Tanzania imejipanga kuanza kuzalisha umeme wa nyuklia ifikapo mwaka 2030, ikiwa ni sehemu ya mpango wa muda mrefu wa kuongeza vyanzo vya nishati na kukidhi mahitaji yanayoongezeka nchini, Mpango huo unalenga kuhakikisha Tanzania inaanza kutumia nishati ya nyuklia katika uzalishaji wa umeme, huku maandalizi na uwekezaji katika eneo hilo ukiendelea kuimarishwa na kukamilika ifikapo 2050.
Mtafiti Mwandamizi wa Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC), Eng. Christina Paul Nyakyi, amesema hayo jijini Tanga wakati akizungumza katika Maonesho ya Wiki ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu Kitaifa, amesema hatua hiyo ni sehemu ya mkakati wa Tanzania kuendeleza matumizi ya teknolojia ya nyuklia kwa ajili ya uzalishaji wa nishati na maendeleo ya taifa kwa ujumla.
Eng. Nyakyi amesema lengo la mwaka 2030 ni Tanzania kuwa imeanza kuzalisha umeme wa nyuklia kupitia mtambo wa kwanza wa kuzalisha nishati hiyo, hii ina maana kuwa mwaka huo unatarajiwa kuwa mwanzo wa uzalishaji wa umeme wa nyuklia nchini, na si kwamba Tanzania itakuwa tayari imefikia kiwango kikubwa cha uzalishaji wa nishati hiyo bali ni hatua kwa hatua na kukamilika mwaka 2050.
Ameeleza kuwa uwekezaji huo ni muhimu kwa uchumi wa Tanzania kwa kuwa upatikanaji wa nishati ya uhakika ni msingi wa shughuli za viwanda, biashara na huduma mbalimbali, Kwa kuongeza vyanzo vya uhakika vya uzalishaji wa umeme, ikiwemo nishati ya nyuklia, Tanzania inaweza kuongeza uwezo wake wa kukidhi mahitaji ya umeme na kupunguza changamoto zinazoweza kujitokeza kutokana na upungufu wa nishati.
Katika sekta ya afya, Eng. Nyakyi amesema teknolojia ya nyuklia ina matumizi mbalimbali katika uchunguzi na matibabu ya magonjwa, ikiwemo saratani, amesema matumizi hayo yanaifanya teknolojia ya nyuklia kuwa na umuhimu mkubwa katika kuboresha huduma za afya na kusaidia wataalamu kupata njia bora zaidi za kugundua na kutibu baadhi ya magonjwa.
Amesema katika sekta ya kilimo, teknolojia ya nyuklia inaweza kutumika katika kuboresha uzalishaji wa mazao yanayoweza kustahimili mazingira mbalimbali, ambapo teknolojia hiyo inaweza kutumika katika juhudi za kudhibiti mbu wanaoeneza magonjwa, hatua ambayo inaweza kusaidia katika kukabiliana na changamoto za kiafya zinazohusiana na wadudu hao.
Aidha, ameeleza teknolojia ya nyuklia hutumika katika sekta ya ujenzi kupitia mfumo wa Non-Destructive Testing (NDT) unaowezesha wataalamu kukagua ubora, uimara na hali ya miundombinu bila kuharibu sehemu inayofanyiwa uchunguzi, ameongeza kuwa TAEC itaendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu matumizi salama na yenye manufaa ya teknolojia ya nyuklia ili kuongeza uelewa na kuondoa mitazamo hasi kuhusu teknolojia hiyo.
Kwa ujumla, mpango huo unaweka msingi wa Tanzania kutumia teknolojia ya nyuklia si kwa ajili ya umeme pekee, bali pia kuchochea maendeleo ya uchumi, afya, kilimo na miundombinu kupitia matumizi salama na yenye tija ya teknolojia hiyo.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...