Libeneke la OBAMA limevuka boda hadi kuingia bongo. Mara baada ya kuona gari ikiwa na sticker ya OBAMA 08’ leo nimekutana na wadau walio-dizaini t-shirt hapa Dar.
Wanasema wanaendeleza libeneke kule Mitaa ya Irish Pub Msasani karibu na TIRDO.
Kwa maelezo zaidi wasiliana na
Ndugu Mayunga
0784547996
/0713547996

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. hizi ndo bangi, huu si wizi tu, mnaacha kumsupport mrema.

    ReplyDelete
  2. Kama si umbea ninini?

    Kwani huko Irish pub kuna wapiga kura wakimarekani?

    Hebu jengeni nchi yenu sio kushabikia mambo ya nje

    ReplyDelete
  3. ndio maana tz tunapaita bongo! deal za maajabu ajabu, support ya obama tanzania itamsaidia vipi huko usa? hata hivyo nampongeza alokuja na mbinu hii, ameona pana opportunity ya kujipatia pesa na ameichukuwa hongera!

    ReplyDelete
  4. ma anon hapo juu bongo hii kula kwataka akili naubunifu ,watu wanafyatua vitu kwa picha za obama wanauza wanaingiza chao mfukoni usifikiri kila m2 hapa bongo ni mkereketwa wa siasa na kwa taarifa tu kampeni zitakapokuwa zikipamba moto marekani na huku bongo vitu vyenye picha ya obama vitapata sana soko ebu jiulize mpaka mwezi november jamaa watatengeneza pesa kiasi gani KUHUSU MREMA sasa hivi hauzi hana tofauti na hip hop ya BONGO narudia tena wabongo wengi makini hawpendi siasa ila kama kuna nafasi ya kula ndio hapo unapowaona wenye akili zao na ubunifu wakkiibuka na logo za OBAMA , BONGO UNAISHI KWA AKILI ZAKO FUNGUA MACHO

    ReplyDelete
  5. Marekani ikifanya maamuzi mabaya dunia inaathirika. Ona sasa bei ya mafuta ilivyojuu kwa sababu ya vita vya iraki. Kwa hiyo hizi siyo bangi.

    ReplyDelete
  6. Siku ya uchanguzi wa akina JK hakuna hata Mmarekani mmoja aliyebeba bango wala picha. Wala wengine hawajua kuna nchi kama TZ ina exists. Sasa nyie kujishaua ya nini?

    ReplyDelete
  7. HUU MICHUZI SASA NI WAZIMU. WATZ KWA KUIGA BASI HATA HILI? MTAIGA MANGAPI? FANYENI KAZI MJENGE TAIFA NA FAMILIA ZENU YA OBAMA WACHIENI OBAMA.

    ReplyDelete
  8. sasa obama anawahusu nini, mnazidi tu kumharibia. maana tayari ni mweusi, na hilo ni doa kubwa sana, unadhani kuna mzungu atakubali kuongozwa na mweusi? nyie tengenezeni t-shirts mjipatie vijisenti

    ReplyDelete
  9. freedom of speech. nyie inawauma nini watu wakibeba mabango ya obama. Mbona alienda Ujerumani na wakatoka watu wengi mno kumsilikiza mpk inamwuuma McCain na kumwita international celebrity? Nyie hamjatulia...kazi kuponda kila kitu bongo. Everyone is entitled to state their beliefs bwana...mmechoka!

    ReplyDelete
  10. Alafu wewe anon wa September 05, 2008 1:37 AM ni fala kabisa. Yani unadhubutu kusema kuwa mweusi ni doa? Toa mawazo duni yako hapa. Unajishusha hadhi mwenyewe! Pumbafu kabisa! Tena unatakiwa kuwa-banned katika hii blog kabisa.
    YES WE CAN!

    ReplyDelete
  11. We anon wa September 05, 2008 1:37 AM fala kweli. Dr Martin Luther King Jr katika ile famous speech yake ya 'I have a dream" alisema...
    "I have a dream that my four little children will one day live in a nation where they will not be judged by the color of their skin but by the content of their character."
    Umeelewa hapo au mpk tutafsiri? we unadhani kwa nini Obama alitoa acceptance speech yake on the 45th anniversary of this speech?
    Wakati mwingine tunajibagua wenyewe!

