"A"
Showing posts with label A. Show all posts
Tuzo za Umoja wa Mataifa za Ubunifu katika Huduma za Umma 'UN Public Service Innovation Awards' zimetolewa leo Juni 26 mwaka huu, nchini Korea Kusini kwenye Kilele cha Wiki ya Utumishi wa Umma ya Umoja wa Mataifa 'UN Public Service Week 2024'.

Nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa 72 zimeshiriki ambapo mifumo 400 iliwasilishwa na mifumo 15 ukiwemo wa e-Mrejesho ilishinda tuzo mbalimbali ambapo, kutoka Afrika nchi zilizoshiriki na kushinda tuzo hizo ni Tanzania na Afrika Kusini pekee.

Mfumo wa e-Mrejesho unawawezesha wananchi kutuma kero au malalamiko, maoni, maswali, na pongezi kidijiti kwenda katika taasisi yoyote ya umma na kisha kupata mrejesho wa utekelezaji wake kidijiti mahali walipo.

Mfumo huu umetengenezwa na Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Mfumo wa e-Mrejesho unapatikana kwa njia tatu ambazo ni kupitia simu ya mkononi kwa kubofya *152*00# na kisha kuchagua namba 9 na kisha namba 2, njia zingine ni kupitia simu janja kwa kupakua Aplikesheni tumizi (Mobile App) ya e-Mrejesho inayopatikana kwenye Play Store na Apple Apps Store, na kwa njia ya Tovuti ya e-mrejesho.gov.go.tz.

Wiki ya Utumishi wa Umma ya Umoja wa Mataifa ni tukio la kila mwaka linaloadhimishwa kimataifa, kwa lengo la kusherehekea thamani na umuhimu wa huduma ya umma kwa jamii.

Tukio hili linasisitiza kutambua mchango wa watumishi wa umma na kuhamasisha vijana kuchagua kazi katika sekta ya umma.

Wiki hii kwa kawaida hujumuisha matukio, sherehe za tuzo, na majadiliano kuhusu jinsi ya kuboresha ufanisi wa utoaji huduma kwa umma duniani kote.




Hatimaye sasa zile zawadi zilizotajwa kutolewa kwa washindi wa mchezo wa Super Heli unaopatikana kwenye kasino ya mtandaoni. Washindi mbalimbali wa TV,Smartphones, na bonasi za kasino zinazidi kutolewa, kama bado hujacheza huu mchezo basi wakati ni sasa. Cheza Super Heli Hapa.

Super Heli kasino unataka kufanana na mchezo maarufu wa AVIATOR ambao pia unapatikana Meridianbet kasino ya mtandaoni, lakini utofauti wake ni kwenye dau na muonekano, Super Heli UNARUSHA ndege ya helikopta kisha itakupa bonasi za kasino kibao.

Super Heli mchezo kutoka Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet unakufanya kuwa tajiri, cha kwanza dau lake ni kuanzia Tsh 100/= lakini pesa hii ina maajabu makubwa ambayo huwezi kuamini imetajirisha wengi ambao wamechagua kucheza huu mchezo. Jisajili hapa ili ufurahie maajabu ya Super Heli Kasino.

Zawadi na Ushindi.

Super Heli mchezo wa kasino mtandaoni kutoka kwa Expanse Studios. Katika mchezo huu, utapata bonasi za kasino kubwa. Kuna malipo ya pesa taslimu papo hapo.

Wachezaji bora wakati wa promosheni ya Super Heli watapokea zawadi zifuatazo kutoka Meridianbet:

        Nafasi ya 1 - Samsung TV inchi 55.

        Nafasi ya 2 - Samsung A24.

        Nafasi ya 3 na ya 4 - TZS 200,000 beti za bure.

        Nafasi ya 5-6 - TZS 100,000 beti za bure.

        Nafasi ya 7-10 - TZS 50,000 beti za bure.

