Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV
TANZANIA inatarajiwa kupokea ujumbe wa viongozi wa elimu ya juu kutoka Malaysia, wakiwemo maofisa kutoka Wizara ya Elimu ya Malaysia, Education Malaysia Global Services (EMGS) pamoja na wawakilishi wa vyuo vikuu tisa watakaoshiriki Maonesho ya Elimu ya Malaysia yatakayofanyika Juni 1–3, 2026 katika Hoteli ya Serena, Dar es Salaam.
Maonesho hayo yanayoratibiwa kwa ushirikiano wa Global Education Link (GEL) na wadau wa elimu kutoka Malaysia yanalenga kufungua fursa za udahili, ufadhili wa masomo, ushirikiano wa kitaaluma pamoja na kuimarisha mahusiano ya elimu kati ya Tanzania na Malaysia.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Global Education Link, Abdumalik Mollel, alisema ujio huo ni wa kimkakati kwa kuwa unaleta pamoja mamlaka muhimu za elimu ya juu, vyuo vikuu na taasisi zinazoratibu wanafunzi wa kimataifa.
Alisema vyuo vitakavyoshiriki vitatoa taarifa kuhusu programu za masomo, gharama za elimu, mazingira ya kujifunzia, taratibu za udahili pamoja na nafasi za ufadhili wa masomo kwa wanafunzi wa Tanzania.
“Hii siyo maonesho ya kawaida ya udahili pekee. Ni fursa ya kuunganisha Tanzania na Malaysia katika elimu ya juu, scholarship, tafiti, ubunifu na ushirikiano wa kitaaluma,” alisema Mollel.
Miongoni mwa vyuo vinavyotarajiwa kushiriki ni Asia Pacific University of Technology and Innovation (APU), University of Malaya, University Putra Malaysia (UPM), University Kebangsaan Malaysia (UKM), UCSI University, University Kuala Lumpur, University Selangor (UNISEL) na Putra Business School.
Mollel alisema maonesho hayo pia yatafungua fursa za ushirikiano kati ya vyuo vya Tanzania na Malaysia kupitia makubaliano ya ushirikiano (MoU), tafiti za pamoja, ubadilishanaji wa wanafunzi na wahadhiri pamoja na programu za kitaaluma na ubunifu.
Alisema maonesho hayo yanatoa fursa muhimu kwa wanafunzi, wazazi, taasisi za elimu na Serikali katika kujenga mahusiano ya kimataifa na kuongeza nafasi za elimu kwa vijana wa Tanzania.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...