eapoti ya uwanja wa ndege wa kimataifa wa
julius nyerere jijini dar unavyoonekana usiku
hakika unavutia

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 34 mpaka sasa

  1. Wadau hebu nielimisheni nimekuwa nikipitia haya makala ya yanahusu matatizo ya uwanja wa ndege wa jk nyerere lakini nisichoelewa watu karibu wote wanaandika Eapoti ya uwanja wa ndege wa julius nyerere. Ningependa kujua nini maana ya Eapoti na nini maana ya uwanja wa ndege maana naona kama eapoti ndio uwanja wa ndege au mimi ndio nakosea ni kama kusema '' barabara ya ocean road'' nifahamisheni wadau maana hata uncle naniii nae kaandika hivyo hivyo.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 27, 2009

    Jamani Suala la udokozi AIRPOT tufanyeje? Nafahamu kuna watu waliokaribu na may be Waziri anayehusika au Hata Rais, jamani mtusaidie kuondoa hii aibu wapeni ujumbe. Sasa kama mtu unabord ndege Canada halafu unapewa onyo uwe macho ukifika Dar, Je mtalii si ataahirisha hata safari kabisa au atashukia Nairobi! Please tusaidiane kuondoa hii aibu

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 27, 2009

    Ni kweli inaonekana vizuri, ni kweli ina jina zuri la Baba yetu wa Taifa. Lakini kama uongozi utashindwa kurejesha heshima ya huu uwanja kwa kuwakamata wezi/wadokozi wa mizigo yetu, hakuna haja ya kuendelea kutumia jina la Nyerere, bali wabadilishe jina na kujiita FISADI INTERNATIONAL AIRPORT!!!!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 27, 2009

    Ni kweli kumependeza; ila kama huduma za uwanja wetu zingekuwa zingara kama sehemu yenyewe naona watu tusingekuwa tunalalamika kuhusu wizi wa mizigo.

    Mara ya mwisho nilivyopita pale nakumbuka hata parking zilikuwa ni mbinde kinoma, I hope walishaweka ila kitu sawa.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 27, 2009

    Panafanana na wizi wa mabegi ya watu.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 27, 2009

    Ni kweli mandhari inavutia ukiwa kwa nje kama panavyoonekana, Ila sasa ukitaka kuona rangi zote kwamba kunavutiaje utokee ule upande wa kule nyuma ya yale maandishi makubwa utajua kuwa kunavutiaje!

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 27, 2009

    SAMAHANI MDAU, LAKINI INGEKUWA BORA ZAIDI KAMA UNGETUDOKEZEA TU NI NINI HAPA KINACHOVUTIA HASA!
    MAANA KWA UPANDE WANGU SIKIONI, SAMAHANI SANA.
    NACHELEA ISIJE KUWA NI TABIA KWAMBA KILA MWENYE PICHA ZAKE ANAZITUMA TU KWENYE BLOG YETU YA JAMII, NA KUDAI ZINAVUTIA!
    HUU SI MTINDO MWEMA, MAANA SI LAZIMA KILA CHAKO KIWE KIZURI, KWANI TABIA HIYO INAWEZA KUKUAMBUKIZA MARADHI YA KUJIBWETEKA, UKAACHANA NA JUHUDI ZA KUJIBORESHA.
    KATIKA ULIMWENGU HUU ULIOJAA VIWANJA VYA NDEGE VYA KUVUTIA HASA, TUSEME KWELI, KIWANJA CHETU BADO HAKIJAFIKIA KUWA NA SIFA YA "KUVUTIA".
    KAZI KUBWA KWELI KWELI INAHITAJIKA KUKIIMARISHA, NA KWA MAONI YANGU, WADAU, KABLA KWANZA YA KUTUMA ITEMS ZETU NA TUFANYE UTAFITI LINGANISHI DHIDI YA ITEMS NYINGINE.
    KWA MFANO, MDAU HAPA ANGEJARIBU KUTAFUTA PICHA MTANDAONI ZA BAADHI YA VIWANJA VYA NDEGE VYA NCHI ZA AFRIKA, ASIA AU MASHARIKI YA MBALI, AONE VINAVYOVUTIA. KWENYE GOOGLE VIKO KIBAO. AKIVILINGANISHA NA HICHO CHA KWETU, ATAELEWA NAKUSUDIA KUSEMA NINI.
    NA SINA MAANA YA KUZIBEZA ITEMS ZA NYUMBANI. MAANA YANGU NI HIYO HAPO JUU.
    AHSANTE
    Mndengereko, Ukerewe