NB: Jisajili na Meridianbet na cheza michezo ya kasino ya mtandaoni upate ushindi kirahisi, Pia ongeza maokoto yako kwa kubashiri michezo mbalimbali yenye ODDS KUBWA. PIGA *149*10# AU tembelea tovuti yao meridianbet.co.tz

Spika Mstaafu na Mbunge wa Kongwa, Job Ndugai (wapili kulia)Mbunge wa Bahi,Kenneth Nollo na Mbunge wa Mpwapwa,George Malima wakikabidhiwa mtungi wa gesi na Meneja Masoko na Mawasiliano wa Lake Energies Group,Matina Nkurlu(kulia)ikiwa ni ishara ya Uzinduzi wa kampeni ya”Kumtua Mama kuni kichwani”iliyozinduliwa na kampuni hiyo kwa kushirikiana na Wakala wa nishati vijijini(REA) yenye lengo la kusambaza mitungi ya gesi 13,500 kwa mikoa ya Dododma,Mwanza,Geita,Morogoro na Arusha, Ikiwa na lengo la utunzaji mazingira kwa kupunguza kama si kutokomeza kabisa utumiaji wa nishati ya kuni na mkaa nchini.
Kutoka shoto Mbunge wa Bahi,Kenneth Nollo, Mbunge wa Mpwapwa,George Malima, Spika Mstaafu na Mbunge wa Kongwa, Job Ndugai pamoja na Meneja Masoko na Mawasiliano wa Lake Energies Group,Matina Nkurlu wakionesha mitungi ya gesi mara baada ya kuzindua rasmi kampeni ya”Kumtua Mama kuni kichwani”iliyozinduliwa na kampuni ya Lake Energies kwa kushirikiana na wakala wa nishati vijijini(REA) yenye lengo la kusambaza mitungi ya gesi 13,500 kwa mikoa ya Dododma,Mwanza,Geita,Morogoro na Arusha, Ikiwa na lengo la utunzaji mazingira kwa kupunguza kama si kutokomeza kabisa utumiaji wa nishati ya kuni na mkaa nchini.

 NA MWANDISHI WETU


MAKUMI elfu ya akina mama na familia zao wa mikoa mitano ya Dodoma, Morogoro, Mwanza, Arusha na Geita, watanufaika na kampeni iliyozinduliwa jijini Dodoma na kampuni ya Lake Energies Group iliyopewa jina la ‘Tumtue Mama Kuni Kichwani’ kwa kuwagawia mitungi 13,500 ya gesi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo jijini Dodoma leo Septemba 1, 2023, Meneja Masoko na Mawasiliano wa Lake Energies Group, Matina Nkurlu, alisema kuwa uamuzi wao huo umelenga kuunga mkono jitihada za Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan za utunzaji mazingira kwa kupunguza kama si kutokomeza kabisa utumiaji wa nishati ya kuni na mkaa.

“Lake Energies tumeona ni vema kuunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA), katika kampeni ya utunzaji mazingira kwa kupunguza kama si kutokomeza kabisa utumiaji wa nishati ya kuni na mkaa na tayari tumeshasambaza mitungi katika mikoa ya Arusha, Morogoro, Mwanza na Geita.
.
“Pia, kampeni hii inalenga kumwondolea mwanamke wa kitanzania adha ya kutumia muda mwingi kwenda kutafuta kuni au mkaa wa kupikia na hivyo kuepukana na hatari za huko maporini na badala yake kupata muda mwingi wa kutunza familia na ndoa zao,” alisema Nkurlu.

Akizungumza kwa niaba ya wabunge wenzake ambao majimbo yao yamehusishwa katika kampeni hiyo, Mwenyekiti wa Wabunge Mkoa wa Dodoma, Mheshimiwa Job Ndugai, aliishukuru Lake Energies kwa mpango wao huo, akiyataka na makampuni mengine kuiga mfano huo wa kumuunga mkono Rais Samia.

“Kwa niaba ya wabunge wenzangu wa Mkoa wa Dodoma, tunawashukuru sana Lake Energies kwa uamuzi wenu huu wa kuamua kugawa mitungi ya gesi kwa akina mama wa mkoa wetu kwa kushirikiana na serikali yetu.

“Kama ilivyo kwa mikoa mingine, akina mama wa Dodoma wamekuwa wakitumia muda mwingi kwenda kutafuta kuni za kupikia hali inayowachosha, lakini pia ikichangia kwa kiasi kikubwa uharibifu wa mazingira. Tunawashukuru sana,” alisema Ndugai ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Kongwa.
Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Geita, Joseph Musukuma, alisema kuwa msaada huo umekuja wakati mwafaka ambao Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, imeonekana kuwajali mno wanawake wa Tanzania kwa kuwapunguzia kama si kutokomeza baadhi ya kero zinazowakabili, ikiwamo ya kutumia muda mwingi kutafuta kuni na mkaa wa kupikia.

