Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dr. Salim Ahmed Salim, akipiga kura leo jijini Dar es salaam ya kumchagua Rais , Mbunge na Diwani. Dkt Salim aliwasili katika Eneo la Soko la Samaki Msasani saa 12.50 Asubuhi na kufanikiwa kupiga kura katika Kituo B 3 cha Soko la Samaki Msasani saa 1.30 Asubuhi.
Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dr. Salim Ahmed Salim akisubiri Kitambulisho chake kutoka kwa Karani wakati Karani huyo akiendelea na uhakiki ili kudhibitisha kama kweli jina lake limo katika daftari la wapiga kura ili aweze kwenda kupata katarasi za majina ya wagombea ili kushiriki zoezi la upigaji kura za kumchagua Rais, Mbunge na Diwani.
Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr. Salim Ahmed Salim, (wa pili kutoka mwisho) akiwa katika mstari unaolekea katika Chumba cha upigaji kura leo jijini Dar es salaam kwa ajili ya kushiriki zoezi la kumchagua Rais, Mbunge na Diwani.Picha na Tiganya Vincent- MAELEZO.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Balozi ana udugu na mcheza mpira wa kikapu Vince Carter? Wana ufanano fulani hivi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...