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 27, 2009

    Mbona giza namna hiyo?Ni hatari kwa usalama wa hapo eaport ndani kumependeza lakini nje kwenye car park ni giza totoro which is not safe for everyone.hata camera za usalama hazitoonyesha vizuri.
    eapot kuna takiwa kuwe full mwanga siyo namna hiyo, hebu michu jaribu kuongea na wahusika acha uwoga na wewe.kama kukuloga hawakuwezi, feza unazo,contact unazo hadi ya mzee kikwete, uzalendo unao sasa kwanini usiwaibukie maofisini kwao na video kamera yako...ACHA UWOGA MICHU.
    MUNGU IBARIKI GLOBU YA JAMII
    MUNGU MPE NGUVU NA UJASIRI MICHUZI.
    CHAO.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 27, 2009

    UZURI WA JENGO SI KITU SI TUNATAKA UTUTUMIE PICHA YA WFANYAKAZI WA HAPO ILI TUWAJUE WANAOTUIBIA VITU VYETU BILA HURUMA TUZIONE SURA ZAO TUNAWAKEME KWA JINA LA MKUU WA WAFALME WASHINDE NA WAMJUE MUNGU ALIYE HAI LA SIVYO DAWA YAO INAKUJA NA WATAJUTA KWANINI WALIIBA

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 28, 2009

    Jamani unavutia hayo maneno au? yaani giza lote hilo bado unaonekana unavutia? kweli bongo tambarare! Hivi hatuoni viwanja vya wenzetu?

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 28, 2009

    Sitamani hata kupaona .
    Hapo hakuna usalama wowote wa mtu anayejishukia ndege na tumzigo twake,mimi sitasahau leptop yangu na camera yangu,,,natamani kushukia sehemu nyingine nikiludi hapo bongo,

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 28, 2009

    HATA MIE NIKIPAONA NATAMANI HATA NITAPIKE. WAFANYA KAZI CUSTOMER SERVICE MBOVU SIJAPATA KUONA, WANA MAJIBU UTADHANI WATU TUNAPANDA NDEGE BURE. WANANUKA WIZI TU MACHO YAMEWATOKA KWENYE MABEGI YA WATU TUU.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 28, 2009

    Nilivyokuwa na hasira na hawa jamaa, nitamtoa mtu mshipa! Wanacheza na mimi hawa, Ngoja nimpigie simu Babu, Hiyo ndio dawa yao hamna nyingine, Si wanajifanya wajanja sio? Subirini, Mtasikia...

    Uwanja wa ndege TZ, Dawa yenu ipo jikoni...

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 28, 2009

    Acheni kelele, mbona mahala kwingine hampigii kelele kama hizi? Kila mtu ala kazini kwake ati! Nyie wenyewe mjitazame mienendo yenuu kwanza? Posho za burebure,marupurupu kila aina safari,nyumba,mfanyakazi,gari ofisi,hamlipi bili za maji umeme,forgery na mambo lukuki. Mlipo sema mambo uria hamkujua madhara yake eeenhe? Kama shule tumesoma ile ile mliyonayo inakuwaje nyie mjipe haki zaidi? Si halalishi wizi ila ni matokeo ubinafsi wenu ndio umetufikisha hapa. Mie nadunda kazini kwangu mwenye wivu ajinyongeeee

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 28, 2009

    HATUTAKI PICHA ZA KUPENDEZA, TUAMBIENI HATUA KADHAA ZIMECHUKULIWA NA SASA "NO WIZI WA MIZOGO" maana ni AIBU KWA NCHI.

