JK akizindua wilaya ya Kilolo leo mchana. Aliyenyanyua mikono juu ni mkuu wa wilaya hiyo Dr Athuman Mfutakambapata
JK akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa chuo cha maendeleo ya jamii Ruaha Iringa pamoja na wanafunzi wa chuo hicho ambao walimwimbia nyimbo nzuri ya kilimo Kwanza
Picha na Habari na mdau wa Iringa
RAIS Jakaya Kikwete leo amezindua makao makuu ya wilaya ya Kilolo mkoani Iringa na kuipongeza halmashauri ya wilaya hiyo kwa ujenzi wa jengo la ghorofa la kisasa kwa ajili ya halmashauri ya wilaya hiyo jengo ambalo limejengwa kwa gharama nafuu ukilinganisha na halmashauri nyingine nchini ambazo zimejenga majengo madogo kuliko hilo kwa gharama kubwa.

Akiwahutubia mamia ya wananchi wa wilaya ya Kilolo katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya ofisi ya mkuu wa wilaya hiyo mara baada ya kuzindua miradi mitatu ukiwemo wa umeme,jengo la halmashauri na ofisi ya mkuu wa wilaya ya Kilolo,Rais Kikwete alisema kuwa kwa upande wake amefurahishwa na uaminifu mkubwa wa halmashauri hiyo katika kusimamia fedha za serikali kwenye ujenzi wa majengo hayo.

Rais Kikwete alisema zipo halmashauri ambazo zimejenga majengo madogo kuliko hayo ila ukitazama gharama zilizotumika ni kubwa kuliko gharama zilizotumika kujenga jengo hilo la halmashauri ya wilaya ya Kilolo ambalo ni jengo la kisasa ukilinganisha na majengo yaliyojengwa katika halmashauri nyingine kwa gharama kubwa.

"Kweli halmashauri ya Kilolo pamoja na makandarasi na wataalam wengine wote mlio shiriki kujsimamia ujenzi wa jengo hilo napenda kuwapongeza sana kwa uaminifu mkubwa mlioonyesha katika ujenzi wa jengo hilo....nasema nawapongezeni sana"

Rais Kikwete alisema kuwa ujenzi wa makao makuu ya wilaya ni moja ya utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM ambao iliahidi kuwa miundo mbinu yote ya makao makuu ya wilaya kujengwa kisasa kabla ya mwaka 2010 kazi ambayo utekelezaji wake umekuwa ukifanywa kwa nguvu zote.

Hata hivyo alisema kuwa huduma kubwa katika halmashauri hiyo ni hospitali ya wilaya ambapo mbali ya kuwa katika wilaya hiyo ipo hospitali teule inayofanya kazi kwa ushirikiano na kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) ila bado serikali ina mpango wa kujenga hospitali ya serikali.
Rais Kikwete alisema kuwa kuanzisha wilaya bila kuwa na huduma za kijamii kama ofisi na ubora wa miundo mbinu ni sawa na kuwabebesha wananchi mbuzi katika gunia.

Awali mkurugenzi mtendaji wa halamshauri ya wilaya ya Kilolo Bosco Ndunguru alisema kuwa jengo hilo lina ofisi 56 ,stoo 4 ukumbi mkubwa mmoja ,kumbi ndogo 2 pamoja na vyumba vingine vingi limewajali watu wenye ulemavu pia kwa kuwatengea maeneo yao.

Alisema kuwa makisio ya ujenzi huo yalifanywa mwaka 2006 /2007 ambayo yalikuwa ni shilingi 2,321,004,000 huku ujenzi halisi utagharimu shilingi 2,005,199,468Bofya hapa
Habari zaidi na picha

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Ushauri wa bure kwa JK. 'Utekelezaji wa ilani ya CCM' imekuwa too much. Kila kitu ilani, ilani, ilani. Wabongo kibao tuliokupigia kura hatumaindi mambo ya kichamachama tunajua serikali tu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...