JK akifunua kitambaa kufungua rasmi jengo jipya la ubalozi jijini Washington Marekani leo asubuhi
Jengo jipya la ubalozi jijini Washington Marekani ambalo JK alilifungua leo asubuhi. Jengo hili limenunuliwa na serikali ya Tanzania kwa jumla ya dola za kimarekani $10,415,000. Chini JK akisaini kitabu cha wageni katika ofisi ya Balozi iliyopo katika jengo jipya la Ubalozi wa Tanzania jijini Washington Marekani leo asubuhi.Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe na wapili kushoto ni Balozi wa Tanzania Washington Ombeni Sefue

JK akisalimiana na wageni mbalimbali na mabalozi waliohudhuria sherehe za ufunguzi wa jengo jipya la ubalozi jijini Washington Marekani zilizofanyika leo asubuhi.
JK akitoa hotuba yake wakati wa ufunguzi wa jengo jipya la ubalozi jijinji Washington Marekani leo asubuhi. Picha na mdau Freddy Maro wa Ikulu





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. why no picture of Mkapa and Obama in the background... that would be more approp.

    ReplyDelete
  2. Duh!! Bilioni kumi za kitanzania hivi hivi zimeenda yaani. Lakini kama watumishi ubalozini wataongeza kiwango cha utendaji kazi maradufu shwaaari tu.

    ReplyDelete
  3. TUOMBE MSAHADA WA RAIS WA RWANDA AONGOZE NA TANZANIA.JK APEWE NAFASI ZA KUWAKILISHA TZ NA RWANDA NCHINI USA.

    ReplyDelete
  4. KWA KWELI WATANZANIA TUNAHITAJIKA KUTAWALIWA TENA ILI AKILI ZETU ZIFANYE KAZI, SHILINGI BILLION KUMI KWA UBALOZI KWA NINI? NYUMBA YA DOLLAR HATA MILLIONI 3 INGETOSHA KUWA OFISI YA NCHI MASIKINI KAMA TANZANIA

    ReplyDelete
  5. Hongera Rais Kikwete kwa kututoa aibu; sasa na New york pia

    ReplyDelete
  6. Si mnaona bwana. Ziara za nje zimeleta matunda, sasa hivi tumejenga jengo la kisasa la ubalozi Marekani.

    ReplyDelete
  7. Khaa!Hatimaye ubalozi unapata sura mpya.Ofisi utadhani unaenda mabanda ya uani uswazi..na wafanya kazi mbadilike maana tabia zenu za utendaji kazi..mmmhhh???Nakumbuka nilivyomleta mzungu wangu wa karatasi hapo wakati na mzuga mtadhani mpo bongo..mnajua nina maana gani..na wale wenzangu na mie tuliofika hapo mnajua fika.

    ReplyDelete
  8. Haya sasa, tumepata jengo swafi ambalo limetugharimu zaidi ya TShs bilioni 13 pesa ya walipa kodi.
    Tunachotaka sasa ni wafanyakazi wa ubalozi kuchapa kazi. Wachape kazi haswa!
    Tunatarajia mazingira mapya ya kazi yatawasaidia kuongeza ufanisi, kuhakikisha pamoja na kutekeleza majukumu yao ya kibalozi kwa wenyeji wetu hapa Marekani, lakini pia wawe mstari wa mbele kusaidia na kusikiliza matatizo yetu sisi wananchi!
    Tunawatakia kila lakheri.

    ReplyDelete
  9. Mbona first lady wetu aonekani kwenye safari za nje siku hizi?

    ReplyDelete
  10. Kweli watanzania bado tuna kazi , hiyo picha hapo juu ya ukutani inayomuonyesha JK na Bush yaani jina la nchi limeandikwa kwa herufi ndogo zote ...

    ReplyDelete
  11. KAULI YA JK KUWA HAJASHINDWA KUTATUA TATIZO LA ZANZIBA NI KAULI YA KIONGOZI ANAYETEGEMEA KUTUMIA NGUVU ZA JESHI DHIDI YA WAPINZANI KUWA ANAO UWEZO WA KUZIMA TATIZO LA HUKO KWA KUTUMIA SILAHA; HIVYO ANAACHA LIKUE APATE SABABU ZA KUTUMIA NGUVU.

