Warembo wanaoshiriki shindano la kumsaka Vodacom Miss Tanzania 2011, wakiwa katika bwawa la Viboko lililopo katika Hifadhi ya Wanyama pori Mikumi mkoani Morogoro jana wakati warembo hao walipotembelea hifadhi hiyo kujionea wanyama aina mbalimbali ikiwa ni sehemu ya ziara yao ya kutembelea vivutio vya utalii nchini kuhamasisha utalii wa ndani.

Na mwandishi Wetu

Warembo 30 wa Vodacom Miss Tanzania ambao walianza rasmi kambi yao Agosti 8 mwaka huu wapo katika ziara ya mafunzo kuhusiana na vivutio mbalimbali vya kitalii vilivyopo nchini na kwa kuanzia wametembelea Hifadhi ya Taifa ya Mikumi iliyopo mkoani Morogoro.

Wakiwa mkoani humo warembo hao walioongozana Maafisa wa Vodacom Tanzania na waandaaji wa shindano hilo watajifunza juu la rasilimali zilizopo nchini ili kuweza kuzitangaza watakapopata nafasi ya kuliwakilisha taifa.

Meneja Uhusiano na Habari kwa njia ya mtandao wa kampuni hiyo Matina Nkurlu amesema wameamua kuwaandalia warembo hao ziara hiyo ili iwasaidie katika kukuza kiwango cha ufahamu walichonacho sasa.

“Vodacom kama wadhamini wakuu wa shindano hili tunafurahi kuona warembo hawa wamejifunza kupitia waliyayaona hapa Mikumi na matumaini yetu watautangaza utalii wa ndani vilivyo watakapopata fursa ya kwenda kushiriki ‘Miss World’,” alisema Nkurlu.

Akizungumza mara baada kukamilika kwa ziara kwenye hifadhi ya taifa ya Mikumi mshiriki Sarha Israel alisema kutokana na waliyojifunza wamepata ufahamu mkubwa juu ya vivutio vya kitalii vilivyopo mkoani Morogoro na kwamba sasa wataweza kuutangaza kiundani popote watakapokwenda.

“Awali nilikuwa naisikia tu hifadhi ya taifa ya Mikumi kupitia kwa wenzangu lakini sasa ni elimu ya kutosha juu ya wanyama na vitu tofauti vinavyopatikana hapa na natarajia nitajifunza zaidi katika Mikoa ya Kilimanjaro na Arusha ambapo ziara yetu itaendelea,” alisema Sarha.

Kwa upande wake Albert Makoye ambaye ni Mkuu wa Itifaki na nidhamu wa Vodacom Miss Tanzania alisema ni matarajio yake ziara hiyo itakayojumuisha mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Morogoro itakuwa yenye mafanikio na kwamba warembo wataweza kujifunza mengi.

Aidha alieleza wakiwa huko watatembelea Manyara, mapango ya mlima Kilimanjaro, Kreta ya Ngorongoro na maeneo mengine yenye vivutio vya kitalii ikiwemo maboma ya Maasai yanayotumika kutangaza utamaduni wa kabila la wamaasai huku yakitangaza utalii wa ndani ambao huiwezesha serikali kujiingizia fedha nyingi za kigeni kutoka kwa watalii wanaotembelea hifadhi hiyo.

Mwaka huu warembo hao wameingia kambini kwa mfumo tofauti na uliozoweleka kwani wamewekwa kwenye jumba maalum la ‘Vodacom House’ ambapo matukio yao yatakuwa yakioneshwa kupitia Star na Clouds TV na watazamaji watapata fursa ya kupiga kura kuchagua mrembo watakayemuona anafaa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...