Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika
Mh. Christopher Chiza
NA MAGRETH KINABO - MAELEZO,DODOMA

SERIKALI imelipa madeni ya vyama vya ushirika 38, ambapo kiasi cha sh. bilioni 15.01 hadi kufikia Desemba mwaka 2010.

Hayo yamesemwa leo Bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Christopher Chiza wakati akijibu swali la mbunge wa Jimbo la Shinyanga mjini(CCM) lililouliza kuwa katika kufufua vyam vya ushirika serikali iliamua kulipa madeni yote ya vyama vya ushirika nchini ikiwemo SHIRECU.

Je ni lini serikali itakamilisha ulipaji wa mapunjo ya mishahara kwa mamia ya wafanyakazi wa SHIRECU mkoani Shinyanga waliopunguzwa kazi au kustaafu kisheria.

Akijibu swali hilo Naibu Waziri huyo alisema miongoni mwa madeni yaliyopo ni deni la watumishi wa SHIRECU waliopunguzwa kazi au kustaafishwa la sh. bilioni 3.27 ambapo kati hizo serikali imeshalipa sh. milioni 654.2 sawa na asilimia 20.

Hivyo serikali itaendelea kutenga bajeti zake za kila mwaka hadi deni litakapokwisha.

Waziri Chiza alisema seriklai inalipa madeni hayo ili kuvifufua kwa sababu ndiyo njia rahisi ya kuwafikishia wananchi wengi misaada na huduma kuliko kumhudumia mtu mmojamoja.

Pia vyama hivyo havitaruhusiwa kuilimbikiza madeni tena na wizara yake itafanya ukaguzi, mara kwa mara ili kudhibiti wizi, ubadhilifu wa fedha na mali unaofanywa hususan wakati wa msimu wa ununuzi wa mazao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 21, 2011

    Kama wanalipiwa madeni mbona huku mikoani na wilayani tunashuhdia mali (majengo, karakana, ofisi, viwanda)za hivi vyama vya ushirika vikuuzwa kinyemela na kiholela bila wanachama kuridhia. Office barers wachache waliosalia wanajiamulia tu na hakuna mikutano ya wanachama na hatujui hizo pesa za kuuza hizo mali zinakwenda wapi. Kyela, Rungwe na kwingine nchini tumeayaona hayo. Serikali inafanya nini na ufisadi huu?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...