".....bwa'mdogo chunga sana....ohoooo." anaonekana kusema mstaafu mmoja akimwambia askari kanzu baada ya wastaafu hao wa iliyokuwa jumuiya ya afrika mashariki kuandamana hadi geti kuu la ikulu kudai mafao yao
wastaafu wa iliyokuwa jumuiya ya afrika mashariki wakiwa wamekaa nje ya lango kuu la ikulu kudai mafao yao jioni hii. hata hivyo mkuu wa mkoa wa dar abbas kandoro alifanikiwa kuwashawishi wastaafu hao kutumia busara na njia za kiungwana kudai mafao yao. waliondoka wakiwa wameridhika baada ya kuahidiwa kuwa malalamiko yao yatafikishwa pahala pake
baadhi ya mabango waliyobeba wastaafu hao


".....asante mwanangu, virungu si suluhu pekee ya matatizo", anaambiwa kamanda selemani kova baada ya wastaafu kutumia busara na kukubali ombi la mkuu wa mkoa abbas kandoro kwamba watafute ufumbuzi kwa njia ya amani
wastaafu wakimpongeza mkuu wa mkoa abbas kandoro kwa kuahidi kusikiliza kilio chao na kukipeleka pahala pake
mkuu wa mkoa wa dar abbas kandoro (mikono kifuani) mkuu wa wilaya ya ilala patrick tsere (shoto) mkuu wa kanda maalum ya polisi ya dar selemani kova (tatu shoto) na maafande wakiwasikiliza wastaafu
mmoja wa viongozi wa wastaafu wa jumuiya ya afrika mashariki akiwashauri wenzie wasikie ombi la mkuu wa mkoa wa dar abbas kandoro kuwataka watafute ufumbuzi kwa busara na amani
mkuu wa mkoa mh. abbas kandoro akiwasili na mkuu wa wilaya ya ilala mh. patrick tsere



s

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. MAKUBWA,AWAJALIPWA TOKA 1977 AIBU GANI HIYO YAN KUDAI MAFAO WASHATUMIA ELA NYING KULIKO WATAKAZOPATA,ELA ZILITOLEWA SIKU NYING NA SERIKAL YA MAREKAN/UINGEREZA, KENYA NA UGANDA WALISHALIPWA,TANZANIA WAJANJA WAKAZILA,HIV VIONGOZ AWAOGOP LAANA KUNYANYASA WAZEE HIVO

    ReplyDelete
  2. wewe michuzi unajua maana ya neno 'akimbo'

    ReplyDelete
  3. This is very nice na nadhani serekali imechukua hatua nzuri kusikiliza vilio vyao. Wazee wetu hawa hawaitaji virungu na hakuna mtu yoyote anayehitaji virungu period katika kudai haki zake.

    ReplyDelete
  4. Hivi ndugu yetu kikwete hao watu huwa huwaoni au vipi? basi hata heshima ya kuwaheshimu ni kama wazazi wako halafu unatuambia wewe ni muumini mzuri unafunga unaswali kwanini unawatesa hao wazee?angalia umerudi kumzika mwenzako juzi tu au umesha sahau?

    ReplyDelete
  5. Hivi hao viongozi wetu wanapowaona wazee wao waliowalea wakisumbuka wanasikia raha gani?
    Jamani chondechonde leo mnawatendea hao na nyie zamu yenu kesho kwani bila kujenga misingi ya uongozi iliyoimara mtakuja kubaki kusema enzi zetu bwana mambo hayakuwa hizi

    ReplyDelete
  6. Shida ni nini? Kwa nini hatuoni aibu kuwasotesha wazee ambao walitoa mchango wao wa ujenzi wa taifa, wakastaafu bila kufisadi nchi, na sasa ni hohehahe. Jamani JK wapeni haki yao. Tulioshikilia ofisi za umma tujiulize baada ya miaka 10, 20, 30, 40, au hata hamsini tutakuwa wapi na katika hali gani iwapo muumba bado atakuwa ametuweka hai!!!!

    ReplyDelete
  7. mbona hawa ni vijana? i wee wa eac kweli? na mbona wanasubiri rais hayupo ndio wanakwenda ikulu? akiwepo hawatokei au wanaogopa vyombo vya dola? walisubiri rais yupo japan kwenye g8 wakaenda ikulu sasa yupo zambia ndio wanakwenda tena wasubiri akiwepo ili ujumbe ufike kwa mlengwa.