    ReplyDelete
  12. huyu atakuwa ni yule jamaa alikuja na kitabu cha Obama ameamua kuja na dili la tshirt sasa hivi

    ReplyDelete
  13. Nyerere aliwahi kusema ukiona mtua nakushauri....na wewe.. utamalizia

    Naamaanisha ukiona wazee wamekubali mtoto wao wa miaka chini ya 18 atiwe na azae kabla hata ya ku-qualify kuwa mtu mzima na hawamfungulii kesi mhusika jua kabisa hapo kuna jambo its extraodinary, unreal na haiwezekani in the world of child abuse na all these scene maana tunaambiwa mpaka uki-add mtoto wa miaka chini ya 18 kwa page ya facebook au bebo na myspace uko hatiani iweje both two wasiwe atiani ingekuwa mtoto wa Obama imagine ingekuwaje?
    Tia akili acha ujinga. Hao hawakusaidii chochote sasa kwanza ana ukoo mrefu uko choka mbaya Kenya hapo. Wewe ndugu yangu fufua treni hizo angalau zisaidie kuokoa foleni mjini yaani ya hapo Ubungo mpaka mjini. Tbt mpaka mjini na zingine as first point mimi bado naonge ana Boris hapa London tunaleta tube Bongo in two yrs sasa huyu jamaa anaguna nini wakati mabasi ya kwenda kwa kasi tuliambiwa tuko mwaka 2000
    Londoner

    ReplyDelete
  14. Kwa watu walioenda shule ya matawi yajuu wanajuwa kuwa rais wa USA ni rais wa dunia nzima hilo halina ubishi mtabisha mpaka kuche huo ndo ukweli, mifano michache tu, hivi nani anafadhali miradi mingi duniani ikiwemo Tanzania, kama si wa-Amerika, nikiitaja michache tu ya Tanzania - UKIMWI, MARALIA,VITABU VYA SHULE, UJENZI WA BARABARA, BAJETI YA TANZANIA, ana wote about dollar? it is a benchmark of all world currencies, na mambo mengi tu ya dunia ambayo hutgemea ushirikishwaji wa USA.

    ReplyDelete
  15. Inaelekea watu hawaelewi the importance of the American precidency to the world. Muulize Kikwete awaelezeni fresh. Foreign Affairs za Nchi zote zinatoa macho na kungojea kwa hamu kuona nani atakuwa rais. Mnadhani Marekani ni nchi ndogo...kha!

    ReplyDelete
  16. ıts neocolonialism nduugu zangu.

    tanzania hatuwezi kujiendesha bila misaada.so acha tujishauwe,sio kupokea misaada tu kila siku wakati wenyewe tunashindwa kuzalisha.

    ReplyDelete
  17. HATA KAMA TANZANIA INASAIDIWA NA MAREKANI MPAKA KUSAFISHIWA VYOO VYETU. RAIS WA MAREKANI NI WA DUNIA NZIMA LAKINI NAULIZA NI MMBONGO YUPI ATAPWEWA NAFASI YAKUMPIGIA KURA HAPA TZ? HUKO MAREKANI PENGINE WAKO WABONGO WALIOKUA NA URAIA WA KIMAREKANI NA WATAMPIGIA LAKINI HAPA TZ! JAMANI KAMA HAMNA LAKUFANYA NENDENI PWANI MKAOGELEE. LOOOOOO MNABOA

    MAMA JOICE

    ReplyDelete
  18. Inaelekea mnakuhusudu sana marekani...kila siku maneno mnasema watu wanaoishi huku lakini leo obama '08.....

    jamani....ujasirimali mzuri lakini mimi ninayeishi huku na najua wengi waioshangaa hili ni watu wanaoishi huku...

    Ukweli ni kuwa home sweet home jamani ....na nimejifunza kuwa watu wataipenda nchi yako iwapo na wewe unaipenda ...wenzetu wazalendo wa damu siye tupo tupo tu ila kuishi huku kunanifanya niipende zaidi nchi yangu....nampenda sana Obama lakini hiyo sticker sijui na t-shirt mmmmmmh labda mnipe hela ndio nitaweka bure siweki wala sivai kabisa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...