    ReplyDelete
  12. Hongera serikali kwa kununua Jengo la Ubalozi.Ingawa pesa ya kununulia inaonekana nyingi lakini in long term faida yake itaonekana, kwa kuwa gharama za nyumba huku nje zinapanda kila mwaka kwa hiyo hilo jengo sio tu Ubalozi lakini pia ni Investment ya nchi.

    ReplyDelete
  13. Mbona mnaimind sana hiyo hela? Cha maana ni Jengo hilo limepatikana, baada ya miaka 10 hiyo hela thamani yake itakua sio sawa na hilo jengo tena,Thamani ya majengo inaongezekaga kulingana na mda,population na mambo mengine kibao.Msipende hela sana watanzania.

    ReplyDelete
  14. bush is history, wekeni picha ya JK na BO

    ReplyDelete
  15. lile la zamani lilitia aibu mno, nadha lilijengwa labda 1890,sasa tunaweza alika wageni wa kwanza Obama

    ReplyDelete
  16. Ukimuona mtu kateuliwa kwenda kuhudumu kwenye Ubalozi nje, ujue basi huyo mtu ni hatari katika medani za kujipanga.

    Nawavulia kofia - mko ju ka' helikopta ya polisi.

    ReplyDelete
  17. Jamani hili engo ni lile lile au ni jipya ? Nakumbuka jengo la ubalozi wa Tz in DC , halikua lime choka sana lakini, ingawa kweli sijui kama ile lift ilikua inafanya kazi, maana ukipanda ngazi zinaiga kelele na lile carpet jekundu dah, hivi yule mama wa Ki black America pale reception ( sijui alikua anaitwa Getrude) bado yupo?, mana lazima atakua na maika 90 sasa.

    ReplyDelete
  18. Je tumelipa cash au tumechukua mkopo bank za marekani, kama ni mkopo mpaka tumalize kulilipia thamani yake itakuwa dollar milioni mia moja na hamsini(US $150) hiyo ni pamoja na riba! Kama tumelinunua kwa cash hiyo ni faida kubwa na lina hadhi ya kimataifa. Milioni 10 sio nyingi kwa Taifa ni nyingi kwa mtu binafsi. Tuna kila lasirimali na uwezo wa kununua hilo jengo. Wee jamaa wa juu Tanzania sio masikini hata kidogo ila watu wake ndo tunaakili za kimasikini tuna utajiri wa kutosha ila ufisadi ndo unasumbua!
    Hongera Mheshimiwa Kikwete kwa kuidhinisha ununuzi wa jengo jipya You mean business. You Rock JK! Next year tutakupa free ticket umelizie kazi!
    Mdau USA

    ReplyDelete
  19. DO WE REALLY NEED THIS SIMBA SPORT CLUB BUILDING

    ReplyDelete
  20. Nasikia Serikali inampango wa kuwauzia majengo ya ubalozi wake watumishi wa serikali.Zoezi hilo ni kama walivyouza nyumba za serikali kaeni mkao wa kula.

    ReplyDelete
  21. WIZI WA 10% NAJUWA HII MICHUZI HUTATOWA KWA WOGA WAKO SI WEWE NI SISI TUNASEMA. UNA-BORE

    ReplyDelete
  22. Mh Hongera Tanzania kwa kununua jengo la bilioni kumi USA kwa ajili ya Ubalozi. Mi najionea uzushi tu, ni sawa na kusafisha kikombe nje wakati ndani kuna funza. Rais jenga Fry-overs bongo watu tujinome na magari na tuweze kujenga nchi kwa haraka. Foleni za bongo, deal moja unafunga siku moja. China siku moja waweza close deals 10 kwa uhakika wa usafiri. Halafu fry-overs zenyewe wala huitaji kutoa hela mfukoni,kama tunakopa, basi tukope kwa ajili hiyo pia, hasa kwa jiji kama Dar. Naipenda sana nchi yangu ila najionea uzushi tu sometimes.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...