Waziri wa Nchi ,Sera, Uratibu na Bunge Philip Marmo akitoa salam za pole kwa familia ya marehemu Rashid Mfaume Kawawa kwa niaba ya ofisi ya Waziri Mkuu ambayo iliratibu mazishi ya marehemu mzee Rashid Kawawa Jumatano jioni kijijini Madale jijini Dar es salaam.
Waziri wa Nchi ,Sera ,Uratibu na Bunge Philip Marmo akitia saini kitabu cha maombolezo ya msiba wa Mzee Rashidi Mfaume Kawawa mara baada ya kuwasili nyumbani kwake eneo la Madale nje kidogo ya jiji la Dar es salaam jana jioni.
Mh. Vita Kawawa Mbunge wa Namtumbo, Songea akiwa ameongozana na Waziri wa Nchi ,Sera Uratibu na Bunge Philip Marmo kuelekea kwenye eneo alilozikwa baba yake mzee Rashid Mfaume Kawawa kutoa heshima
Mh. Vita Kawawa Mbunge wa Namtumbo, Songea akiwa ameongozana na Waziri wa Nchi ,Sera Uratibu na Bunge Philip Marmo kuelekea kwenye eneo alilozikwa baba yake mzee Rashid Mfaume Kawawa kutoa heshima
Mh. Vita Kawawa Mbunge wa Namtumbo, Songea ambaye ni mtoto wa Marehemu Rashid Kawawa akimkaribisha Waziri wa Nchi ,Sera Uratibu na Bunge Philip Marmo mara baada ya kuwasili nyumbani kwa marehemu Rashidi Mfaume Kawawa Madale, jijini Dar es salaam kukabidhi michango ya rambirambi kutoka kwa marafiki mbalimbali jana jioni.
Mh. Vita Kawawa Mbunge wa Namtumbo, Songea akiwa ameongozana na Waziri wa Nchi ,Sera Uratibu na Bunge Philip Marmo kuelekea kwenye eneo alilozikwa baba yake mzee Rashid Mfaume Kawawa kutoa heshima
Waziri wa Nchi ,Sera, Uratibu na Bunge Philip Marmo akimkabidhi kwa niaba ya ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Rehema Rashid Kawawa, mtoto wa marehemu Mzee Rashid Mfaume michango mbalimbali kutoka marafiki mbalimbali wakiwemo Mawaziri, Wakuu wa Mikoa, Mashirika, Taasisi na watu Binafsi. Zaidi ya shilingi milioni 24 ikiwa ni michango ya rambirambi zilikabidhiwa kwa familia ya marehemu Rashid Mfaume kawawa jana jioni.
Picha na Aaron Msigwa wa Maelezo
Mimi nadhani kwa usalama waziri angekabidhi cheki badala ya bulungutu la minoti, ingawa kuna ulinzi mkali hapo nyumbani, haionyeshi mfano mzuri.
ReplyDeleteFAMILIA YA SIMBA WA VITA PAMOJA NA VIONGOZI WA SERIKALI MKAA PAMOJA KUJADILI JINSI YA KUMUENZI MZEE KAWAWA KWA NJIA YA KUWEKA KUMBUKUMBU KUBWA ITAKAYO ENDANA NA HESHIMA YAKE KWA TAIFA LA TANZANIA.
ReplyDeleteMWALIMU NYERERE YEYE ANA TAASISI YAKE KWA HIYO MZEE KAWAWA NAYE ANATAKIWA AWE NA KITU CHA KUMBUKUMBU KWA FAIDA YA VIZAZI VIJAVYO.
Hiyo pesa wakigawana watoto wote kila mmoja atalamba kama milioni moja na ushee hivi kila mototo, wachilia mbali mjane wa marehemu. Sio haba yaweza hata kununua mabati kuezekea nyumba. Poleni sana kina Zamaradi. Anaesema pesa ingekuwa cheki ingeandikwa jina la nani? Usicheze na mambo ya mirathi mkuu. Inaweza kutenganisha familia
ReplyDeletepole sana da Zamaradi Kawawa, frm ex jangwani alumni in USA.
ReplyDeleteMichuzi asante kwa picha hizi .Vita nimesomanae hapo Mzizima Sec.School(1978-1981).Hivi sasa ni mbunge!.Pole sana Vita kwa msiba wa Mzee Kawawa.Pia ningependa kujua kama mtu yeyote anaewajua mmoja wa hawa old schoolmates wangu Freddy Mzena,Pamela Kasambala,Gerald Elinaza,Thekla Mwombela,Merci Mhina,John Makanza,Abdul Wahid(tubby),Lilian Ngowi au Samuel Mwaijande.Wote hawa ni Mzizima class 1978-1981.Hapo juu ni jina langu la awali.
ReplyDelete