Wadau,
Hii ni shule ya Minaki iliyoko Kisarawe, shule hii inahistoria ya kutoawasomi wa mwanzo wa nchii hii, lakini sasa hivi imechakaa kama inavyoonekana. Nimesikia kuna ufadhili wa kuikarabati upya
Mdau Rhxoqsa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. HII NDIO SIFA YETU WATANZANIA.TWAJUA KUTUMIA TU BILA KU-MAINTAINS.HIVI VIONGOZI HAWAKUYAONA MAJENGO KAMA HAYO YALIPOKUWA YANAANZA KUONYESHA DALILI ZA KUHARIBIKA??? KWELI TWAYAANGALIA HADI YANAFIKIA KIWANGO HIKI. GHARAMA YA KUFANYA UKARABATI WAKE HAPO SI INAKUWA SAWA TU NA KUJENGA JENGO JIPYAA???. AMA KWELI TWAJUA KUFUJA!!!

    ReplyDelete
  2. WE MDAU ULISOMA MINAKI MIAKA YA 47 NINI??MANAKE HILO JENGO HALITUMIKI KWA MDA MREFU SANA TOKA MIAKA YA 80 MIMI NIMESOMA KUANZIA 1999-2002
    HILO JENGO ALIKUWA ANAKAA MKOLONI LAKINI MINAKI BADO IPO BOMBA TU KISHENZI:

    ReplyDelete
  3. Zamani walikuwa wanasema Tanzania hakuna culture ya 'Maintenance' tunajenga halafu tunaachia ijitunze eneyewe. Naona hakuna mabadiliko na tabia hii mbovu. Inasikitisha.

    Baba yangu, alisoma hapo enzi za mkoloni. Akikusimulia enzi hizo na walimu wakoloni doh, huwezi kuamini ni shule hiyo iliyokongoroka sasa.

    ReplyDelete
  4. Mimi ni minaki old boy 1999-2001,nadhani wa kwanza kuhusika katiak suala nzima la ukarabati au maintainence ni watu kama mimi na wengine walibahatika kupitia hapo, sasa sijui tutasaidiaje shule yetu. by the way hiyo ni relic la jengo la zamani sana na iliachawa kutumika long time.

    ReplyDelete
  5. Baba Yangu pia alisoma hapo hiyo shule bado mbona inaendelea vizuri tu. Minaki hilo jengo walikuwa wakikaa walimu wakikoloni lipo kama jengo tu la kumbukumbu.

    ReplyDelete
  6. Bro. Michuzi, hilo jengo ni la zamani sana. Lilikuwa hivyohivyo tangu nilipokuwa nikisoma hapo mwaka 1977 na 1978.

    ReplyDelete
  7. jirani wa libaba hapa kwa maana ya makongoro dweller!!! hilo jengo bora liake ivo ivo

    ReplyDelete
  8. Pamoja na mimi kulikuta hivyohivyo mwaka 1987-89, lakini nasikitika tunashindwa kutunza historia. Ni muhimu tukafikiria jinsi ya kuliweka katika mazingira mazuri bila kuathiri ualisia wake.