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 28, 2009

    anoni wa 10:14 acha kujigongagonga kwa michuzi!!! michuzi mwenyewe chapa ya mombasa ohooo!!!

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 28, 2009

    michuzi hauko serious. hivi haka kauwanja unaweza kukafananisha na eapoti ya Jomo Kenyatta airport?? haka kwanza kana terminal ngapi kama sio moja tu wakati wenzetu pale uwanja wa ndege wa jomo kenyatta airport wana terminals 12?? eapoti inayovutia zaidi afrika mashariki ni jomo kenyatta na kwa afrika nzima ni Johannesburg/jobegi.
    Uwanja wetu una kila aina ya uozo.
    1. ka-uwanja ka-baya na kadogo
    2. Ufisadi uwanjani hausemekani
    3. WAFANYAKAZI WA UWANJANI HAPO WANA LUGHA MBAYA MBAYA MBAYA KUPINDUKIA
    4. HAO WAHINDI WALIOPEWA TENDA YA KUENDESHA HUO MGAHAWA PALE WAITING ROOM WAMEIGEUZA TANZANIA KUWA LONDON VYAKULA VYAO WANACHARGE BEI ZA KUUWA MTU KWA KUWA WANAJUA WATEJA WANARUKA MAMTONI KWA HIYO WANA MAPOUND AU MA $.
    5. MAPOLISI WANAOWEKWA EAPOTI NI WALA RUSHWA NA HAWAFANYI KAZI YOYOTE ZAIDI YA KUKUANGALIA USONI NA KUOTEA KAMA UMEBEBA COCAINE
    6. WALE WAFANYAKAZI WANAOKAA PALE KWENYE CHECK INN DESKS WAKIWAKILISHA AIRLINES MBALIMBALI NDIO PEKEE WENYE LUGHA NZURI HAPO UWANJANI LABDA KWAKUWA KWAO WAO MTEJA NI MFARME, LAKINI KWAKWELI WAO KIDOGO WANA LUGHA NZURI
    7. PALE TUNAPOKAGULIWA PASSPORT NA KUJAZA VILE VIKADI VYA IMMIGRATION PALE KABLA HAUJAKUNJA KULIA NA KUKWEA VILE VINGAZI KWENDA WAITING ROOM, HAO WAFANYAKAZI WA UHAMIAJI HAPO WANA LUGHA MBOVU NA WANAJIFAANYA UTADHANI WAO NDO WANAKWENDA ULAYA WAKATI MIMI NDO KIDUME MWENYEWE NINAYERUKA
    8. WAFANYAKAZI WA UHAMIAJI KWENYE HIZO POINTS ZA DEPARTURE NA ARRIVALS WAJITAHIDI KUONGEA LUGHA ZA KIGENI VIZURI KWANI WATAMBUE SI WOTE WAPITAO HAPO WANABONGA KISWAHILI
    9. MWISHO: WAFANYAKAZI WA KITENGO CHA KUPAKIA NA KUSHUSHA MIZIGO WA SWISSPORT HAPO DAR EAPOTI JAMANI WAFUNDISHWE HOSPITALITY WAACHE WIZI. HAO WATU WANAIBA MALI ZA WATU BILA HURUMA, MI JAMANI IPO SIKU NTAKUJA KUWATEGESHEA LIJOKA TENA COBRA, ILE AKIFUNGUA TU MZIGO WANGU ANALO USONI PWAAAAA WAKIMFIKISHA MUHIMBILI SAA NGAPI SUMU ISHAPITIA MOYONI OHOOO!!
    10. NARUDIA WAFANYAKAZI WA KUPAKIA NA KUSHUSHA MIZIGO UWANJA WA NDEGE DAR MNALIABISHA TAIFA ACHENI KUPORA JASHO LA WENZENU, NYIE HILO NDO BOX LENU KWANINI NASI TUKIPIGA BOX LETU HUKU MNATUIBIA MBONA SISI HATUWAIBII LENU???
    PROFESA WA NORWAY MLIYEMUIBIA LAPTOP NI AIBU KWA NCHI
    mwisho mi nitaanza kuweka nyuki au mi-joka kwenye sanduku langu mkifungua tu na uroho wenu mnalo!!!
    ahsante

    ReplyDelete
  18. AnonymousJuly 28, 2009

    hapo ndio panavutia vitu vya wizi.

