Kaka Issa,
kwanza nakushukuru saaaaaaana kwa kazi nzuri unayofanya. Mimi ni msomaji mzuri wa blog yako na kwa kweli ndiyo nnayoitegemea zaidi kunipatia habari za nyumbani. Kwa kweli nilisikitishwa sana na makosa ya operesheni yaliyotokea katika hospitali ya MOI.
Hata hivyo hayakunishangaza kwani madaktari na wauguzi ni wanadamu na makosa hutokea. Pamoja na kwamba kulingana na unyeti wa kazi yao makosa yanapotokea ni uhai wa mtu mashakani.

Huku niliko Minnesota imetangazwa kwenye taarifa ya habari madaktari wamefanya upasuaji na kumtoa mgonjwa figo nzima badala ya iliyokuwa na ugonjwa wa saratani. Walipoipeleka kwa uchunguzi ndipo ikagundulika haikuwa na tatizo lolote na badala yake yenye tatizo ndiyo iliyoachwa.

Si kwamba natetea lililotokea MOI bali nataka kuonyesha tu hata huku kwenye nchi kubwa zenye vifaa, utaalamu na mpangilio wa kazi makosa yanatokea.
Habari zaidi kuhusu tukio hili linapatikana hapa http://www.kare11.com/news/news_article.aspx?storyid=501880


Tuchukuliane mizigo kwa upole.

Mdau

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Wewe Mdau hujasema ukweli. Hao walikosea tokea wanapopima badala ya kuweka alama kwenye Figo mbovu waliweka alama kwenye figo iliyonzima. Kwa hiyo madaktari walivyokuja kutoa walitoa ile ilikuwa na alama ambayo haikuwa sahihi. Kwa hiyo hapo lawama ni za watu wa chini nyie CNA sio madaktari.

    ReplyDelete
  2. What is real your point? Tatizo sio kutokutokea kwa makosa, tatizo ni jee waliofanya makosa wanatake responsibility? Au inakuwa hardball. Sio Michigan tuu kwenye hayo matatizo, all over usa yanatokea. Sema people learned from that mistake, new research zinafanywa kuboresha healthcare.

    ReplyDelete
  3. ASANTE KWA KUHALALISHA UZEMBE ULIOTOKEA MOI.

    ReplyDelete
  4. Hata hapa UK kumekuwa na makosa yanatokea mara kwa mara kwenye hospitals. Wakati mie najifungua kuna mwanamke alichomwa sindano ambayo ni ya kuwatuliza wagonjwa wa akili. Lengo ilikuwa achomwe epidural ambayo ni ajili ya kupunguza uchungu. Haijulikani dawa hiyo ilifikaje labour ward na nani aliyeileta. Yaelekea hata Doctor incharge hakufanya kazi yake ipasavyo kwani ndiye anaye kagua na ku-sign dawa zinazotolewa. Mama wa watu alikufa muda si mrefu kabla hata hajajifungua. Na sio wa kwanza, kuna mwanamke mwingine mwaka juzi alikufa hospital hiyo hiyo kwa kuchomwa sindano ambayo hakupaswa kuchomwa.
    Uzembe upo hata huku

    ReplyDelete
  5. Jamani tuacheni kujustify mambo ya hospital za marekani na muhimbili . Kama alivyo sema huyo anon wa pili kutoka juu "waliofanya makosa wanatake responsibility". Sasa muhimbili iko tayari kuchukua mzigo huo ? Kuhakikisha kuwa huyo mtu aliekosea anasaidiwa mpaka mambo yarekebishwe na anasaidiwa kaitka kila hali ili maisha yake ya rudi kawaida? Kama yule kaka aliye lemaa anaangaliwa bado na muhimbili ..anaenda physical therapy ? ana wheel chair ana vifaa vingine vingi vya kusaidia kurahiziha maisha yake ya ulemavu ? Na hatua gani zinachukuliwa kuhakikisha hili jambo halitokei tena ???
    afisa wa Afya, Md

    ReplyDelete
  6. Two wrong doesn't make it right.....Mwenzetu huyo atalipwa na ndugu zake wataishi vizuri hao wa bongo wao ndugu waliokua wanamtegemea niaje...

    Na kwani USA ndio Mungu basi kwa vile wao wanafanya makosa basi it is okay...IT is not okay Kosa ni Kosa

    ReplyDelete
  7. waosha vinywa tu wabongo , madaktari wetu wanafnaya kazi nzuri ,kama ni wabaya mbona bado mnaenda hapo MOI na panajaa, sio unafiki huo je mna ujanja wa kwenda ulaya kutibiwa nyie mnapenda kutoa rushwa zikiwaumiza mnalia ,nani alimuambia huyo mgonjwa atoe rushwa wakati alisharuhusiwa si laaana zake tu hizo sasa mungu kamlipa mnalia
    mtaosha vinywa saaana lakini mkiumwa mtajongea kwa madaktari

    ReplyDelete
  8. waosha vinywa tu wabongo , madaktari wetu wanafnaya kazi nzuri ,kama ni wabaya mbona bado mnaenda hapo MOI na panajaa, sio unafiki huo je mna ujanja wa kwenda ulaya kutibiwa nyie mnapenda kutoa rushwa zikiwaumiza mnalia ,nani alimuambia huyo mgonjwa atoe rushwa wakati alisharuhusiwa si laaana zake tu hizo sasa mungu kamlipa mnalia
    mtaosha vinywa saaana lakini mkiumwa mtajongea kwa madaktari

    ReplyDelete
  9. ama kweli mtu unaweza kuwa umetawaliwa mawazo hata kama uko ulaya, yaani hii kitu sijui itaondoka lini kwa waafrka walio wengi, YAANI KITU HATA KIWE KIBAYA NAMNA GANI, 'HATA ULAYA KIPO'', KILA KITU HATA KIWE KIBAYA VIPI KINAHALALISHWA ETI KWA SABABU HATA ULAYA KIPO!!!! HUU NI UTUMWA WA MAWAZO, NDIYO SABABU MTAA MZIMA UNAWEZA KUKUTA MADUKA YOTE YANAUZA BIDHAA ZINAZOFANANA, HATA BLOG WENGI WANAANZISHA, kisa hata Muchuzi mbona anayo!!!!! jamani ifikie Muda hao wazungu watuige sisi, binadamu wote tu sawa.

    Nenda China fanyeni hivyo mnavyosema kama mtu hajanyongwa!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...