mwimbaji maarufu wa taarabu nasma khamisi kidogo (shoto) akiwa na mtani wake wa jadi khadija omar kopa katika hafla moja kipindi cha nyuma.
Nasma Khamis Kidogo, ambaye alitamba kwa vibao kadhaa ikiwa ni pamoja na 'Mambo iko Huku' alipokuwa na Muungano Cultual Troupe, amefariki dunia katika hospitali ya Temeke usiku wa kuamkia leo akiwa anasumbuliwa na ugonjwa wa moyo.
Mipango ya mazishi inafanyika ila bado haijajulikana kama atazikwa Dar ama kwao Kilwa. Habari tutaoa kadri ziavyoingia. Globu ya jamii inatoa mkono wa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki pamoja na wadau wa taarabu kwa kuondokewa na Nasma Khamisi Kidogo
Sio siri kwamba Nasma alikuwa chachu kubwa ya maendeleo ya muziki wa taarabu nchini na Afrika nzima, juhudi ambazo zake yeye na za khadija Kopa ziliwezesha kuzaa 'mipasho' na 'sebene' vinavyotamba kwa sasa katika taarabu ya kizazi kipya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 22, 2009

    innaalillahi wainnaa ilayhi raajiuun! inshl mwenyezimungu atamuhifadhi mahala pake pazuri

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 22, 2009

    RIP Nasma..yaani misupuu nilivyosoma heading macho yamenitoka karibu nipass out jamani.
    poleni familia ya late nasma na wadau wote wa rusha roho

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 22, 2009

    niliangalia namba za mdau wa milioni 6 iliypiita zilikuwa bado kumi na saba alfu leo morning naona bado 65 na ushee kulikono mkuu?

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 22, 2009

    Nawapa pole ndugu wa mama huyu, nilikuwa napenda anavyoimba

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 22, 2009

    Poleni sana watoto wa marehemu, Ahmadi, Aisha wa pale Ukonga- Majumba sita.

    Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.

    Mdau-USA

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 22, 2009

    Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi Inshaalah.

    Mkulima-Kijijini Gezaulole.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 22, 2009

    RIP Nasma.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 23, 2009

    Jamani poleni sana yaani sikuamini niliosoma hii habari kweli imenishtua mno,Mwenyezi Mungu aiweke roho yake mahala pema peponi vilevile awape nguvu ndugu na jamaa wote wa marehemu.
    mdau scandinavia.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 23, 2009

    Michuzi, can you please put a link of one of her songs? Thanks.
    Mdau

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 23, 2009

    "This world is not my home I'm just a passing through
    My treasures are laid up somewhere beyond the blue
    The angels beckon me from heaven's open door
    And I can't feel at home in this world anymore
    Oh Lord you know I have no friend like you
    If heaven's not my home then Lord what will I do
    The angels beckon me from heaven's open door
    And I can't feel at home in this world anymore

    I have a loving mother just up in Gloryland
    And I don't expect to stop until I shake her hand
    She's waiting now for me in heaven's open door
    And I can't feel at home in this world anymore
    Oh Lord you know...
    [ guitar ]
    Just over in Gloryland we'll live eternaly the saints on every hand are shouting victory
    Their songs of sweetest praise drift back from heaven's shore
    And I can't feel at home in this world anymore
    Oh Lord you know" by Jim Reeves
    R.I.P Mama

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 23, 2009

    Namuombea Mungu amlaze mahala pema...Inasikitisha sana....
    Hii ndiyo siri ya Mungu haitakaa ijulikane kamwe....Yani kila mmoja angekuwa anajua atakufa lini nadhani tungepata muda tosha wa kuagana na vile vile kutubu...
    Sauti yake ilikuwa nzuri sana hasa akiimba nyimbo za kubembeleza a.k.a mahaba. Tutabakia kumuenzi kwa kuzisikiliza nyimbo zake.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 23, 2009

    Mungu akulaze mahali pema peponi, tulikupenda lakini mungu kakupenda zaidi, hapa siyo nyumbani kwetu , sote tu safarini, umetutangulia nasi tutakufuata. R I P NASMA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...