    ReplyDelete
  19. AnonymousJuly 28, 2009

    Ahh!we Michuzi mbona unautani mbaya?Ahh hilo giza soo.Uongo sio kazi,kumbe kweli bongo kuna giza.Hapo ni airport,hivi kwa mfuga mbwa kukoje?Khaa hebu ongezeni taa hapo kiwanja na kwenye parking lot.

    ReplyDelete
  20. Ni kweli mandhari inavutia ukiwa kwa nje kama panavyoonekana, Ila sasa ukitaka kuona rangi zote kwamba kunavutiaje utokee ule upande wa kule nyuma ya yale maandishi makubwa utajua kuwa kunavutiaje

    ReplyDelete
  21. AnonymousJuly 28, 2009

    KINGINE JAMANI WAWEKE AIRCONDITION MULE DNANI YAANI KAMA UKIWA UMERUDI TZ YAANI UNATAMANI UTAPIKE HILO JOTO MWEE UNASUBIRA MZIGO UJE MAJASHO YANAYOKUTOKA KICHEFUCHFU RUFU MPYA ZA AJABU JAMANI MWEEE WAWEKE JAMANI HIZO FENI HATA MAANA NILIKUJA 2004 HALI ILEILE HADI SASA LO AIBU CHEKI AIRPOT ZA WENZETU ZINAVUTIA HATA WASIWASI WA KUSAFIRI SIJUI AJALI HUWAZI

    ReplyDelete
  22. AnonymousJuly 28, 2009

    pazuri sana pia kwa wizi ni pazuri!

    ReplyDelete
  23. AnonymousJuly 28, 2009

    jamani huu uwanja ni wizi mtpu.....kila kitu cha hapo uwanjani kimepinda.
    mbaya zaidi wakati wa arrival mnapanga foleni kuelekea kwenye ukagzi wa paspoti, loh...pananuka mikojo...mana vyoo vipo hapo hapo...na hilo joto halisemeki....jirekebisheni tondoe doa....

    ReplyDelete
  24. AnonymousJuly 28, 2009

    mie mwenzenu nilishaamua kuacha haya mambo sababu yanatakiwa kufuatilia right from the top. kama dg wao angekua anafanya spot-visits na kufukuza watu haya mambo hayangekuwepo sana. mabosi wetu wanakaaga tu ofisini ndio maana tuna shida za namna hii tanzania.

    ReplyDelete
  25. AnonymousJuly 28, 2009

    WABONGO SIFA YAO KILA KITU KUPONDA, KULALAMIKA NA MADHARAU TU.ALIYEIBIWA EAPOTI AMEOMBWA AFIKISHE TAARIFA KWA WAHUSIKA ZIFANYIWE KAZI NYIE MNAPONDA HATA HUO USHAURI. MDAU ALIYEFANYA KAZI EAPOTI KAJARIBU KWAELEZA UTARATIBU WA UPAKUAJI MIZIGO NA HILO PIA MNAPONDA. JINSI MNAVYOPIGA VIJEMBE HAPA MNATAKA KUWAGEUZA WAFANYAKAZI WOTE WA EAPOTI WAONEKANE MAFISADI NA WAZEMBE.KUNA WACHAPA KAZI SAFI PALE WANAOJITUMA KWA NGUVU ZOTE LAKINI MTAWAKATISHA TAMAA KWA VIJEMBE VYENU VYA KUKURUPUKA BILA UTAFITI.SOLUTION PEKEE KAMA UMEIBIWA RIPOTI KWA WAHUSIKA TOA FLIGHT NUMBER NA TAREHE YA SAFARI HALAFU KAMA HAIJAFANYIWA KAZI NDIYO ANZA KULALAMIKA.SASA HIYO TABIA CHAFU ITAONDOLEWAJE BILA KUWEPO VIELELEZO? TUNAPENDA SANA KUOSHA VINYWA KWA KUANGALIA UPANDE MMOJA TU WA SHILLINGI.ANGALIENI HATA WAZAWA KUANZA KUSHIKA HATAMU MGODI WA BULYANHULU MNAPONDA!POTELEA MBALI, NIMEAMUA KUWATOLEA UVIVU LEO WAOSHA VINYWA MAANA MMEZIDI MNO KUPAKA. KILA KITU KWENU BONGO KIBAYA.