“Kwa niaba ya wanawake wa Jimbo langu la Geita, tunawashukuru sana kwa kutufikiria katika kampeni yenu hii, Mungu awabariki sana,” alisema Musukuma.

Naye mwakilishi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Injinia Michael Kyessi, aliitaka jamii ya watanzania kubadilika kwa kugeukia katika matumizi ya gesi kwa kupikia na shughuli nyinginezo zinazohitaji nishati ya moto badala ya kuni na mkaa.

“Ukataji miti umekuwa chanzo kikubwa cha uharibifu wa mazingira nchini, hivyo tunawashauri wanawake na watanzania kwa ujumla, kugeukia katika matumizi ya gesi badala ya kuni na mkaa kama sehemu ya kuunga mkono jitihada za serikali yetu ya Rais Samia Suluhu Hassan kupitia kampeni ya ‘Kumtua Mama Kuni Kichwani’.

“Wanufaika wa mitungi hii 13,500 katika mikoa ya Dodoma, Arusha, Morogoro, Geita na Mwanza, wakawe mabalozi wa wenzao katika maeneo yao kuhakikisha jamii inaachana kabisa na matumizi ya nishati ya kuni na mkaa,” alisema.

Mbali ya bidhaa ya gesi, Lake Energy Group wanajishughulisha pia na uuzaji na usambazaji wa petrol, dezeli, mafuta vilainishi ya mashine, nondo na bidha nyinginezo pamoja na kutoa huduma ua usafirishaji wa bidhaa mbalimbali

Kampuni ya Meridianbet kila iitwayo siku hufikiria watafanyanini kwaajili ya kuwaunga mkono wanaanchi ambapo hii leowamefika eneo la kawe ambapo linapatikana jeshi la polisi nakuweza kutoa Reflector kwa polisi wa usalama barabarani, hukuRefletor hizo zikipokelewa na mkuu wa kitengo hicho SP-ShattaOCD ndiye aliyepokea vifaa hivyo.

Meridianbet hurudisha kile kidogo wakipatacho kwenye jamiihuku wakielewa umuhimu wao na mahitaji yao kila siku hukusafari hii waliamua kuwamulika polisi Kawe huku wakijua kuwavitawasaidia kwenye shughuli zao za kila siku.

Baada ya kupokea Reflector hizo ASP Rose Maira amesema;"Niwashukuru wenzetu wa Meridianbet kwa kutuletea msaadahuu utakaosaidia Askari katika kutimiza majukumu yao bilauoga hata usiku kwa sababu watakua wanaonekana, katikakuelekea kilele cha wiki ya nenda kwa usalama barabaranimsaada huu umekuja muda muafaka".
Mkuu wa kitengo cha Masoko na mawasiliano Meridianbet Martina Nkurlu amesema kuwa “Tulikuja wiki iliyopita hapakutoa Reflector kwa bodaboda lakini tukaona hata Askari wetuwa usalama barabarani wana changamoto hii, leo tukaamua nawao kuwaletea msaada huu tukiamini katika juhudi zao za kulinda usalama barabarani katika Serikali hii ya Jamhuri yaMuungano wa Tanzania”

Meridianbet wababe wa odds kubwa na kasino ya mtandaoniwaliwatembelea jeshi la Polisi Kawe na kuwapa Reflector kwaajili ya matumizi yao wakiwa barabarani.

Ukiwa na meridianbet unaweza kubashiri mubashara, tembelea maduka ya meridianbet uweze kucheza michezo yasloti na kasino ya mtandaoni.

Beti na Meridianbet mechi za ligi zote, odds ni kubwa sana, usikose pia Kasino ya mtandaoni ya Meridianbet yenyemichezo rahisi ya sloti kama Poker, Aviator, Roulette.

NB: Habari njema kwako, Meridianbet imesikiaombi la wengi imekuja na Jackport kubwa ya mechi 13 kwa dau dogo la kuanzia 1,000/=TZS mshindiatajinyakulia donge nono la Tsh 85,000,000/= PIGA *149*10#



Baada ya kutunukiwa tuzo ya mshindi wa kwanza ya Mlipa Bora na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) katika kilele cha Wiki ya Mlipa Kodi iliyomalizika hivi karibuni,Wafanyakazi wa Mgodi wa Twiga Minerals wa Barrick North Mara, wamepokea taarifa hiyo kwa furaha na kulipokea kombe la ushindi lilipowasili mgodini hapo.


