Tume ya Taifa ya Uchaguzi imesitisha kampenzi za uchaguzi Jumatatu na Jumanne ili kupisha mtihani wa Taifa wa kuhitimu darasa la saba ufanyike bila bughudha.

Taarifa ambayo imetolewa na NEC na kusainiwa na Mkurugenzi Mkuu, Mh. Rajabu Kiravu, inasema kuwa hatua hiyo ni kutaka mitihani kufanyika kwa utulivu.

“...kwa kuwa mikutano ya kampeni za uchaguzi mara kwa mara imekuwa ikifanyika karibu na maeneo ya shula za msingi, tume baada ya kushauriana na vyama vya siasa imeamua kwamba pasiwepo na kampeni za uchaguzi zozote siku ya Septemba 6 na 7 mwaka huu,” alisema.

Alisema kuwa ili kupisha mitihani hiyo, NEC imeagiza wasimamizi wa uchaguzi kuhakikisha hakuna kampeni zinazoendelea kwa siku hizo mbili.
Kampeni zitaendelea tena rasmi tarehe 8 Septemba hadi 30 Oktoba 2010, imesema taarifa hiyo ya NEC.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...