Marehemu Askofu Stephen Mwakasuka
Leo, tarehe 15/11/2010 imetimu miaka miwili tangu tulipoondokewa na mpendwa wetu Askofu Stephen Mwakasyuka.
Ni kweli kifo hakizoeleki, kwani sisi Watoto, Ndugu, Marafiki na Wapendwa wote tumejitahidi kuzoea hali ya kutokuwa na mtu muhimu huyu bila mafanikio.
Sisi, akina Phoebe, Florence, Jossey, Tungibwaga, Mponjoli, Atuganile, Frida, Salome, Gwakisa, Christian na Lazaro pamoja na wapendwa wote tunazidi kuliwazwa na imani kwamba ipo siku tutakuwa pamoja baada ya taabu zote za dunia kwisha.
“Nikasikia sauti ikitoka mbinguni ikisema, Andika, Heri wafu wafaao katika Bwana tangu sasa. Naam asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao” - Ufunuo 14: 13

Poleni sana akina Atuganile na ndugu zako kwa kumpoteza baba. Namkumbuka Askofu Mwakasyuka alipokuwa pale Rungwe Mission na baadaye akahamia Lutengano. Kyala abhape amaka bho tukukumbuka ukufwa kwake "Mungu awape nguvu na faraja tunapokumbuka kifo chake" Ameni.
ReplyDeleteTulikupenda sana Babu, lakini Mungu alikupenda zaidi.
ReplyDeletePole sana mpenzi dada Frida!
ReplyDeleteJoe