Na Karama Kenyunko Michuzi Tv
TANZANIA na Singapore zimefungua ukurasa mpya wa ushirikiano baada ya kusaini mikataba mitano na hati za makubaliano katika sekta mbalimbali hatua inayolenga kuimarisha biashara, uwekezaji na ushirikiano wa kiuchumi kati ya nchi hizo mbili.
Mikataba iliyosainiwa inahusi kuondoa kodi Mara mbili (Double Taxation) muendelezaji wa ujuzi, biashara za kaboni, mashauriano ya kidiplomasia na uwezeshaji wa biashara.
Mikataba hiyo itapunguza gharama za kufanya biashara, kupunguza vihatarishi vinavyotazamwa na wawekezaji na kuongeza imani kwa wawekezaji wanaotaka kuwekeza katika nchi hizo mbili.
Amesema nchi hizo pia zinaendelea kufanya kazi kuelekea mfumo wa pamoja wa utekelezaji wa biashara ya kaboni chini ya Kifungu cha sita cha Mkataba wa Paris huku zikihamasisha maendeleo endelevu.
Akizungumza katika Jukwaa la Biashara na Uwekezaji la Tanzania na Singapore jijini Dar es Salaam, Rais Tharman amesema dunia inakabiliwa na mazingira mapya ya biashara yenye kutokuwa na uhakika, hivyo kuna umuhimu wa kujenga njia mpya za ushirikiano wa kiuchumi na minyororo imara ya ugavi.
Kwa upande wake, Rais Samia Suluhu Hassan amesema yeye na Rais Tharman walifanya mazungumzo yaliyowezesha kusainiwa kwa makubaliano na hati za ushirikiano kwa manufaa ya nchi hizo mbili.
Amesema hatua hiyo inaonyesha dhamira ya pande zote mbili kuharakisha utekelezaji wa makubaliano yaliyofikiwa na kuinua uhusiano wa Tanzania na Singapore katika viwango vya juu zaidi.
Rais Samia amesema ziara hiyo ya Rais wa Singapore imekuja wakati nchi hizo zikiadhimisha miaka 45 ya uhusiano wa kidiplomasia na kwamba ni mara ya kwanza katika historia Rais wa Singapore kufanya ziara ya kiserikali nchini Tanzania.
Amesema Tanzania na Singapore zinaendelea kufurahia uhusiano mzuri unaojengwa katika misingi ya kuaminiana, ushirikiano na manufaa ya pamoja.
Na hii ni habari ya pili kuhusu fursa za biashara na uwekezaji.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiongoza Ujumbe wa Tanzania kwenye mazungumzo na Ujumbe wa Singapore uliongozwa na Rais wa Nchi hiyo Mheshimiwa Tharman Shanmugaratnam, tarehe 09 Juni, 2026.
Viongozi hao wawili wamefanya mazungumzo rasmi yaliolenga kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Singapore katika maeneo mbalimbali hususani biashara, uwekezaji, maendeleo ya rasilimali watu na ujuzi, pamoja na uchumi wa kidijitali.Mazungumzo hayo yalifuatiwa na utiaji saini wa mikataba na Hati za ushirikiano kati ya nchi hizo mbili, na mkutano wa pamoja na waandishi wa habari.









Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...