JK akipita katikati ya magari mengi yasiyoondolewa bandarini na kusababisha msongomano mkubwa, rais kikwete alikutana na tatizo hilo wakati alipotembelea bandari kujionea mwenyewe ufanisi wa taasisi hiyo
JK akipita kandoni mwa meli kubwa ya mizigo ambayo ilimaliza kupakua mizigo yake jana mchana lakini kukosekana kwa tishari (meli ndogo ya kusindikiza) kumefanya meli hiyo na nyingine haipo pichani zisiondoke bandarini hadi leo wakati rais kikwete alipotembelea bandari na hivyo kusababisha meli nyingine kushindwa kutia nanga bandarini

JK akitoa maagizo alipokuwa bandarini
Rais Jakaya Kikwete amesema ana orodha ya majina ya wafanyakazi wa kampuni ya ukaguzi na ukadiriaji wa mizigo ya TISCAN, wanaoshirikiana na wafanyabiashara kukwepa mizigo yao kukaguliwa na kuamuru wafanyakazi hao wafukuzwe kazi mara atakapokabidhi majina hayo.
Rais Kikwete alitoa kauli hiyo leo alipofanya ziara ya ghafla katika Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), ambapo alisema orodha hiyo anaifanyia kazi. “Majina hayo sasa nayafanyia kazi, waambie watu wa Maktaba (makao makuu ya kampuni hiyo) mtindo wanaofanya unajulikana, sitawaumbua hadharani, majina yao nitawapa wakubwa zao na nikiwapa tu watoeni kwenye kazi,” alisema.
Rais Kikwete alisema wafanyakazi hao wamekuwa na tabia ya kushirikiana na wafanyabiashara na kuwapa mbinu za kufanya, ili mizigo yao inayoingia nchini, isiweze kupitishwa kwenye mashine ya ukaguzi inayotumia mionzi, hivyo kutozwa kodi ndogo.

kwa habari zaidi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 30 mpaka sasa

  1. Tishari ni 'burge' hutumika kubeba mizigo toka meli ikiwa haijatia nanga ktk bandari.

    Nafikiri mtoa habari ana maana ya Pilot Boat ambayo huziongoza meli kubwa kupita ktk mkondo mwembamba wa mlango wa kungia ktk bandari ya DSM. Wembamba huo wa mlango wa kuingilia bandari ya DSM huitaji waongozaji(navigators) wenye uzoefu na mazingira ya kipekee ya bandari salama iliyoanzishwa na Sultani za Zanzibar.
    Mdau
    Kigamboni.

    ReplyDelete
  2. Kwenye huo mlundikano wa magari, nimeyaona magari matatu ya mafisadi wa PSRC. Je, serikali ina taarifa ya mafisadi hao wa PSRC au inaangalia BOT pekee???

    ReplyDelete
  3. Wahenga wanasema ukionacho kwenye kioo ni tafsiri halisi ya mwenye sura hiyo.
    Rais kuanza kufukuzana na vibaka wa customs inaashiria mapungufu makubwa katika utendaji wa kazi.

    Mdau
    Faustine
    http://drfaustine.blogspot.com/

    ReplyDelete
  4. JK kazi anaiweza lakini wanamwangusha watu walio chini yake. Kila mtu bongo anataka kula. Hili ndilo tatizo kubwa na solution moja ni kuwaondoa wote hawa na vijana kama sisi tuingie kazini. Hongera JK!!!!

    ReplyDelete
  5. Hivi, JK kabla ya kwenda Bandarini alikuwa ofisini/kazini/ikulu au alikuwa ana misele mingine street???

    Maana mapigo aliyopiga utafikiri kaingia kitaa one time weekend fulani hivi!

    Duh, kama u-simpo basi jamaa yuko simpo kimavazi

    ReplyDelete
  6. Jamani naomba nisaidieni,ina maana hakuna waziri anayeshughulika na masuala ya bandari mpaka mheshimiwa Rais alishughulikie suala hili??Ama kazi za mawaziri zipi?Msinicheke kwani kuuliza si ujinga.Na mwisho labda tu niulize wanachi wenzangu,kama hali yenyewe ndiyo hii rais anafanya kazi hata za mawaziri si hatuna haja ya kuwa nao bali tuwe na makatibu wakuu tu wamalize kazi ili tupunguze mzigo kwa serikali kuwalipa mishahara na huduma nyingine mawaziri vivuli?WIZI MTUPU!

