Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja na Naibu wake Ili Malima wakipongweza baada ya kupitishwa Makadirio ya Bajeti ya Wizara yao 2011-2012 leo Dodoma.(PICHA ZOTE NA MWANAKOMBO JUMAA) 


Mbunge wa Same mashariki Anne Kilango Malecela akichangia Bungeni leo'
Mbunge wa Bumbuli na Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Nishati na Madini Mh. January Makamba akichangia hoja leo
Msemaji wa kambi  ya Upinzani Bungeni Freeman Mbowe (miwani) akibadilishana mawazo na mbunge wa Ubungo (CHADEMA) John Mnyika wakati wa majadiliano ya kupitisha hoja ya Makadirio na Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini kwa mwaka wa fedha 2011-2012 Dododma leo

Waziri wa Nishati naMadini William Ngeleja akiingia Bungeni leo


Waziri wa Nishati naMadini William Ngeleja akiwakilisha Makadirio ya matumizi na Mapato ya wizara yake leo Bungeni(Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO)


Na Ripota wa Globu ya Jamii, Dodoma
Bunge limepitisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini iliyowasilishwa upya leo mjini Dodoma na Waziri wa wizara hiyo Mh. William Ngeleja.

Katika maelezo yake, Mh. Ngeleja amebainisha kwamba serikali imepania kutokomeza kabisa tatizo la umeme nchini haraka iwezekanavyo, na kulitafutia jibu la kudumu tatizo hilo sugu.


Mh. Ngeleja kaliambia Bunge kwamba kampuni ya Symbion Power ya Marekani na Shirika la Hifadhi ya Jamii nchini (NSSF) wamepewa zabuni ya kuingiza nchini mitambo ya kuzalisha umeme wa dharura, katika mpango huo wa serikali.

Symbion Power ni kampuni ambayo ilinunua mitambo iliyokuwa ikimilikiwa na kampuni ya Dowans Tanzania, imepewa zabuni ya kuzalisha megawati 205 za umeme, wakati NSSF wataingiza mitambo yenye uwezo wa kuzalisha megawati 150. 


Kwa mujibu wa taarifa ya Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, iliyowasilishwa na kujadiliwa mbele ya Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini ambayo Mwananchi limeiona, mpango wa dharura kati ya Agosti 2011 na Desemba 2012 itaigharimu Serikali Sh1.24 trilioni. 


Kasema miradi inayotarajiwa kutekelezwa ni ya dharura itakayozalisha megawati 1,032 zikiwemo 572 kati ya sasa na mwezi Desemba mwaka huu na megawati 460 zaidi ifikapo Desemba 2012. 


“Ili kukabiliana na mgawo wa umeme kwa kipindi cha dharura, Serikali kwa kushirikiana na sekta binafsi, pamoja na taasisi za umma itatumia uwezo wa mitambo iliyopo nchini kukodisha na kununua mitambo ya kufua umeme itakayotosheleza mahitaji ya sasa na baadaye,” amesema Ngeleja, ambaye pia aliomba radhi kwa usumbufu uliopatikana wakati wa kuwasilisha bajeti hiyo mara ya kwanza wiki tatu zilizopita. 

Pamoja na kuung mkono hoja ya Waziri Ngeleja, Wabunge wameitaka serikali kuhakikisha kwamba kila lililoahidiwa linatekelezwa na kwamba hii hali ya dharura isiwepo tena katika sekta hiyo.

Katika kukamilisha Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda amekubaliana na rai hizo za Wabunge na kusisitiza kwamba ahadi hizo zitatekelezeka endapo kama mapato yatakusanywa ipaswavyo na kuelezea matumani yake kwamba TRA itafanya kazi zake kwa umahiri ili kutimiza malengo ya kupata fedha za kutimiza ahadi hizo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. MH! itakuwaje TRA wasipofikisha malengo yaliyowekwa? TRA watatoa wapi hizo pesa wakati uchumi unakufa kutokana na matatizo ya umeme na mafuta? Time will tell.

    ReplyDelete
  2. There is a lot of potential in Wind Energy in Tanzania. A company called Wind East Africa in Singida is doing just that. This was even discussed in Bunge today: http://pushobserver.mediacore.tv/media/deputy-minister-of-minerals-presenting-on-wind-ene

    ReplyDelete
  3. Solution to the problem of electricity in Tanzania is not what is being done year in year out, i.e. renting generating equipment, now meeting target of tax collection by TRA!!!, etc. Electricity problem is a 'dirty money' generators benefiting some 'vigogos'. For years we have had this problem, the solution has been the same but the problem is not being solved. Grow up people, the solution is clear but they are not doing it because they don't want to solve the problem. They earn lots of money, and they have power everywhere they go and live; why should they bother? only a normal Tz like you and I with our survival businesses are crying out day and night. They tell us the problem is water level or lack of rain, now if you pile up equipment that consume same energy that is lacking do you think you can generate enough electricity? Why don't they go for greener energy production through solar, wind, tidal wave, etc? To solve electricity problem, leadership - the beneficiary of the problem must change.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...