Marehemu Stumay Bakari wakati wa uhai wake.
Bibi Salma Bakari Mlay[Bibi Hope]wa Mbagala anatoa shukrani zake za dhati kwa Watu wote walioshiriki katika Kumuuguza Dada Yake Mpendwa Stumay Bakari,hadi umauti ulipomfika Tarehe 9/06/2011 na Kuzikwa uko Mbagala Saku 10/06/2011.

Shukrani kwa majirani wote wa Temeke Quartes alipokuwa akiishi Marehemu pia majirani wote wa Mbagala Saku.

Shukrani za pekee ziwafikie Mama Yahya na Baba Nelly wa Temeke Quartes .Pia Shukrani za pekee ziwafikie Stara Kitwana Kondo,Subira Kitwana Kondo,Huria Kitwana Kondo pamoja na Mwenyekiti wetu Wa Serikali ya Mtaa wa mzambarauni Saku Bwana Muharami.

Sio rahisi kutoa shukrani kwa mtu mmoja mmoja bali Watu wote walioshiriki kwa namna moja au nyingine naomba wapokee shukrani zangu.

Dada yetu ametutoka wakati bado tulikuwa tunamuhitaji sana lakini yote ni kazi ya Mungu
haina makosa.

INNA LILLAHI WA INNA ILAIHI RAJIOON.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...