    ReplyDelete
  7. Health and safety !
    Baba rais Kofia ipo wapi ?
    ama ndo yale yale ya kazi ya mungu ?
    Mfano gani unaonyesha hapa ?
    safety boots huna ?na HV pia ?
    Unajua gharama tulizotumia kukuchagua ?
    Kwanini usisubiri umalize kipindi chako cha urais ndo uanze ku take chances ?
    Njoo nikuazime vyote hivyo hapa nabebea mabox kama huna
    Kaima Uk

    ReplyDelete
  8. Halafu huwa wanafidia kwa kutoza mizigo mingine kodi kubwa zaidi. Fikiria umenunua gari kwa $5000 unakaratasi zote zinazoonyesha hivyo, unafika bandarini wanakuambia thamani ya gari lako ni $10000 na wanachukua malipo yao based on $10000. Nchi yetu ni ngumu sana kuendelea based on mazingira ya corruption yanayokuwepo. Suala la Port costs serekali inatakiwa ilipe umuhimu mkubwa maanake ni kuwanyima watanzania haki yao ya kumiliki vitu kama usafiri kwa kudouble costs wakati wanajua hatuna viwanda vinavyotengeneza magari. Nchi zilizoendlea magari yanatengeneza humo humo hamna mtu anayelipia port costs kuagiza magari kutoka nje na ndio maana everybody can own a car

    ReplyDelete
  9. Naomba aliyepiga hii picha atupatie maelezo kama JK alikuwa amevaa suluari aina ya "jeans".

    ReplyDelete
  10. Mh. Rais, Hivi hakuna Mabosi wa mamlaka husika mpaka majina yakakufike wewe? Ondoa nao maana wamezembea kazini, walitakiwa kujua na kuchukua hatua kabla hujasema.

    ReplyDelete
  11. Jamani mimi kunakitu kimoja ambacho nashishindwa kukielewa katika maamuzi mengi ya ya viongozi wetu na utendaji mzima wa serikali yetu.Tatizo la rushwa katika bandari ya Dar na sehemu nyingine unawanufaisha viongozi wachache kwa serikali kokosa mapato makubwa kutokana na matendo ya viongozi wachache pesa ambazo zingeliweza kusaidia katika kupunguza machungu kwa walalahoi.Badala ya kuona hatua zinachukuliwa dhidi ya waalifu hao.Tunasiki wakipewa muda kurudisha pesa pesa mfano swala la EPA n.k.Kuhusu swala la bandarini kwa wanaohusika katika kuwasaidia waalifu kukwepa kodi-na hao wanaowasaidia ni waalifu pia-Badala vyombo vya sheria kuchukua hatua dhidi ya watu hawa wanakwenda kwa Rais kuomba ruhusa ya kuwachukulia hatua watu hawa!Na Rais badala ya kuelekeza kuchukuliwa hatua anaenda bandarini kuwatishia waalifu na wavunja sheria kua majina anayo kama majina anayo kwanini asichukue au vyombo vya sheria visiwachukulie hatua?!Kama Mh.Rais alikua hajayafanyia kaziya nini kutaja ya kwamba majina anayo?Au nikuwapa muda watu hawa fufuta ushahidi au kukimbia nchi?Tumekua tukisikia katika majukwaa ni jinsi gani serikali yetu isivyopenda na inavyopigana vita dhidi ya walarushwa lakini katika vitendo tunashuhudia MAZINGAOMBWE!!!!!!MUNGU IBARIKI TANZANIA.

    ReplyDelete
  12. kuna tatizo lingine hajalisema, wizi bandarini, inataoa picha mbaya sana, ki ukweli hata majirani wanaotumia hiyo bandari wangekuwa na option wangeachana nayo..bro michu kama vp iwepo mada ya bandarini ku zungumzia mapungufu na namna ya kuyaondoa, ki binafsi nachukizwa sana na kutowajibika na wizi,mi ni mtanzania nafanya kazi na kuishi Rwanda, juzi nimepewalift kwenye convoy ya magari toka dar kati ya magari 8,5yametolewa radio, pia kuna mfanyakazi mwenzangu kanunua gari kufika bandarini hakuna control box,inatia hasira sana%^#@#%^&^*(*&(&^*^%&$ kwa nini Jk bado anawalea hao wasiowajibika?? au ana lake Jambo? ama ndo kulipa fadhila? @#$%^&*()_)(*&^%$#&%&^%%$^& *10000 waizi wote bandarini

    ReplyDelete
  13. Kamua baba...kamua baba...hadi kieleweke. Ukimaliza hapo njoo Kipawa na Gongo la mboto vibaka wanatusumbua sana

    ReplyDelete
  14. HII KALI YAKE SIKIA RAIS ANATEMBELEA BANDARI MIMI NASHANGAA WAKATI NASIKIA NCHI INAKWENDA KWENYE GIZA SI WACHA HAYO MACONTAINER YA JAZANE WAKATI ANATAKIWA KUHAKIKISHA KUNAPATIKANA UVUMBUZI WA TATIZO LA UMEME SASA WANASHINDANA NUNUA USINUNUE MITAMBO YA DOWARNS,LETENI UVUMBUZI WA UMEME KWANZA HUKO BANDARINI RAIS UNAENDA KUTAFUTA NINI???? NCHI KWENDA KWENYE GIZA??? HUU NI MWENDO MZURI KWA TANZANIA

    ReplyDelete
  15. Mr president and your team ,someone need to take health and safety at work issues seriously as well, man !
    whats wrong with you guys ?