    ReplyDelete
  8. Kwa Ufupi picha ya tatu toka juu unaeweza sema " Habari ndiyo Hiyo"

    ReplyDelete
  9. hawa bado wana ndoto za kutatuliwa hili swala?Kubalini yaishe hili shirikisho lilishakufa hata kabla sijazaliwa.Imetoka hiyo ikirudi pancha.Na msijidanganye kuwa JK atawasaidia kwa vile ni Muislam mwenzenu,Mwinyi aliwaacha Solemba na alikuwa anakwenda Msikitin na nyinyi.Nasema haya sababu kuna waislam wengi wanadhani mtu akiwa Muislam basi atawasaidia.Kalaghabaho.

    ReplyDelete
  10. ABBAS KANDORO toa mikono mifukoni, hao ni wazee wako nahisi wana umri mkubwa kuliko wewe, madaraka na umri, umri mbele madaraka nyuma

    ReplyDelete
  11. Annon wa September 04, 2008 10:57PM
    Kama unawaona Vijana hapo basi uelewe kwamba wazazi wao ndio walikuwa wafanyakazi wa EAST AFRICA na kwa sasa wameshafariki na wao (Vijana) ndio wame-rithishwa mafao na haki zao. Hivyo sasa hivi wao ndo principal recipients na wanaenda ikulu kuomba haki za wazazi wao.
    Haki yao wapewe maana bila wao tusingekuwa hapa.
    Angalia chuo kikuu vijana wakigoma kwa fedha za kichele , fedha zao zinalipwa mara moja na wazee waliofariki wakiandamana toka mwaka 1989 mpaka leo hakuna malipo.
    Ndo ujue vijana tunataka haki yetu sasa na tunaona wazee kama wajinga.

    ReplyDelete
  12. Anony wa 10:57 You have a very big Point there!

    ReplyDelete
  13. bongo tambarare.....

    ReplyDelete
  14. kwa kweli hii ni aibu sana kwa inchi tajiri kama hii... chunguzeni kwani ofisi wanazotoka wastaafu hao zinameundwa tume ambazo zinakula pesa kila wiki heti wanachunguza files za wastaafu kwa hiyo wanakula kuliko wanaostahili kulipwa .... chunguzeni hii inatia doa nchi yetu na laana kwa maendeleo ya nchi

    ReplyDelete
  15. hii ni aibu kwa serikali yetu na jamii yetu. Kwanza serikali inashindwa nini kuwalipa hawa jama fedha zao, wakati malikia alizitoa kitambo, na kenya na uganda washasahau sakata hili, bado sisi tu, wapawe chao waache kuwazingua vikongwe wa watu.
    Pili, jamii yetu ya kibongo haina umoja katu, kila kikundi cha watu kinadai maslahi yake pekee, bila kupata msaada kutoka kwa wanajamii wengine. Utaona wanafunzi wa chuo wanaandama, mara walimu wanatishia kugoma, mara wafanyakazi, mara madaktari, mara wafanyakazi wa bandari na reli, bado polisi tu kutishia kugoma na sijui itakuwaje?
    Sasa hapa jamaa wanatumia udhaifu huu wa watu kudai haki katika vikundi-vikundi kuendelea kukandamiza, katu hatuwezi kuipata haki hiyo..

    ReplyDelete
  16. Tanzania bwana. Vitu vya ajabu sana.

    ReplyDelete
  17. hii ndio hasara ya 'collective responsiblity' hakuna anaeweza kushikiliwa kuwa ndie anaeshindwa kazi. Wote wamejitoa na mhusika hajulikani hapo wizara ya fedha.
    Hii ni aibu ya kiafrika, kumdhalilisha mzazi wako!!
    hata laana tunapata na bado tunashangaa mambo hayaendi, wakati tunajilaani wenyewe.
    MUNGU TUREHEMU.
    Lakini je kuna sababu maalum kwa nini hawa hawalipwi?
    Ofisi husika inasemaje?
    ni pesa hakuna? au ni waongo? au makaratasi yao hayaeleweki? au computer haziwatambui?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...