TIMU YA MPIRA WA KIKAPU YA MAVETERANI WA DAR ES SALAAM (OLDGUARDS VETERANS BASKETBALL CLUB) YENYE MAKAO YAKE MAKUU PALE GYMKHANA , OCEAN ROAD WANAONDOKA KESHO TAREHE 29 OCTOBA 2011 KWENDA ZANZIBAR KUCHEZA MECHI ZA KIRAFIKI PAMOJA NA TIMU ZA MAVETERANI WA ZANZIBAR NA ARUSHA 
 
PAMOJA NA KUDUMISHA UDUGU WA KIMICHEZO BAINA YA WACHEZAJI WA ZAMANI, TIMU HIYO ITATUMIA FURSA HIYO KUTOA POLE KWA NDUGU NA JAMAA WALIOPATWA NA MSIBA WA KUZAMA KWA MELI YA MV SPICE ISLANDER HIVI KARIBUNI
 
OLDGUARDS WANATOA SHUKURANI ZA PEKEE KWA KAMPUNI YA AZAM MARINE KWA KUTOA USAFIRI WA KWENDA ZANZIBAR
 
TIMU YA OLDGUARDS AMBAYO ITAJUMUISHA TIMU YA WANAUME NA WANAWAKE WANATARAJIWA KUREJEA MJINI DAR ES SALAAM , JUMAPILI TAREHE 30 OCTOBA 2011
 
 
LAWRENCE CHEYO
MWENYEKITI WA BARAZA LA WADHAMINI - 
OLDGUARDS BASKETBALL CLUB

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...