mabalozi wa zain wakila mikonozzzzz baada ya kukabidhiwa bendera zao za kazi
mkuu wa wilaya ya nanihii akikabidhiwa bendera yake ya kupererusha kila anapoenda kuwakilisaha zain
lady jd akipokea bendera yake
bosi wa masoko wa zain (corporate) constantine magavilla na mabalozi wa zain
meneja masoko (corporate) wa zain constatine magavilla akiwatangaza lady jd na mkuu wa wilaya ya nanihii kuwa mabalozi wa zain leo
gadna g. habasha na binti wa mkuu wa waliaya ya nanihii mamou wakiwapongeza lady jd na mkuu wa wilaya ya nanihii kwa kuwa mabalozi wa zain. chini bosi wa masoko (consumer) wa zain kelvin twissa akila pozi na lady jd, mkuu wa wilaya ya nanihii pamoja na mamou muhidin kwenye hafla hiyo
KAMPUNI YA SIMU ZA MKONONI YA ZAIN IMEWATANGAZA MKUU WA WILAYA YA NANIHII PAMOJA NA MSANII LADY JD KUWA MABALOZI WA ZAIN, KATIKA HAFLA ILIYOFANYIKA SASA HIVI MAKAO MAKUU YA KAMPUNI HIYO SEHEMU ZA KIJITONYAMA, MAJI MACHAFU, DAR.


Zain Yateua Mabalozi wa ‘One Network’

Dar es Salaam, September 12, 2008; Zain kampuni ya simu za mkononi inayoongoza katika nchi 22 Barani Afrika na Mashariki ya Kati imeteua na kutangaza mabalozi wa huduma yake ya One Network, ambayo ni huduma ya kwanza duniani kuondoa mipaka katika mawasiliano.
Zain iliweka historia katika sekta ya wawasiliano duniani ilipozindua huduma ya One Network kwa mara ya kwanza November 2006 ikitoa huduma katika nchi za Afrika Mashariki; Tanzania, Kenya na Uganda. Huduma hii sasa inapatikana katika nchi 16 katika Bara la Afrika na Mashariki ya Kati.
Katika mkutano na waandishi wa habari Meneja Masoko wa Zain Tanzania, Costantine Magavilla aliwatangaza mwanamuziki maarufu nchini Judith Wambura, anayefahamika kama Lady Jay Dee na Muhidin Issa Michuzi, mwandishi wa habari na mpiga picha mwandamizi kama mabalozi wa huduma ya Zain ya One Network kuanzia Ijumaa mwezi huu.
Lady Jaydee na Michuzi wameteuliwa kwa ajili ya mafanikio waliyonayo katika fani zao. Lady Jay Dee amekuwa katika fani ya muziki kwa kipindi cha miaka saba sasa na ni moja katika ya waimbaji wa kike wanaoongoza nchini kwa sasa. Lady Jaydee ambaye ameajiri watu 10 katika bendi yake, anatajwa kuwa msanii anayeongoza nchini kwa kushinda tuzo nyingi.
Aidha, Lady JayDee ameshinda Tuzo la Shirika la Utangazaji la BBC kwa kuwa na wimbo bora na ametumbuiza mara tatu mbele ya Rais Jakaya Kikwete. Lady JayDee ameteuliwa mara nne kushiriki katika Tuzo za Kora ambapo na mwaka huu atashiriki, vile vile Lady Jaydee ameshinda mara tatu Tuzo Bora ya muziki wa video inayotolewa na Channel O.
Michuzi kwa upande wake licha ya kuwa mwandishi wa habari na mpiga picha mwandamizi mwenye mafanikio pia amamiliki blog ambayo inaoongoza kwa umaarufu nchini ikisomwa na mamilioni ya watu wanaoishi ndani na nje ya Tanzania.
‘’Tunaamini kwa kushirikiana na Lady Jay Dee na Michuzi tutaweza kuwasisimua na kuwafikia watu wengi zaidi na kusambaza habari za huduma yetu kabambe ya One Network inayofanikisha upatikanaji wa mawasiliano kwa urahisi na bei nafuu katika nchi 16, mambo ambayo yatasaidia jamii na uchumi kukua kwa kasi zaidi. Watu wataweza kuendelea kuwasiliana hata wakivuka mipaka, na biashara inayovuka mabara itashamiri zaidi kwa sababu ya huduma yetu ya One Network, ambayo kimsingi ni sehemu ya ahadi ya Zain ya kutengeneza ulimwengu maridhawa.
“Naona fahari kuteuliwa na Zain Tanzania kuwa Balozi wake wa huduma yao ya One Network, na nawashukuru Zain kwa kunifanya sehemu ya huduma hii inayosisimua ya One Network ambayo imebadilisha mawasiliano ya simu za mkononi duniani kwa kuwa huduma ya kwanza kuunganisha mabara duniani kwa kuondoa mipaka na kupunguza gharama za mawasiliano.