Twiga Minerals Corporation, inasimamia shughuli za: Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu mkoani Shinyanga; Mgodi wa Dhahabu wa North Mara uliopo Tarime– pamoja na Mgodi wa Dhahabu wa Buzwagi (Pangea) ambao pia upo Shinyanga ambao kwa sasa uko katika hali ya kufungwa.


Mnamo mwaka wa 2020, Twiga Minerals Corporation ililipa kodi ya mapato kiasi cha dola milioni $119, ambapo mwaka 2021, ililipa dola milioni $96.


Mapema mwaka huu, Wizara ya Madini iliitambua Twiga kama mchangiaji mkubwa wa mapato ya serikali kwa mwaka 2021. Kampuni yake tanzu - North Mara Gold Mine pia ilishinda tuzo ya Mshindi wa Kwanza miongoni mwa Wamiliki wa Leseni Maalumu za Uchimbaji katika Utekelezaji sera ya ushirikishwaji wazawa katika mnyororo wa uchumi wa madini (Local content) kwa mujibu wa Sheria ya Madini kifungu namba 123 mnamo mwaka 2021.


Akitoa taarifa ya utendaji wa kampuni katika kipindi cha robo mwaka kwa vyombo vya habari mwezi Oktoba, Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Barrick Gold Corporation Dk, Mark Bristow, alisema kuwa Twiga imechangia kwa zaidi ya dola bilioni 2.187 katika uchumi tangu mwaka 2019. Kati ya hizo, dola milioni 878 zililipwa katika mfumo wa ushuru na kodi mbalimbali za Serikali.
Kuhusiana na kusaidia biashara za ndani, Dk. Bristow alisema kuwa asilimia 80% ya manunuzi yenye thamani ya kiasi cha dola bilioni $ 1.025 yalikuwa ya bidhaa za ndani.

Baadhi ya Wafanyakazi wa Mgodi wa Barrick North Mara wakifurahia tuzo

Baadhi ya Wafanyakazi wa Mgodi wa Barrick North Mara wakifurahia tuzo

Baadhi ya Wafanyakazi wa Mgodi wa Barrick North Mara wakifurahia tuzo





 

 


 Mwindaji pekee wa kike kutoka TACHA Bi. Fina Felix akipokea cheti cha kufuzu mafunzo ya umiliki na utumiaji wa silaha kutoka kwa ASP Hamis Luyeko (kushoto.)
ASP  Hamis Luyeko akizuungumza wakati wakufunga mafunzo hayo amewapongeza TACHA kwa kuonesha nidhamu kwa jeshi la polisi na kuwataka watanzania kujiunga na chama hicho.


 

CHAMA cha Uhifadhi na Uwindaji Tanzania (CHATA,) kimeiomba Serikali kutoa leseni za umiliki wa silaha kwa wanaopata mafunzo na kutunukiwa vyeti ili waweze kutumia silaha hizo kwa umahiri zaidi bila kudhuru wanyama na raia.

Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Chama cha Uhifadhi na Uwindaji Tanzania (CHATA,) Kanali Thomas Ndonde (rtd) mara baada ya kufungwa kwa mafunzo ya siku mbili ya kuwajengea uwezo, umahiri na kujiamini zaidi katika matumizi ya silaha yaliyofanyika katika viwanja vya Shabaha jijini Dar es Salaam na kueleza, chama hicho kimekuwa kikihakikisha wanachama wanapata mafunzo na wanaofanya vizuri wanapata vyeti vinavyotolewa na jeshi la polisi.

‘’TACHA inajumuisha wawindaji wenyeji wanaofanya shughuli za uwindaji kwa kufuata sheria na miongozo ya uwindaji kwa kuzingatia matakwa ya Serikali….Na mafunzo haya ni ya lazima kwa mujibu wa sheria tunalishukuru jeshi la polisi kwa kutoa mafunzo haya ya nadharia na vitendo kwa siku mbili na kutunuku vyeti na  tutakaguliwa kwa kipindi cha miaka mitano ili kujenga ufanisi zaidi .’’ Amesema.

Pia ameishauri Serikali kutoa leseni kwa raia waliopata mafunzo na kupata vyeti ili waweze kutumia silaha zao bila kudhuru wanyama na raia na kuwataka watanzania kujiunga na TACHA ili waweze kupata mafunzo hayo.