    ReplyDelete
  16. Nna shaka na ufatliaji wa vitengo vya madini na nishati na bandari kwa kipindi kimoja. Muda wote umepoteza kutembea nchi za watu sasa ndio unaanza kufuatilia vitengo ambavyo mnavitafutia sababu ya kuwapa Wachina au makuburu wenu kwa bei ya kuuza njugu.
    Sisi tunaelewa mnataka kuuza tenda madini nishati bandari. Uzembe wa vibaka n danganya toto, hpa deal ni kuuza na kupata 10%.
    Tatizo la kurundikana kwa magari ni kwamba mfumo wa kodi sio mzuri kwa hiyo badilisheni na kusafisha system yenu kabla ya kuanza kuvamia vibaka, wakale wapi? Nyie mnavaa jeans za Ulaya na kutembea na Range Rover, Volvo, BMW, Cadillac, na Maserati. Wao wakale wapi? Accountability should start from the top and move down.

    ReplyDelete
  17. TATIZO LA KURUNDIKANA MIZIGO BANDARINI LINASABABISHWA NA SERIKALI YENYEWE,KATIKA NCHI ZENYE URASIMU KATIKA AFRICA NAFIKIRI TANZANIA NI KWANZA TATIZO NI HILI TARATIBU ZA UTOAJI MIZIGO BANDARINI TANZANIA PROCESS YAKE NI KUBWA MNO,KWA MFANO UNAWEZA KUCLEAR GARI UGANDA AU KENYA TOKA CUSTOMS WITHIN 2-3 DAYS NA NUMBER PLATE JUU TANZANIA KIAMA,WAMEWEKA TBS,TISCAN,TRA HAO WOTE WAFANYE VALUATION NA KUANGALIA KAMA NI LA UMRI GANI KWA TBS,KOTE HUKO NI RUSHWA TUPU,NA UNACHUKUA WIKI NNE MPAKA TANO,GARI ULILONUNUA DOLA 5000 NI KWELI WATAKWAMBIA NO DOLA 10,000 VINGINEVYO UCHEZE WA SIUPLIFT,MIMI NASHAURI BORA TANZANIA MKAWEKA KWA MFANO GARI ZIINGIZWE ZA UMRI USIOZIDI MIAKA MITANO TUKAJUA VALUE YAKE NI HII,KULIKO KUPELEKA TBS DOCUMENTS ZINAKAA WIKI KWA USUMBUFU MTUPU TBS WAONDOLEWE KWENYE KUHAKIKI MAGARI WANACHELEWESHA BURE HII NI KUWAABIA WATU NA FEDHA ZINAENDA KWA SERIKALI DOLA 5O TU WAKATI WALIOPEWA LESENI ZA INSPECTION NA TBS WANAPATA MPAKA DOLA 350 KWA KAZI GANI?????

    ReplyDelete
  18. Watanzania lipi jema kwenu? akisafiri mnachonga kuwa hafanyikazi haangalii matatizo ya ndani ya nchi, sasa ametulia anashughulikia matatizo kama mlivyokuwa mnalia bado mnachonga kuwa anaingilia kazi za mawaziri sasa mnataka afanyeje??? hongrea JK chapa kazi

    ReplyDelete
  19. yaani hao wazungu ndio wanajua health n safety. (kofia,high visibilty jacket n safety boot, rais alitakiwa apewe vyote hivyo akiangukiwa na kitu mguuni vidole hana) na hao wa tz hamna hata mmoja anaetilia maanani usalama eneo la kazi


    mdau uk

    ReplyDelete
  20. ...majina, majina,orodha, orodha, vitisho, vitisho.....I have heard all this before! time someone ACTED!!!!USIBANIE HII mICHU.

    ReplyDelete
  21. hiyo inamaanisha waziri anayeshughulikia sekta ya bandari ni miyayusho we mpk Mh.Rais kaenda mwenyewe.JK fukuza huyo Waziri sanamu na kuchagua mtendaji mzuri atakaye kupunguzia mizunguko kama hiyo kwa kuhakikisha kila kitu kinaenda sawa.