‘’Kama Mtanzania siku zote nafurahia kupata fursa ya kufanya jambo linalogusa jamii na katika suala hili ninaona fahari kupewa fursa ya kusambaza habari na mambo mazuri ya manufaa ya One Network ili kuongeza uelewa wa Huduma ya One Network ambayo itafanya mawasiliano wakati wakuvuka mipaka kuwa rahisi na ya gharama nafuu,’’ alisema Lay Jaydee.
Muhidin Issa Michuzi kwa upande wake amesema anaona fahari kuteuliwa na Zain kuwa Balozi wa One Network kuwasaidia kusambaza manufaa ya kibiashara na ya mtu binafsi yanayopatikana kutokana na huduma ya One Network.
“Zain ni kampuni inayosisimua na ninaona furaha kujihusisha na kampuni inayoongoza na kuweza kutangaza manufaa ya kibiashara na ya mtu binafsi yanayopatikana kutokana na huduma ya One Network.


"Kubwa zaidi natoa shukrani kwa Zain kwa kuutambua mchango wa wanahabari hususan blogu na hii heshima si yangu mimi pekee bali ni ya ma-blogger wote wa Tanzania ambao Zain imeanzisha mchakato tunaogombania - wa kutambuliwa rasmi kwamba blogu ni kipasha habari chenye hadhi kama vingine vyote," alisema Michuzi.

Zain mapema wiki hii mjini London imeshinda tuzo ya Dunia ya Miundombinu Bora ya Biashara isiyotumia nyanya kwa sababu ya huduma yake ya ‘One Network’.



Huduma ya One Network inaunganishwa kwenye simu ya mteja wa Zain mara moja mteja akivuka mipaka bila kuwa na urasimu wa kujisajili kabla au kulipia ada ya kujisajili.


Wateja kadhalika wanaweza kupiga na kupokea simu kwa gharama za nyumbani wanapokuwa wanawasiliana na mteja wa Zain aliyesafarini. Mteja huyu naye kwa kutumia One Network atapokea simu zinazoingia bure na ataweza kupiga simu nyumbani kwa gharama za nyumbani.

One Network ni huduma ya kwanza duniani inayoondoa mipaka na kupunguza gharama za mawasiliano kwa kuwawezesha wateja kupiga na kupokea simu bure bila kulipia gharama za zuru za kimataifa wanapovuka mipaka katika nchi 16 ambazo zimeunganishwa na huduma ya One Network Barani Afrika na Mashariki ya Kati.


Wateja pia wataweza kuongeza salio kwa kutumia muda wa maongezezi unaopatikana katika vituo zaidi ya maelfu, vinavyopatikana katika nchi yoyote yenye huduma ya One Network.


‘’Zain inaamini huduma ya One Network itawavutia wateja wengi wapya kwenye mtandao wa Zain, na kadri huduma hii inavyoendelea kukua itachangia kwa kiasi kikubwa kwa Zain kutimiza malengo yake ya mwaka 2011 ya kufikia wateja milioni 150 na kuwa moja kati ya kampuni 10 zinazoongoza duniani kwa mawasiliano ya simu za mkononi,’’ alisema Magavilla.


Nchi zenye huduma ya One Network ni; Bahrain, Burkina Faso, Chad, the Republic of Congo, the Democratic Republic of Congo, Gabon, Iraq, Jordan, Kenya, Malawi, Niger, Nigeria, Saudi Arabia, Sudan, Tanzania na Uganda.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 36 mpaka sasa

  1. sasa mbona muchuzi hutuelezi huyo mamou ndo nani? inaonyesha kama mwanao vile na amekuja kukupongeza wewe. hebu tuambie mapema tulete posa.

    mdau TSN

    ReplyDelete
  2. Duh! michuzi we ndo unakula nchi ya tanzania! yaani unapiga kazi kama 10 hivi! ila nakutakia kila la kheri we mtu safi sana!!

    shizzle, Buffalo Texas.

    ReplyDelete
  3. Hivi huyu mkuku wa wilaya ya nanihii ndio nani?

    ReplyDelete
  4. Mkuu wa nanihiii!
    Kwa niaba ya wadau wanaopenda blog yetu ya jamii nakupongeza kwa kuwa ambasada wa zain!
    juu mkuu wa nanihii , juu blog ya jamii!
    mdau sweden

    ReplyDelete
  5. Naona una banner ya tigo ...hapo juu on your blog, hakuna muingiliano wa maslahi kati ya Tigo na Zain kuhusu nafasi yako mpya?

    ReplyDelete
  6. diko diko mbona unajipakazi namna hiyo?