Awali mkufunzi wa mafunzo hayo ASP Hamis Luyeko alikipongeza chama hicho kwa kuonesha nidhamu kwa Jeshi la Polisi na kufanikisha mafunzo hayo na kuwataka raia kujiunga na TACHA ili waweze kupata mafunzo, leseni na vibali vingine vinavyohusu silaha.  

Kwa upande wake Mratibu msaidizi wa  Umahiri wa Utumiaji na Utunzaji wa Silaha za moto za Kiraia nchini kutoka Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Polisi Tanzania (TPFCS,) Ravent Vedasto ameipongeza TACHA kwa kuhakikisha kila mwanachama anapata mafunzo hayo ambayo ni kwa mujibu wa sheria ya The Firearms and Ammunition Control Act ya mwaka 2015.

‘’Ni lazima kwa wamiliki wa silaha kupata mafunzo haya na kupatiwa vyeti, hadi sasa raia wapatao 5000 wamepata mafunzo haya na kwa miezi mitatu kuanzia Julai mwaka huu hadi Oktoba raia 2000 wamepata mafunzo…mpango ni kuwafika nchi nzima kwa zoezi hili ifikapo 2025/2026.’’ Amesema.

Amewataka raia kujiunga na TACHA ili waweze kupata mafunzo hayo muhimu ya kuwajengea uwezo, umahiri na kujiamini zaidi na kupatiwa vyeti mara baada ya kuhitimu mafunzo hayo.

Mwindaji pekee wa kike kutoka TACHA ambaye amefuzu vyema katika mafunzo hayo kwa kupata alama za juu na kukabidhiwa cheti Bi. Fina Felix amesema, amejifunza uwindaji akiwa mdogo kutoka kwa familia yake na amekuwa mahiri katika uwindaji licha ya jamii kuona fani hiyo ni ya wanaume.

‘’Wanawake tunaweza kufanya kila kitu, nitoe wito kwa wanawake wengi zaidi kujifunza fani hii na kuifanya kazi hiyo kuwa sehemu ya kujiingizia kipato.’’ Amesema.

Kwa upande wake mwakilishi wa kampuni ya Orxy ambao wamedhamini mafunzo hayo Gracious Matunda amesema udhamini huo unakwenda sambamba na kampeni ya utunzaji na uhifadhi wa mazingira kwa wawindaji na wananchi kwa ujumla na wanahahimiza kutumia nishati ya gesi kwa kupikia kwa gharama nafuu na salama zaidi na kuacha kukata miti ili kutunza mazingira na kuepuka na mabadiliko ya tabia Nchi yanayoleta athari mbalimbali ikiwemo ukame.











mafunzo yakiendelea.
Mwakilishi wa kampuni ya Orxy ambao wamedhamini mafunzo hayo Gracious Matunda akizungumza mara baada ya kufungwa kwa mafunzo hayo na kueleza kuwa udhamini huo unakwenda sambamba na kampeni ya utunzaji na uhifadhi wa mazingira kwa wawindaji na wananchi kwa ujumla na wanahahimiza kutumia nishati ya gesi kwa kupikia kwa gharama nafuu na salama.




 

 

 

 

 

 



Mkurugenzi wa Manunuzi Benki ya CRDB, Pendason Philemon (watatu kulia) na Moureen Mollel, Meneja Mipango ya Biashara Benki ya CRDB (wapili kushuto) pamoja na viongozi wengine waandamizi wa benki hiyo katika picha ya pamoja wakionyesha tuzo ya Benki Bora katika kipengele cha Huduma kwa Wateja (Most Preferred Domestic Bank at Customer Service) na tuzo ya Huduma Bora za Kidijitali katika Sekta ya Benki (Most Advanced Digital Banking Services) Afrika Mashariki ambazo benki hiyo imetunukiwa katika hafla ya tuzo za Consumer Choice Awards zilizofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jana Novemba 12, 2022. Hii ni mara ya pili mfululizo kwa Benki ya CRDB kushindo tuzo hizo zinazotokana na maoni ya wateja/ watumiaji wa huduma.
Mkurugenzi wa Manunuzi Benki ya CRDB, Pendason Philemon (kulia) akipokea tuzo ya Huduma Bora za Kidijitali katika Sekta ya Benki (Most Advanced Digital Banking Services) Afrika Mashariki kutoka kwa Mkurugenzi wa Biashara na Masoko Vodacom, Linda Riwa katika tuzo zako Consumer Choice Awards zilizofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jana Novemba 12, 2022. Katika tuzo hizo Benki ya CRDB pia ilitunukiwa tuzo ya Benki Bora katika kipengele cha Huduma kwa Wateja (Most Preferred Domestic Bank at Customer Service).
Mkurugenzi wa Manunuzi Benki ya CRDB, Pendason Philemon (kulia) akipokea tuzo ya Benki Bora katika kipengele cha Huduma kwa Wateja (Most Preferred Domestic Bank at Customer Service) kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kilombero Sugar, Guy Williams katika tuzo za Consumer Choice Awards zilizofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jana Novemba 12, 2022. Katika tuzo hizo Benki ya CRDB pia ilitunukiwa tuzo ya Huduma Bora za Kidijitali katika Sekta ya Benki (Most Advanced Digital Banking Services) Afrika Mashariki.

