katika kuonesha umahiri na ubunifu wa hali ya juu ulioipeleka jahazi modern taarab katika bahari kuu ya muziki huo nchini, mzee yusuf na kundi lake sasa wana madansa katika maonesho yao ambao linapopigwa sebene hufanya vitu si vya kawaida jukwaani. hii ilikuwa usiku wa kuamkia leo katika ukumbi wa bwawa la kuogelea wa city garden hotel gerezani (zamani railway club) dar
mzee yusuf akiongoza jahazi wakati wa shoo hiyo kali
mbunge wa temeke mh. abbas mtemvu alishindwa kujizuia na kuja kumtuza mzee yusuf kwa vitu vyake vya uhakika.
baadhi ya malkia wa jahazi
mpiga kinanda anayepagawisha
mkono wa dhahabu akipeleka wadau dubai huku shoto akionekana thabiti mtoto wa ilala akipapasa kinanda. listi imetimia jahazi modern taarab






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Jahazi litazama kwakuwa ndombolo sasa

    ReplyDelete
  2. Mh,hii mpya sasa sio kihivyo MZEE unahitaji ubunifu mpya sio huu,kaa chini utafakari wapi ulopojikwaa sio kama hivi

    ReplyDelete
  3. hongera, kaka kumbe bado upo juu mpaka Mh, kakubali, Jahazi juu juu juu kabisa.

    ReplyDelete
  4. Nakumbuka zamani nakaa hapo Gerezani nyumba namba 13 (Nyumbani kwa kina Matusi)Tulikuwa hatulali usiku ni makelele ya Bendi au harusi kwenye ukumbi wa Gerezani.Nafikiri uwepo utaratibu wa kutoa huo uchafuzi wa mazingira mpaka sasa tumeadhirika na makelele hayo toka utotoni mpaka sasa!!

    ReplyDelete
  5. Brave! lakini hilo koti halikuchomi na joto kweli kaka yangu?

    ReplyDelete
  6. Taarab na wanenguaji wapi na wapi??. Mzee Yusuph bibi yako ni Bi kidude nenda akakupe funzo la Taarab mana hii sio Taarab bali ni unashindana na twanga sasa,

    ReplyDelete
  7. mkubwa Taarab ya sasa ni mabadiliko makubwa sana , taarabu ya zamani Gita si la umeme watu wanakunywa kahawa akuna bia, karibu kwenye maisha ya ki leo, hongera mzee yusuph.

    ReplyDelete
  8. Hii siyo taarab.

    ReplyDelete
  9. Wa Gerezani namba 13, Nyumbani kwa kina Matusi.

    Kwanini hukuwauliza wazazi wako kwamba nani kaanza kujenga hapo? hio club au nyumba namba 13?
    Kama club ndio ya kwanza kujengwa basi waliyajua toka mwanzo matokeo yake

    ReplyDelete
  10. Hivi mzee unataka kutuhuzunisha sisi wapenzi wako wa sauti yako na taarabu zako,,haijakuwepo taarabu kunengua kama kina werason au twanga pepeta! ah,,labda nafuu uhamie huko tu.Sio ugeuze taarabu iwe ndombolo ya solo.

    ReplyDelete
  11. mmh! Koti la ngozi bongo?

    ReplyDelete
  12. Kama hataki nipe mie, nipe mie, nataka paja,haya-yaya-yaya-yaya-yaya-yaya-ya! kipapatio!

    ReplyDelete
  13. Khe! mzee yusuph jiachie mwaya,wanaokuponda hawajui taarabu.mabadiliko babu.linawahusu!scince na technolojia.wape vitu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...