Wakazi na wageni wa Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara (DITF) sasa wanapata huduma za kibenki ndani ya Viwanja vya Saba Saba kupitia Tawi la NMB Saba Saba, linalofanya kazi kuanzia Juni 28 hadi Julai 13, 2026.

Tawi hilo linatoa huduma za kufungua akaunti, kuweka na kutoa fedha, malipo ya Serikali, bima na huduma za kidijitali, pamoja na ATM na mawakala waliopo viwanjani.

Kaimu Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, William Nkuna, alisema tawi hilo linalenga kusogeza huduma karibu na wananchi na wafanyabiashara wanaohudhuria maonesho.

Pia, NMB inatoa ushauri wa mikopo na huduma za kidijitali, huku wateja wakipata mikopo ya hadi Sh milioni 2 na wafanyabiashara hadi Sh milioni 5 kupitia simu.

 Kaimu Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, William Nkuna (katikati, mwenye shati jeupe), akimwelekeza Afande Bwakiswa Mwakeja kuhusu huduma zinazopatikana katika Tawi la NMB Saba Saba katika kipindi chote cha maonesho. Kushoto ni Jumanne Magige Richard, Afisa Mauzo wa Benki ya NMB.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...