=====  ======   ======

Benki ya CRDB imeendelea kudhihirisha kuwa benki bora na kinara nchini kwa kutunikiwa tuzo mbili za umahiri katika sekta ya fedha nchini katika tuzo za Consumer Choice Awards zilizofanyika jana Novemba 12, 2022 katika ukumbi wa mikutano wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam.

Tuzo ilizotunukiwa Benki ya CRDB ni ile ya tuzo za Huduma Bora za Kidijitali Afrika Mashariki, pamoja na Huduma Bora kwa Wateja. Hii ni mara ya pili mfululizo kwa Benki ya CRDB kushindo tuzo hizo zinazotokana na maoni ya wateja/ watumiaji wa huduma.

Akizungumza wakati wa kupokea tuzo hizo, Mkurugenzi wa Manunuzi Benki ya CRDB aliwashukuru wa wateja, washirika, wadau wa benki hiyo, pamoja na Watanzania wote kwa kuendelea kuifanya Benki ya CRDB kuwa bora zaidi.

"Tunawashukuru sana kwa kuendelea kutufanya kuwa bora zaidi. Ahadi yetu ni kuendelea kuwa wabunifu katika huduma zetu ili kusaidia kuboresha maisha ya Watanzania," alisema Pendason.

Katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, Benki ya CRDB imefanya mageuzi makubwa ya kimkakati katika biashara yake ambayo yamepelekea kupata matokeo mazuri kiutendaji, ikiwa ni pamoja na uboreshaji wa huduma, na ukuaji wa faida.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB amewashukuru wateja, wanahisa na wawekezaji wa Benki hiyo kwa kuifanya benki hiyo kuendelea kuwa bora zaidi.

Mwaka 2022 umekuwa wamafanikio makubwa kwa Benki ya CRDB hivi karibuni benki hiyo inetunukiwa tuzo mbili za ‘Benki Bora Tanzania kwa na majarida maarufu ya fedha na uchumi duniani ya Euromoney na Global Finance kutambua umahiri wake katika kuongeza ujumuishi wa kifedha katika ukanda wa Afrika Mashariki na kuboresha maisha ya watu.

Pendason ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuboresha mazingira ya biashara nchini akibainisha hiyo pia imekuwa chachu ya Benki ya CRDB kufanya vizuri.
Monday 24th October, Dar es Salaam: Delegates from the United States of America (USA) have arrived in Dar es Salaam, Tanzania for a trade mission organized by Equity Bank Tanzania in collaboration with the East African Business Council, Minnesota Africans United, Global Minnesota and Prosper Africa, a U.S. 

Government initiative that connects U.S. and African businesses with new buyers, suppliers, and investment opportunities. The trade mission will see at least 10 foreign delegates representing various institutions in corporate America engage with over 500 local entrepreneurs, MSMEs and corporates through organized panel discussions, one on one business networking sessions and site visits to businesses in Dar es Salaam and Zanzibar and thereafter proceed to Kenya for a similar engagement.
Mr. Raphael Onyango, Equity Group Director, Corporate Banking.

Earlier this year, Equity Group launched the Africa Recovery and Resilience Plan, a socio-economic transformation plan that Equity has seeded with a USD 7 billion fund with the aim of impacting 100 million people within the African continent through its financial and social impact initiatives and reaching 5 million MSMEs and 25 million individual customers, to create 50 million jobs.

