Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) unafuraha kuwatangazia  kuwa huduma za safari za abiria zitaanza tena hapo Jumanne Januari 24, 2012 saa Moja usiku kutokea Stesheni ya Dodoma  kwenda Kigoma.  Kutoka Dodoma kwenda Kigoma  kutakuwa na safari mbili yaani siku za Jumanne na Jumamosi na kutoka Kigoma kuja Dodoma ni siku za  Jumatatu na Alhamis..

Tiketi kwa wasafiri wa Dar es Salaam zitaanza kuuzwa kesho Jumapili Januari 22, 2012asubuhi Wasafiri katika stesheni nyingine za reli ya kati wawasiliane na Mastesheni Masta husika kwa ajili ya kupata tiketi za safari. 

Uamuzi wa kuanzia safari Dodoma umechukuliwa kimkakati kutokana na eneo korofi kati ya  Kilosa, Kidete, Godeghode na Gulwe kuwa halitabiriki ikizingatiwa msimu wa mvua za masika utaanza muda sio mrefu ujao.

Aidha wasafiri watakaokuwa wamekata tiketi za safari husika wanahimizwa kuwasili mjini Dodoma mapema kabla ya saa moja usiku ili kuwahi safari bila ya kuchelewa.

Mafundi wa TRL wakishirikiana na wale wa RAHCO walikamilisha kazi ya ukarabati wa sehemu korofi za Godegode mkoani Dodoma  jana Januari 20, 2012 na kuwezesha treni ya abiria kuvuka eneo hilo na kuwa tayari kutoa huduma itakayoanza Jummane ijayo.

Halikadhalika Uongozi wa TRL unashukuru kwa uvumiivu ulionyeshwa na wasafiri na wananchi kwa ujumla wakati huu mgumu wa usafiri wa reli ya kati na kwamba unaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza wakati wa kuanzisha huduma hiyo Dodoma ambayo ni uamuzi wa muda tu hadi hali itakapotengemaa ya maeneo korofi.

Imetolewa na Ofisi ya Uhusiano TRL

kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji  Mhandisi K.A.M Kisamfu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. SOMETIMES HUWEZI KUAMINI KAMA TANZANIA KUNA HUDUMA ZA TRAIN

    ReplyDelete
  2. Matatizo ya TRL ni sababu serikali iliwakabidhi wawekezaji uchwara.

    ReplyDelete
  3. WAWEKEZAJI WA KIHINDI WARUDI KWAO WAMEKUJA KULA TU . HAKUNA LOLOTE LA MAENDELEO ILA KURUDI NYUMA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...