    ReplyDelete
  9. NI KWELI HILO JENGO NI LA ZAMANI SANA ! NIMEKUWA NIKIPITA HAPO TANGU MWAKA 1976 KAMA SIKOSEI PAKO HIVYO HIVYO ! LKN HAINA MAAANA KUPAACHA KAMA PALIVYO BUSARA NI KUPATENGENEZA ILI WENGINEO WAJAO WAONE KUMBUKUMBU YA NCHI YETU NZURI SANA ALIYOTUJALIA MWENYE ENZI ! BASI KAMA HALINA MAANA LIONDOLEWE KABISA SABABU UKIPITA PALE MINAKI LAZIMA UTAANZA LIONA HILO KWA KUWA LIKO BARABARNI KABISA ! NATUMAI WADAU WA PALE WIZARANI ELIMU POLICY AND PLANNING MTAPATA UJUMBE NA HASA HII HARAMBEE ILIOANZISHWA YA KUWAKILISHA PICHA ZA MAJENGO YA SHULE ZA ZAMANI HAPA KWETU ITATUPA HAMASA KUBWA YA KUSHAWISHI AU KUWAKUMBUSHA WASHIKA DAU WOTE JUU YA KUYAENZI MAJENGO YENYE HISTORIA ILIYOPENDEZA NA VILE VILE JAMAA WA POLICY AND PLANNING WA WIZARA YA ELIMU WAONE MAJENGO YALIOJENGWA NA MKOLONI YALIVYOKUWA IMARA NA YAPO MPAKA LEO ! SIJUI HAYO MAJENGO YAO MAPYA MFANO WA MABANDA YA KUKU ATAFIKIA UMRI HATA WA MIAKA 30 ? TUENDELELEZE LIBENEKE.........
    Mzushi

    ReplyDelete
  10. Asante sana kaka michuzi umetukumbuka saana wadau wa minaki ni siku nyingi nimepita hapo kaka tulikuwa tunakaa hapo chini kusibiri costa za kutoka king tudrop town na kwa vibonde wetu pugu mkuu!! Mim Stephen Nyagonde A-LEVEL PCB mwaka 2004-2006 nilikuwa nalaa mnyampala, Hilo jengo kaka ni la kihistoria limejengwa na wakoroni so linaachwa kwa ajili ya ukumbusho na kwa taarifa kaka ilikuwa ofisi ya headmaster enzi hizo ikiitwa S.t Andrew mkuu na ilikuwa shule ya kwanmza kuwa A-level tanzania 1958 ni watu wengi saana wamepita hapo akiwepo John samwel malechela, daniel yona, makweta, mkuu wa majeshi mstaafu mwita waitara na wengineo wengi, wadau wangu Dr andrew lukwaro vp umeiona hii kutoka huko china ulipo, Alvin nkya huko america, Rajab kiaratu huko patrice lumumba russia, Joseph mwasambili muchs, Laurent mwakakonyole mzee wa pori,Emmanuel mabula, Ally maya, Bryan Andrew, luka mkeni, Magoti james, Isaya mwaisamila, Juma issah, eliakim kagimbo, Ntugwa nyorobi, Aman semi, Dr isack christopher- Muchs, Dr beno mbeya- muchs, chalres kimambo, pius mbeya, samiji mlemba na masela wengine kibao wa EGM Emma Mlay, Christian christopher, Jeromin patrice manamuona michuzi analonga nini? Na kwa taarifa yenu wakuu kaka David silinde ni mpiganaji mkubwa balaa ndani ya chuo kikuu Dar es salaam toka pori mpaka upiganaji kweli anatisha tunamkubarianakaribia kuukwaa uraisi wa chuo! kaka Emanuel ndengerio mzee wa makongoro vipi huko Chech pamoja na Maxwell kishe maisha yanasonga huko!! Jamani mama kiyungai hayupo tena nasikia afande sogoi naye amehama mkuu!! Na mheshimiwa kaaya amechizi kaaamishiwa wizarani!! sasa wadau lazima tuform data base ya wana minaki tupigane kiume tuijenge shule yetu wakuu!! Mungu amrehemu headmaster wetu mpendwa Mjale alitulea!! Hio ndiyo minaki kaka michuzi formely S.t Andrew!!! tutaboresha hilo jengo lakini litaachwa hivyo hivyo kwa ajili ya historia na lita kuwa la kitalii zaidi!!Wadau lakini kuna umuhim wa kuiboresha shule yetu minaki yatupasa ma Alumin wote wa minaki tukutane tufanye corabo tunyanyue shule yetu!!!

    Stephen joseph nyangonde
    Department of zoology and wildlife
    University of Dar es salaam

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...