The robust Plan has seen the Group champion investments by private sector in the agricultural and extractive sectors, manufacturing and logistics, trade and investment, the MSME sector, social and environmental transformation and the promotion of a technology-enabled economy in order to support financial empowerment and wealth creation. 
Danford Muyango, Senior Manager Institutional Business

This trade mission is among the many initiatives that the Group through its regional banking subsidiaries in 6 countries has put in place to accelerate the implementation of the Africa Recovery and Resilience Plan and to champion the sustainable building back better of the African continent post the COVID-19 pandemic. 

Speaking at the official launch of the trade mission, Tanzania Private Sector Foundation (TPSF) Director Policy Advocacy and Membership Management, Outreach and Capacity Building, Zachy Mbenna said, “We extend a warm and cordial welcome to the visiting delegates from the USA and the local private sector players and look forward to positive engagements that will lead to business realization. Our interactions during this trade mission are critical as this will enhance knowledge exchange enabling us to meet the needs of the immediate market and the global trends in consumer behaviour.” 

The TPSF Director also urged the attending delegates to explore Tanzania for investment areas and tap into agriculture and logistics with additional investment opportunities in tourism, the MSME sector and mining. Also speaking at the official opening ceremony in Dar es Salaam, the American Chamber of Commerce in Tanzania Board Member Burak Buyuksurac said, “As the American Chamber of Commerce in Tanzania, we are excited to be here today and appreciate the efforts by Equity to organize this great trade mission. We believe that this will lead to the creation of more business opportunities between Tanzania, Kenya and the USA.” 
Mr. Octavian Mshiu, CEO - Open Group of Companies and Board Director, TPSF

The visiting delegates have come as a group through Minnesota Africans United, Global Minnesota and Prosper Africa and are keen on working with local businesses to either set up shop in Tanzania or sign export/import agreements for local materials and finished goods. Equity Bank Tanzania Managing Director Isabela Maganga said, “Investment in trade will not only empower our people but will also build our economy. 

A growing economy means improved lives and livelihoods. Tanzania has massive potential in agriculture, manufacturing, mining, energy, tourism, transport and logistics among many other sectors. 

Equity Bank is partnering with its customers and the people of Tanzania to create value from these vast resources by bringing awareness to the opportunities in Tanzania.” She also added that over the next 7 days, the international delegates will experience Tanzania by visiting key SMEs and corporates which will play a central role in helping them to understand the opportunities within the market, the policies and regulations that govern operation, the fiscal policies and financial solutions available at their disposal through Equity Bank. 

Sultan Abdalla, General Manager, Galco Limited & GSM Group

This trade mission follows the Kenya-DRC Trade Mission that was organized by EquityBCDC in the DRC which saw over 300 Kenyans travel to the DRC to explore investment opportunities in November 2021 and builds on the White House visit of Her Excellency President Samia Suluhu Hassan’s visit to the United States in April of this year. 

Raphael Onyango Equity Group Director Corporate Banking said, “Equity as a pan-African bank has purposed to champion the build back better of the African continent through implementing the Africa Recovery and Resilience Plan. This trade mission to Tanzania and Kenya will capacitate, coordinate and champion business connections between USA and Tanzania and Kenya.”

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC,) Nehemia Mchechu akizungumza na Chama cha Wafanyabiashara Afrika Kusini katika kikao kilichowakutanisha kwa lengo la kujadili fursa za uwekezaji katika sekta ya nyumba, Mchechu amesema NHC itaendelea kulitangaza shirika hilo ili kuvutia wawekezaji wakubwa na wadogo kutoka ndani na nje ya nchi.
 

SHIRIKA la Nyumba la Taifa (NHC,) limekutana na Chama cha Wafanyabiashara cha Afrika Kusini na kwa lengo la kuwaeleza nini NHC inafanya na fursa lukuki za uwezekaji zinazopatika kupitia shirika la  nyumba nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kikao hicho kilichofanyika jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC,)  Nehemia Mchechu amesema, NHC inaamini katika uwekezaji wa ndani na nje na uchumi mzuri wa Afrika Kusini unahitaji uwekezaji mkubwa ikiwemo katika sekta ya nyumba kwa nchi kama Tanzania ili azma ya kuwa na makazi bora kwa wananchi ifanikiwe kwa kiwango kikubwa zaidi sambamba na kutengeneza ajira  kwa watanzania.

