Katika mwendelezo wa kuimarisha utimamu wa mwili na akili, Benki ya CRDB imeendeleza programu yake ya Wellness Day inayolenga kuwapa wafanyakazi nafasi ya kujali afya zao kwa kuwa na uwiano kati ya majukumu ya kiofisi na maisha binafsi Jijini Bunjumbura - Burundi.

Kupitia Wellnes Day inayoadhimishwa tangu mwaka 2021, wafanyakazi wa Benki ya CRDB hupata mafunzo na semina juu ya siha ya mwili, lishe bora pamoja na ustawi wa akili.

Akizungumza katika programu hiyo ilyofanyika viwanja vya Serenity Garden (Avenue du Large) ambako wafanyakazi walikuwa wanafanya mazoezi ya aina tofauti pamoja na kushiriki michezo sambamba na kupima afya. Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Benki Burundi, Fredric Siwale mara baada ya kuwaongoza katika mazoezi ya viongo, alisema mfanyakazi anapokuwa na afya njema na saikolojia yake ikakaa sawa basi atakuwa na uwezo mkubwa wa kutimiza majukumu yake na kuwahudumia wateja kwa viwango vinavyokubalika.

“Wakati wote Benki yetu imekuwa mstari wa mbele katika kuwajali sana wateja na wadau wetu. Wakati wote tunalenga kuwapa huduma bora lakini tunafahamu hatuwezi kufanikisha hilo bila kuwa na wafanyakazi wenye utulivu wa mwili na akili, hii ndio maana ya kuwa Benki kiongozi ambapo kwa mwaka huu Benki imetunukiwa tuzo ya Mwajiri bora "Top Employer" aliongeza Siwale.

Wellness Day ni mkakati wa Benki yetu ya CRDB kutoa fursa kwa wafanyakazi kupima afya, kupata ushauri wa vyakula vya kutumia pamoja na utatuzi wa changamoto nyingine yoyote inayoweza kupunguza ufanisi wa mfanyakazi,” aliongeza Siwale.

Huu ni mwendelezo wa programu hiyo ambayo kwa mwaka huu ilizinduliwa jijini Mwanza, baadae kufanyika kanda ya Kasikazini, Kusini, Magharibi na sasa imefanyika Burundi lengo ni kuwafikia wafanyakazi wote katika kanda zote nane za Benki ya CRDB pamoja na nje ya nchi ambako benki inatoa huduma kuhakikisha wafanyakazi wote wa taasisi hii kubwa zaidi ya fedha nchini inakuwa na wafanyakazi wenye weledi na wanaotoa huduma za kiwango cha juu.

Akieleza jinsi walivyojipanga kufikisha programu hiyo kwa kila mfanyakazi, Kaimu Mkurugenzi Rasiliamali watu wa Benki ya CRDB, Timoth Fasha amesema wataalamu wa afya wanashauri juu ya kupata usingizi wa kutosha, kufanya mazoezi ya mwili, kupata lishe bora pamoja na ushauri juu ya afya ya akili hivyo ni muhimu kwa kila mfanyakazi kuyafahamu mambo haya na kuyaishi.

“Mfanyakazi anaweza akajisahau kuijali afya yake kutokana na sababu mbalimbali za majukumu ya kikazi. Hivo kupitia Programu ya Wellness Day, tunawakumbusha wafanyakazi wetu umuhimu wa kuwa na ratiba ya kuulinda mwili kwa vipimo vya kitabibu, mazoezi pamoja na ushauri wa kitaalamu. Hii ni muhimu kwa sababu mafanikio ya Benki ya CRDB yanatokana na mchango wa kila mmoja wetu hivyo ni muhimu kuwa na afya njema ili kuendeleza ubora huo kwa wateja wetu,” amesema Fasha.

Kutokana na wingi wa majukumu, mfanyakazi anaweza kujikuta anatumia muda mwingi kukaa ofisini hivyo kutofanya mazoezi ya mwili au kuzungumza na watu wengine hali ambayo ikidumu kwa muda mrefu inaweza kusababisha msongo wa mawazo iwapo kutatokea hata changamoto ndogo tu kwa mhusika.

Kupitia Wellness Day, wafanyakazi wa Benki ya CRDB wanapata fursa ya kushiriki michezo ya aina tofauti, mazoezi ya viungo pamoja na kukutana na madaktari na washauri nasaha wanaotoa elimu ya saikolojia, mahusiano, matibabu, msongo wa mawazo, pamoja na lishe na usimamizi wa mtindo wa maisha.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...