    ReplyDelete
  22. hao jamaa ukipeleka gari lako na docs zote ikiwepo invoice uliyonunulia wanakataa,watakwambia si tunafata kitabu chetu.Ili wakuumize kwenye kodi hicho kitabu sijui kimetengenezwa kwa misingi gani sijui gari ya £2000 watakwambia £4000.

    ReplyDelete
  23. Kama JK anataka kuboresha utendaji wa hawa wala rushwa hakuna dawa ya kuwapa warning, dawa ni ku outsource watu toka nchi zenye uzoefu na bandari na mambo ya kodi kama Royal Crown, unawaachisha wote hapo bandari kazi kwa mpigo na kuwaambia waombe kazi upya, halafu wakiomba wanakuwa disqualified kwa low performance wakati royal crown wanatrain watu wapya pale bandari.

    Inapitishwa sheria ya ufisadi bungeni kuwa ukikutwa na hatia ni kifungo cha maisha jela, maana kunyonga watu wa haki za binadamu watatupigia kelele. Ili mtu akikutwa kaiba au kasababisha hasara ya mabilion yaozee alipoyaficha kwani hata toka jela maisha.

    Hapo watu watakuwa na discipline, lakini hii ya miaka mitano wanaiba halafu wanajua wakitoka jela tayari wana mitaji.

    ReplyDelete
  24. Mdau aliyezungumzia safety kazungumzia suala la msingi sana. Wazungu hapo wamepiga kofia gumu na vest zenye rangi zinazoonekana. Msafara wa watu weusi unaendaenda tu. Mtu akipigwa konzi la chuma kizito akajeruhiwa vibaya anamsingizia Mungu wakati Mungu keshamaliza kazi kwa kumpa vifaa vya kujihami.
    Hii kazi hata sio kazi ya waziri. Menejimenti ya sehemu husika inatakiwa kuwa na majibu ya utendaji kazi za siku hadi siku.

    ReplyDelete
  25. Mbona naona mashangingi tu, hiyo bandari haipokei vistarlet?

    ReplyDelete
  26. Mgawe hana uwezo na bodi ya bandari iliundwa na Mramba wakati akiwa waziri wa miundombinu.alijaza watu wasio na uwezo na ali propose mgawe awe mkurugenzi huku hana uwezo wala hajui chochote.waondoke haraka hawa makapi ya MRAMBA.

    ReplyDelete
  27. Hivi rais anajuwa ukuu wa mamlaka aliyonayo au anachezea tu hicho cheo...rais ni taasisi,system inatakiwa ifanyekazi ...haina ulazima wa yeye kuwa kila mahali wakatii wote ili watu wafanye kazi...wewe fikiria tangu mwezi wa 11 mwaka jana hadi juzi ameshatrembelea bandari mara 3 au 4...yet hakuna kinachofanyika...,sasa yeye akishindwa nani ataweza????

    sioni mantiki ya ziara za namna hii kama hazina matokeo....mombasa wako safi pamoja na kuwa kibaki hajapata kutia mguu pale zaidi ya kumtuma Raila mara moja tu!

    akiwaendekeza itabidi awe anaenda kila siku na mwisho haitasaidia ....

