilitakiwa nitoe
shilingi milioni kumi, sasa milioni kumi kwa mjasiriamali tukisema
tunaanza na vifungashio hii malighafi itanunuliwa kwa kitu gani, hili ni
suala gumu sana kwetu" aliongeza Dadi.
"Ili
kuendana na kasi ya ukuaji wa viwanda na biashara serikali haina budi
kuangalia eneo la viwanda vidogo vidogo na vya kati kupata vifungashio,
hiki ndio kikwazo kikubwa sana kwetu sisi" alisisitiza.
Hata
hivyo alisema kikwazo kingine ni katika kupatiwa mikopo katika Taasisi
za kibenki ambako hata ukiwa na vigezo vya kibiashara bado kuna suala la
kukosa hatimiliki ambalo kwa upande wa visiwani ni tatizo kubwa hasa
katika maeneo ya biashara.
"Kwa
ushahidi nilionao muheshimiwa, hii taasisi ya benki ya CRDB kule Pemba
ilivyoanza kazi tuliona ni benki nzuri sana, lakini katika kupata mikopo
imekuwa ni kikwazo kikubwa kutokana na mashariti magumu wanayotuwekea,
kwenye kiwanda changu meneja wa benki alikuja kututembèlea na akakuta
bidhaa tulizonazo alifarijika sana na akaona tunafaa kukopesheka, lakini
kikwazo kikubwa hatuna dhamana"alieleza.
"Watanzania
au hasa visiwani tumekuwa na tatizo la kutokuwa na hati miliki katika
maeneo ambayo ni dhamana zinazohitajoka katika Taasisi za kifedha, hivyo
tunaomba serikali kuweka sera inayotekelezeka kuhusu mikopo ili tuweze
kukopeshwa, katika mazingira hayo ya kifedha tunahitaji kuzalisha vitu
vizuri" aliongeza.
Akitoa
ufafanuzi kuhusu vikwazo vya wajasiriamali Naibu Waziri Exaud Kigahe
alisema viwanda vingi nchini ni vya uchakataji mazao ya kilimo jivyo
kuna haja ya kuongeza thamani mazao hao na kuongeza kuwa kikwazo cha
vifungashio siyo tu viwanda vidogo bali hata kwa viwanda vya kati.
Kigahe
alibainisha kwamba vifungashio ni sehemu ya ubora wa bidhaa na kukiri
kuwepo kikwazo cha mikopo na kwamba katika maonyesho hayo serikali
imechukua jukumu la kualika Taasisi zote za kibenki ili kuwezesha
wajasitiamali wadogo kipata mikopo kwenye Taasisi zao ikiwa ni pamoja na
kupitia kwenye Mashirika kama SIDO ambao pia wanakopesha kupitia mifuko
ya wananchi.
"Ndugu
zangu viwanda vingi vya Tanzania ni vile vinavyohusiana na uchakataki wa
mazao ya kilimo, na ndivyo ambavyo tunaviona hapa, nitoe pongezi kwa
wenzetu ambao wana mashine zinazotumika kuongezea thamani ya mazao,
kimsingi maonyesho haya yamekuwa kichocheo kikubwa kwa mkoa wa Tanga"
alisema.
Sambamba na hilo
aliupongeza mkoa wa Tanga kwa kuendesha maonyesho hayo kiufanisi huku
akiitaka mikoa mingine nchini kuiga mfano kwa lengo la kuongeza thamani
mazao ya kilimo na utoaji huduma
"Nipende
kutoa shukurani kwa viongozi wote walioshiriki kufanikisha maonyesho
haya, ni jambo la faraja kwa kushirikiana na serikali hii ya mkoa,
nimeambiwa kuna washiriki zaidi ya sabini na nne, kwa makampuni mengine
hayajafanikiwa kushiriki kwa tatizo moja au jingine niwaombe sana kadri
yatakavyoendelea mshiriki, lengo la serikali ni kuona hatumuachi mtu
nyuma" alieleza.
Kigahe aliongeza kuwa lengo la serikali na kuwa na uchumi wa viwanda ambao ni jumuishi kwa ajili ya maendeleo ya watu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...