    ReplyDelete
  7. Hongera Mh Mithupu na Mama Jide...mwenye nacho anaongezewa siku zote.
    Mithupu ehe...hapo Capt Habash kaja kumpa co Jide, bila shaka Mamou Muhidini ndo ubavu wako wa kushoto au ndo atakaimu ukuu wa nanii kwa muda???
    Harafu naona kama Kevin amepooza vile, TiGo ulikuwa umewashika mwanawane...lkn kama mbuzi wa Zain ni mnono sana tuendeleee mwanamme.

    ReplyDelete
  8. MKUU WA WILAYA YA NANIHII.. LINI UTAPOZI NA MAI WAIFU WAKO, ANGALAU KULA NAYE LANCHI HADHALANI? KILA SHUGULI UPO MWENYEWE TU SIYO VIZURI HIVYO KAKA.

    ReplyDelete
  9. Safi mkuu wa wilaya ya nanihii si ajabu kesho kusikia mkuu wa mkoa nanihii halafu mkuu wa nchi nanihii na mamou muhidin kuwa first lady, shemeji anapendeza sana!!

    Mdau ughaibuni middle east!

    ReplyDelete
  10. Hongera sana Mkuu wa Wilaya!!

    Majukumu ya balozi wa Zain ni nini ? Embu tudodosee kidogo.

    ReplyDelete
  11. Ha kaka Michuzi, ninaomba contact za Magavilla. Kijana mtanashati, ameshaoa?

    ReplyDelete
  12. Michu mbona wewe hujavaa kijani au walikushtukiza

    ReplyDelete
  13. Mkuu wa wilaya ya....., hongera sana kaka!!! Ukiona unapata vijiko vya hivyo ni ishara nzuri kwamba upo karibu sana na jamii!! Kaka Issa, endeleza juhudi zako na ujue kuwa wanajamii tutakutegemea na tunatambua mchango wako!!

    Mola akuongoze... Ramadan Karim!

    ReplyDelete
  14. Dada Jide, need I say more?? Sista keep up the good work na Mungu azidi kukuzidishia....

    Dada unatisha manake!!

    ReplyDelete
  15. Acheni hizo huyo ndo Mai waifu wakee

    ReplyDelete
  16. Jamani eleweni mithupu anamaanisha nini kusema "mamou muhidini" binti wa mkuu wa wilaya ya nanihii anamaanisha ni binti yake.Angekuwa mkewe angesema my wife wake.LOl mithupu miye nitakuwa mkweo.teh teh teh hongera sana. GB

    ReplyDelete
  17. make them greens Mithupu.ukineemeka wewe ndo neema ya blog hii ya jamii.pleasure all ours!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  18. hongera Bro' Michuzi,mafanikio yako ndio mafanikio ya wanajamii atiiii.chako che2,che2 che2.haha big ups MHE. Balozi teh teh. WARNING: Usi2mie tena maneno "Mkuu Wa Wilaya ya nani hii" from now on "Mhe. Balozi wa nani hii" hahaha

    ReplyDelete
  19. mkuu wa nanii mi nimevutiwa na MAMOU kama bint yako ndio ujue dodo lishawiva fanya mpango wa contact zake watu tujilie dodo letu
    kwako we halamu,

    big up u and jide ,mwenye nacho uongezewa na hasiyekuwa naco.....

    Tigo vs Zain sijui itakuwaje hapa!?

    mwaka huu patachimbika

    ReplyDelete
  20. Dah, wanakuongezea kofia tu-2!? ngoja nitakuita Ofisi kwangu tule lunch hapa Wall Street..

    sio Mashaka..

    Wabongo bwana watu wa hatari sana, yaani unataka kumposa Mke wa Michuzi na wala hawajaachana!? what do you mean
    ..msifananishe maziwa na tui la nazi???


    ===

    Buffalo,
    New York

    ReplyDelete
  21. Ishara nzuri hiyo, Big time both Jide na Mkuu wa nanii
    Londoner

    ReplyDelete
  22. Big up Michuzi na Jaydee. You deserve this 'award.' Nawatakia kila la kheri mabalozi. Bro usisahau kuwapa wadau namba ya Mamou, wenda wana vitabu vya 'topiki mupya.'

    ReplyDelete
  23. Wadau maelezo ya picha yanasema huyu Mamou ni mwanae(binti),mbona macho juu hamsomi mkaelewa??Big up broda from anotha motha

    ReplyDelete
  24. Kuna wadau walikuwa wana mashaka kwamba mabadiliko ya jina kuwa Zain ilikuwa ni mbinu ya kukwepa kodi fulani fulani kama wanavyofanya wawekezaji wengine. Madai haya yana ukweli?
    Isije ikawa mkuu wa nanihii ya nanihii unafundishwa ufisadi.
    Wadau, mtafuteni Mzee wa Vijisenti Chenge aongoze kamati ya kupitia upya hili.
    Hongera sana Michuzi.