    Mzalendo Limbukeni.

    ReplyDelete
  26. AnonymousJuly 28, 2009

    hawa mabosi wetu wa iraport ni rushwa tu wanataka na kuagiza chips kuku halafu wanakaa mofisini tu kuongea mambo ya dili, na wapi watapata kula! matumbo tu! jamani mlioko majuu njooni basi muondoe huu ujinga wa dar intarnational mavi airport!

    ReplyDelete
  27. AnonymousJuly 28, 2009

    1) Kweli Mwalimu Nyerere angalijua kuwa uwanja wa ndege uliopewa jina lake una wezi wa mizigo ya abiria kiasi hicho sidhani kama angekubali jina lake litumike.
    2) Anon wa Jul 28 04:42 wacha kujishebedua. Umesafiri kupitia viwanja vingapi vya ndege hadi ujidai kutoa huo mlinganisho. Hapa tunaongelea kutatua matatizo yanayoikabili eapoti yetu ili ukitoka kubeba boxi na vijidolari vyako wasikulize. Ni kweli kuna matatizo, lakini sikubaliani nawe kuwa ni wafanyakazi wote wa Swissport au Uhamiaji wana lugha mbaya kwa wageni na abiria, hiyo siyo kweli. Labda imetokea bahati mbaya kwako kwa sababu unaonekana una tabia ya kujishebedua.

    ReplyDelete
  28. AnonymousJuly 28, 2009

    air port yet inaitwa JULIUS NYERERE INTERNATIONAL AIRPORT. lakini hadi leo hii ukiingia au kutoka nje mihuri yao imeandikw DIA (DAR ES SALAAM INTERNATIONAL AIR PORT) watu anashindwa kubadilisha mihuri wanataweza kubadilisha nini tena? to be honest wabongo tunanuka..........

    ReplyDelete
  29. AnonymousJuly 28, 2009

    Wabongo tunajidanganya!! Reputation ya nchi yetu ilivyo nje na hako ka-eapoti chetu na ukiongezea wizi wa mizigo ya abiria na urasimu wa wafanyakazi ni aibu tupu!!! Ni moja ya eapoti mbaya na ya kizamani barani Africa!!!

    ReplyDelete
  30. AnonymousJuly 28, 2009

    Yaani hapa nimefanya booking yangu ya ndege kutoka hapa Ughaibuni kuingia Dar kama baada ya week 2 nasikia kichwa kinaniuma kabisa, manake nina vifaa vingi vya electronics, nimejaribu vyote kuviweka kwenye handluggage lakini naona haiwezekani kutokana na limitation ya size and weight ya handluggage. Nitajaribu kubadilisha flight yangu nishukie Kenya, nikishindwa naona nitapata pressure! manake wadau mmenitisha. Naombeni ushauri nifanyeje ili vitu vyangu vipite salama manake siwezi kuviweka vyote kwenye handluggage.