 Mchechu amesema, kupitia kampeni ya 'Royal Tour' iliyozinduliwa na Rais Samia Suluhu Hassan NHC itaendelea kutembea nayo na kulitangaza shirika hilo ili kuvutia wawekezaji wakubwa na wadogo kutoka ndani na nje ya nchi.

''Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa akielekeza na kusisitiza umuhimu wa sekta binafsi katika kuchangia maendeleo ya Nchi…Sekta binafsi ndiyo itafanya biashara na serikali itabakia kusimamia sera za kuwajengea mazingira rafiki wawekezaji ikizingatiwa kuwa, hapa nchini kuna fursa muhimu za kibiashara ikiwemo uongozi imara.’’ Amesema Mchechu.

 Akieleza mipango ya NHC Mchechu amesema kwa mwaka huu wa fedha shirika hilo litatumia  Bilioni 413.7 kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa nyumba katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo utekelezaji wa mpango wa ujenzi wa nyumba kwa wananchi wa hali ya chini na kati ambapo nyumba 5000 zitajengwa kupitia mpango  wa Samia Housing Scheme (SHS.)

''Mradi huu wa nyumba za kuuza na kupangisha nyumba wa SHS, umelenga  kuenzi kazi nzuri anazofanya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan katika kuletea maendeleo na tunatamani watanzania  wamkumbuke kwa jitihada hizo baadaye.’’ Amesema.

Amesema kuwa asilimia 50 ya nyumba hizo zitajengwa jijini Dar es Salaam,  asilimia 20 Dodoma na mikoa mingine ya Tanzania asilimia 30 na kwa Mkoa wa Dar es Salaam ujenzi wa nyumba 500 zitajengwa kuanzia mwezi Septemba mwaka huu  katika eneo la Kawe na Medeli jijini Dodoma nyumba 100 zitajengwa.

 Mchechu pia ameushukuru   Ubalozi wa Afrika Kusini Nchini Tanzania kwa kuendelea kushirikiana na  kuwashirikisha fursa za uwekezaji zilizopo Tanzania wawekezaji kutoka Afrika Kusini.

Akieleza mikakati ya NHC Mchechu amesema, Shirika linapanga utekelezaji wa miradi mipya ya sekta ya nyumba pamoja na mpango wa kushirikiana na sekta binafsi utakaozinduliwa mwezi huu pamoja na kutekeleza miradi mipya ya makazi katika jiji la Dar es Salaam itakayowanufaisha wananchi wa hali zote pamoja na kumalizia miradi ya kimkakati iliyokwama kutokana na sababu mbalimbali.

 Pia amesema, miradi ya ujenzi wa nyumba katikati ya jiji la Dar es Salaam ikiwemo Kawe, Kinondoni, Mchikichini, Temeke utatekelezwa na shirika hilo kwa kushirikiana na sekta binafsi na ujenzi huo utajibu changamoto za makazi, biashara na watanzania wataishi  na kuweza kununua nyumba hizo kwa gharama nafuu, na watakaopewa kipaumbele katika makazi hayo ni wakazi waliokuwa wakiishi hapo na wananchi wengine wenye uhitaji.

Aidha amesema kuwa NHC mejipanga katika kufanya mageuzi makubwa katika sekta ya nyumba na watakutana na   waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali nchini wakiwa kiungo muhimu na kueleza mikakati ya sekta ya nyumba.

 Mkurugenzi wa Chama cha Wafanyabiashara wa Afrika Kusini wanaofanya biashara na kuwekeza nchini Manish Thakra akizungumza katika kikao hicho.

Vilevile Mkurugenzi wa Chama cha Wafanyabiashara wa Afrika Kusini wanaofanya biashara na kuwekeza nchini Manish Thakrar amesema, NHC imetangaza fursa nyingi ambazo wameona ni vyema washiriki fursa hiyo ya uwekezaji hasa katika miradi ya sekta ya nyumba za makazi.

Ameeleza NHC imeonesha miradi ambayo nchi yoyote duniani inaweza kuwekeza na ushirikishwaji wa sekta binafsi unaofanywa na NHC utaleta matokeo chanya katika kutatua changamoto ya makazi kwa wananchi hasa katika maeneo ya miji na kuzitaka nchi za Afrika kuiga mfano huo kwa utekelezaji na kuja kuwekeza katika ardhi ya Tanzania ambayo mazingira yake yana tija kwa manufaa ya biashara na jamii.