    ReplyDelete
  25. Sasa Michuzi si unaona mwenzio amekuja na Mai Samsing wake?
    Sasa we mbona umekuja na Mai dota wako?
    Kwani Mama yake kasafiri au?

    ReplyDelete
  26. Michuzi nakusifu kwa kuwa ni Mtanzania mwenye jitihada za kuondokana na umasikini, huna longolongo na ndio maana mwenyezi Mungu nae anakuona. Endelea kukaza buti mh muu wa wilaya ya nanihii!

    ReplyDelete
  27. permission to bring mahari, sir

    ReplyDelete
  28. Oh my kwanza honera...Hiyo ni part time job au another full time job? Wasije wakakuchosa sana.


    Na huyo ni binti wako? Hongera tuonyeshage basi familia yako. Honesty achana na waosha vichwa au vinywa but wengine hii blog ni kama breakfast yetu. I feel like I know you more that you could imagine. It will be nice to knowyour family too

    Kama ni mwanao hongera. She is a cute little girl

    Mdau
    USA

    ReplyDelete
  29. Hongera michuzi, huyo binti wako ana miaka mingapi?
    Na kama kuna demu anataka mwenza hapa awasiliane na nami
    Mdau
    USA

    ReplyDelete
  30. Hongera sana kaka michuzi, kidogo kidogo ujaza kibaba sasa hivi tutasikia jakaya kakuchagua kuwa mbunge wa viti maalum ha ha ha.sasa ukipewa kiti cha ubunge usitusahau sasa wadau wako ukawakirishe malalamiko yote.kila la kheri mufti.
    Mdau mzawa

    ReplyDelete
  31. Tarehe September 12, 2008 2:48 PM, Mtoa Maoni: Anonymous.

    Mdau ulieuliza kwanini Kelvin kapoa, hajapoa kwa kutaka kuna wenda wazimu wanajijua walichofanya kwenye blog zao. Mungu atawalipa

    ReplyDelete
  32. Muwe na akili huyo ni mke wa pili wa Michuzi mmesahau yule wa safari ya Uganda alikuwa wa kwanza huyu ndo mke wake sasa si mtoto. Ombeni radhi

    ReplyDelete
  33. TO WHOM IT MAY CONCERN...!

    JAMENI NI MIMI NALITOLELA PETER NIMERUDI TENA SIKUWA NA NAULI YA BASI KUJA MJINI KUTOKEA MBAGALA KUANGALIA NET. SASA MICHUZI HILI NI SUALA ZURI SANA MIMI KAMA NILIVYOJIELEZA TANGU AWALI NIMEMALIZA MUZUMBE CHUO KIKUU NINAUPEO WA HALI YA JUU WA KIMATAIFA NA HATA HUMU NDANI NIMESOMA VITABU VINGI SANA, NINA WAFAHAMU HATA KINA BILL O`REILY, BILL COSBY,BILL CLINTON NA MKE WAKE NA YULE MAMA MWEUSI WA MASUALA YA KIGENI DR. RICE NIMEFUATILIA SANA MAFULIKO YA KATARINA N.K SASA KAKA MICHUZI NINGEPENDA UNIUNGANISHIE KAZI HAPO JIKONI ZAIN KIBARUA CHOCHOTE MIMI KINGEREZA KINA PANDA SANA KAMA KISWAHILI TU, KUNA NDUGU YANGU HATUFAHAMIANI AMEWAHI KUNIKASHIFU ETI KINGEREZA CHANGU NI CHA MAKOSA HATA KISWAHILI NAKOSEA SPELLING, BUT I THINK HE IS JEALOUS KWA SABABU BABA YETU ALIMWACHA MAMA YAKE. LAKINI SISI WOTE NI KINA PETER NALITOLELA MIMI NILISOMA ST. ANTONY MBAGALA YEYE SIJUI ALIKUWA WAPI PRIMARY LAKINI WOTE TUMEMALIZA MZUMBE. MICHUZI NISAIDIE NIPATE KAZI HAPO NDUGU YANGU MSHAHALA WANGU TUTAKUWA TUNAGAWANA KIPINDI CHOTE CHA MIEZI SITA YA MWANZO. ASANTENI WOTE

    ReplyDelete
  34. Nalitolela unaniacha hoi sana na comment zako. Nakutakia kila la kheri ndugu yangu!

    ReplyDelete
  35. kuna wengine wamerithishwa majina na mbegu ya uwendawazimu!

    ReplyDelete
  36. sometimes i can`t understand this guy Nalitolela is he a fake one or the real Nalitolela I used to know those days at Muzumbe? p;lease its time each of you so called nalitolela Peter show your pics so we know who is who!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...