    ReplyDelete
  31. AnonymousJuly 28, 2009

    Welcome home, lazima mkaribishwe ili mjue kuwa hii ndio bongo-Bongo Dar-es-salaam!
    Unapoingia mjini unafutwa matongotongo,ili uone vizuri. Poleni sana mlioingizwa mjini. Sio kwamba nawakebehi, ila nawaonyesha jinsi gani nchi yetu ilivyo. Mkiwa nje mnajisahau, mnakalia kufungua matawi ya VYAMA, Sasa hayo ndio matokeo yake.
    Tumekuwa tukiwaimbia kuwa nchi yetu inanuka ufisadi hamtaki kuelewa, mnaona kama tunawawekea kauzibe,sasa myaone kwa macho. Hii ni kama babaisha toto, hamjatulia home,mtayaona mengi.
    Welcome home and pole sana, sisi tukitumiwa vizawadi kwa njia ya posta tunabakiwa kusaini makatatasi nakubambikiwa gharama kubwa, ili tushindwe kulipa,na vikirudishwa ndani ili ukatafute hela ukirudi unaambiwa hakuna kitu.
    Karibuni home na mjisikie nyumbani

    ReplyDelete
  32. AnonymousJuly 28, 2009

    Ebu chukueni hii wadau, ni ya mda kidogo ka miezi 9 ivi imepita!
    Si Bro. alitaka nkamsalimie pale Cansas city,siunajua tena mambo ya kusafisha macho huko mbele kwa wenzetu weupe? Kimbembe sasa wakati wa kurudi pale kwenye Airport ya Ticha! mama yangu Ki-digital kamera changu,Ki-lapjuu changu,vijisimu vya wazee home,na vizaga zaga vya madenti pale home duh aiubu hadi leo sijawahi kuviona tena mara ya mwisho nlivicheki Shem alipokuwa akivifungasha pale home kwa Bro! Huyo anaesema eti unashulikiwa ukiibiwa ni mwongo mi nlifika hadi uongozi wa juu wakaishia njoo kesho mara njoo kesho kutwa bado tunawasiliana na watu wa security(afu siunajua vitu vyenyewe nlimpiga bomu Bro yaani inauma kinoma)nlitembea hadi nkaishiwa nauli za kutoka KIBAMBA-G'MBOTO,basi mi nkafikili wameniotea labda kwasababu ilikua first time(kumbe hata wazoefu?) sasa nshapanga kama nkipata zari tena Bro akani-call ntashukia Entebbe npitie MTUKULA nkasalimie home pale KAMACHUMU kidogo then ntimbe-DSM.
    By Mdau Mbeki 4rm St.Joseph College of Engineering & Technology(CoET)Brigita Campus-DSM

    ReplyDelete
  33. AnonymousJuly 28, 2009

    Hat KLM wapima mizigo ni wezi tu, mara utasikia mzigo umezidi, zaidi wanmwita supervisor, na kunagalia mzani mara utasikia dada anasema inabidi huyo alipie. Mara akiondoka mpimaji anakwambia niwekee pesa kwenye Passport yote tutayaweka sawa. Kumbe hata uzito huo unakuwa umebambakikiwa tu. Hap Uwanja wa ndege Bongo kuna uozo wa hali ya juu sana tena Sana panuka wala rushwa na unyanyasaji wa hali ya juu sana.

    ReplyDelete
  34. AnonymousJuly 30, 2009

    jamani we michuzi unakuwa kama uajsafiri na kuona viwanja vya ndege vya watu?mlitudanganya na kutengeneza uwanja kwa nje lakini embu ingia ndani kunanuka tena afadhali wakati wa kuingia kuliko kutoka yani ndio umefika tz na marafiki zako ambao umewasifia kuhusu nchi yako ukifika airport unaanza kusikia aibu ruswa imejaa sakafu na majengo ya ndani machakafu hata kupiga rangi basi kupendeze unakuta vijana wamevaa nguo chafu wao kazi yao kusubiri wanaokuja na kujidai kuwaelekeza jambo kumbe wanataka kuiba au wapewe pesa jamani tunatia aibu watanzania.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...