Katibu NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Ndugu Kenani Kihongosi amesisitiza kuwa Vijana ndio walinda Nchi hivyo wanatakiwa kuilinda amani ya nchi ili waweze kufanya shughuli za uzalishaji kwa maendeleo ya Taifa na familia zao.
Ndugu Kenani ameyasema hayo leo tarehe 10 Agosti 2026 wakati akitoa mada kwenye Mafunzo ya Uongozi wa Seneti za Vyuo vya Kati na Vyuo Vikuu yanayofanyika katika Chuo cha Mafunzo Ihemi mkoani Iringa.
Pia, ametumia jukwaa hilo kukemea lugha chafu zinazotolewa kwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mitandao ya kijamii na kuwasihi vijana kuwa mstari wa mbele kumtetea Rais na wasikae kimya.
Aidha ametoa wito kwa Vijana wa Chama cha Mapinduzi ndani na nje ya Tanzania kulipa Ada ya uanachama akieleza uhai wa Chama cha Mapinduzi (CCM) unatokana na wanachama kulipia ada.








.jpeg)






Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...