Ankal Michuzi Salamaleko,
Nimerejea tena, safari hii nna swali ambalo naomba msaada tutani ili wadau wa Globu yetu ya Jamii wanisaidie.
Ni hivi ankal, kila mara nabishana na dereva wetu aitwaye Saidi kuhusu huu mtindo wake na madereva kibao wa hapa Dar wanapofika sheli kutia mafuta garini. Yaani huwa wananishangaza pale wanapoanza kutingisha gari wakati mafuta yanakaribia full tenki wao hukitingisha gari ili mafuta yawe yanajaa vizuri, Jee hii ni kweli ama ni magumashi?
Mdau Tandamti

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Hii inaweza kuwa na ukweli mdau mtoa maada. Na sababu kubwa ni kwamba kutokana na utalaam wangu kidogo ni kwamba matank ya mafuta ya magari huwa hayapo moja kwa moja kama unavyoona pipa. Huwa yana partition kwa ndani..yaani kama vyumba hivi japokuwa huwa vimeungana. so sababu ya kufanya hivyo ni kupunguza ile nguvu ya mafuta kuweza kutingishika wakati gari likiwa mbioni hasa katika barabara mbovu. Hii ni hatari kwani yanaweza kusababisha ku leak na pengine hata moto.

    Mdau wa Dodoma

    ReplyDelete
  2. Kama umelishuhudia hilo ukiwa Dar wala usipoteze muda wa kufikiria maana uelewa wa madereve wa bongo wanaufahamu wao wenyewe na wake zao. Kutanua wao, kuchomekea wao, matusi ndio usiseme hivyo wala usishangae kuona wanatingisha magari kwa imani ya kushindilia mafuta! Na kuna wengine huwa hawaweki mafuta kwenye tanki moja kwa moja anaenda na kidumu anapimiwa kisha anamimina kwenye gari. Hao ndio madereva wetu bana

    ReplyDelete
  3. Hakuna mantiki yoyote ktk swala hilo.

    ReplyDelete
  4. hiyo ni kweli kabisa kwani hata mimi mwenyewe ni mmiliki wa mabasi ya daladala hapo jijini dar na kila ikifika wakati wa kumaliza kazi huwa tunapitia kujaza mafuta kwajili ya kesho na huwa tunatingisha ili mafuta yaingie mengi kutokana mafuta yanakuwa na gesi na yanafanya kama mapovu haraka kupanda mpaka juu ya mlango wa tank sasa unatingisha povu linashuka na kuendelea kujaa wese

    mdau mahakama kuu ya dunia.

    ReplyDelete
  5. Inaitwa bleeding yaani kutoa upepo, unaweza pia kuweka jiwe na kulipanda na tairi la nyuma upande wa tenki na upepo utatoka wenyewe bila ya kutikisa

    ReplyDelete
  6. hiyo inaweza saidia kama deveva wenu anaweka lita tano au chini ya hapo ktk tanki kwani anataka mafuta yaende ktk partion inayotakiwa.Ila kama anaweka zaidi ya lita 10 au kujaza tanki kabisa hiyo tingisha tingisha haina maana yeyote.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...