    ReplyDelete
  28. Mrundikano huo bandarini,hivi hapa nchini tutaendelea kuitegemea bandari moja tu ya Darisalaama hadi lini? Ni kipi kinachotukwaza tusifikirie kuzipanua na kuziboresha Bandari zetu za Tanga,Bagamoyo,Lindi na Mtwara?Kuhusu hilo hivi kweli tutaendelea kusubiri ushauri na misaada kutoka nchi zanje? Hii ni aibu.Bandari hizi japo ni zetu Watanzania,lakini SIYO ZA KWETU PEKE YETU! Majirani zetu ambao nchi zao hazikubahatika kuwa katika mwambao wa bahari na hivyo kutokuwa na Bandari siyo kwa mapenzi yao bali kutokana na sababu za kijiografia na kihistoria,nchi kama za Rwanda,Burundi,Eastern DRC Congo,Zambia,Malawi,Uganda,nk, nchi zote hizo na wao pia wana haki na kila sababu ya kuzitumia Bandari zetu!Tena kwa gharama nafuu sana karibu ya bure!Tusiwaadhibu hawa ndugu zetu kwa kukosa Bandari,basi tukaligeuza hilo kuwa Mtaji wa Kibiashara na kutoza Ushuru Mkubwa mno kupita kiasi.Iwapo kuziendesha Bandari hizo sisi wenyewe tumeshindwa,basi tusione haya kuwashirikisha hawa majirani zetu katika kuchangia gharama za kuziendesha na kuziboresha kwa manufaa yetu wote.Lingine la muhimu ambalo hapa ndio mahala pake kulikumbushia ni lile linalohusu utozaji wa aina zote za Kodi na Ushuru wa Bandarini kwa Bidhaa zote zitokazo nchi za nje (import duties / excise tax ).Rais Kikwete badala ya kulalama tu kuhusu ukwepaji wa kulipa ushuru bandarini,mimi binafsi ningerudia tena wito wangu kwake,hebu afanye tathmini ya kina kuhusu Viwango vya Kodi na Ushuru vinavyotozwa hapo bandarini Darisalama!Ushuru utalingana na bei ya gari lingine jipya uliloliagiza na hata kuzidi?Why is this so?are those repressive taxes justified?why tax consumers so heavily?to whose advantage?Gari la aina hiyo hiyo kutoka nchi ileile moja na kuletwa na meli ileile Darisalama,gari hilo utalinunua nchi za jirani kwa bei nafuu zaidi kuliko ukilinunua palepale Darisalama,licha ya ukweli kwamba gharama za uchukuzi wa gari hilo toka Darisalama hadi nchi hiyo ya jirani zingelifanya gari hilo kuwa ghali zaidi katika nchi za jirani kuliko hapahapa nyumbani!Ukichukua Ushuru huo mkubwa wa bandarini UONGEZE RUSHWA ILIYOKITHIRI,basi bei za bidhaa zinalazimika kuwa ghali mno!Na mtu atakaye umia na kuatirika zaidi katika hilo ni MLAJI WA MWISHO,mwananchi wa mitaani ambaye ndiye mlipa kodi na ndiye mpiga kura!Serikali yetu imejisahau kiasi ambacho kinahatarisha mustakabali wa nchi yetu!Serikali sasa imegeuza Mapato yake yatokanayo na Kodi kutegemea zaidi mapato yatokanayo na kodi na ushuru wa bidhaa za nje bandarini!The country's Tax Revenue is so heavily dependent on Imports Taxes (import duties,levies and excise tax).This is extremely dangerous to the economy!Tumekuwa tukishauri serikali iangalie uwezekano wa kupanua wigo wa kutoza kodi na ushuru (expanding the tax base),BUT,this has only met Lipstick Diplomacy and political rhetorics!NOTHING DOINGS AT BEST!Punguzeni ushuru na kodi bandarini wa bidhaa za nje ili kudhibiti MFUMUKO WA BEI,wapi,kila mtu katia pamba masikioni,kila mtu kanogewa na ulaji!Hakuna anayejali kwamba uchumi umezidi kuporomoka zaidi na kuwapa majirani zetu nafasi ya kujiimarisha zaidi katika viwanda na uzalishaji katika sekta nyinginezo!Utapunguzaje Rushwa Bandarini ikiwa viwango vya Kodi na Ushuru ni vikubwa mno kupita kiasi? Maana hata utozaji huo mkubwa wa kodi na ushuru bandarini SIO KWAMBA UNAFANYIKA ILI KULINDA VIWANDA VYETU VYA NDANI,not all!What is there to protect anyway?What Industries are you talking about? Utozaji huo mkubwa wa Kodi na Ushuru Bandarini ni KWA AJILI KUTUNISHA MAPATO YA SERIKALI TU ambao una "Boomerang effects"katika uchumi wetu,in the negative corrosive eefect!Eroding away all the successes that have been attained at great cost and sacrifice.The Net Impact to the Battered Economy is what we see in our daily life,that of "exporting domestic jobs overseas",literally killing fragile infant domestic industries,which every Tanzanian would have thought was Kikwete's paramount executive responsibility!But look at what we are witnessing today!That Misuse is Our Tax Money,did you know that? Eti Bunge halina mamlaka ya kuihoji serikali mpaka kwanza itumie,what a joke?----tonnie---

    ReplyDelete
  29. ngoja niwaambieni kitu, hawa wazungu ticts ni wajanja sana, jana wameona rais anakwenda bandarini, wakakataa trucks za kupakia container zisiingie, ili waonekane wao wamemaliza kazi yao ila agents/transporters ndio wazembe, ila jana trucks zote zilikuwa nje!!!, next time JK ukienda usitoe taarifa, vamia kama mwanzo ulivyokuwa unavamia maofisini. kaza buti Mkwele wetu!!!

    ReplyDelete
  30. mimi nakufa na jeans yake na blazer (very sexy)
    sijawai kumwona mkapa amevaa jeans,

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...