Ndugu John Hans Badi - Mmiliki na Mhariri Mkuu wa Daily Mitikasi Blog, anachukua fursa  hii kutoa shukrani za dhati kwa watu wote walioshiriki, kwa namna moja au nyingine katika kumuuguza hadi maziko ya mpendwa Mama yake Mzazi, Esther Nyimbo Badi  aliyefariki dunia siku ya Jumatano Feb. 22, 2012 Majira ya Saa 12:30 jioni katika  Hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam na baadaye kuzikwa Kijijini Ilembula (W) Njombe, Iringa.

Shukrani za pekee ziwaendee Madaktari wa Hospitali ya Taifa Muhimbili na Aga Khan ambao walikuwa wakipigania ili kuokoa maisha ya mpendwa marehemu Mama yetu bila kuchoka hadi dakika ya mwisho neno la Mungu lilipotimia.

Shukrani pia ziwaendee Familia yote ya Marehemu Dr. Luhangano Joseph Badi ikiongozwa na Dada yetu Mkubwa Mama Blandina Nyoni, shemeji zetu kwa jitihada walizozifanya za kujaribu kuokoa maisha ya Mama yetu.

Pia nawashukuru  Wanahabari, Bloggers na wadau wote ambao kwa namna moja ama nyingine walijumuika nami katika kunifariji na kunitia moyo katika kipindi hiki kigumu, ama kwa njia ya simu, E-mails, ana kwa ana. 

Si rahisi kumtaja mtu mmoja mmoja ila shukrani pia ziwaendee Mama Mdogo Eliza, Binamu zetu pamoja  ndugu jamaa na marafiki.

Sina cha kuwalipa zaidi ya kuwaombea kwa Mungu abariki kila jambo mnalolifanya hapa duniani na hakika mmejiwekea thawabu nyingi kwake. Kwa kuwa kila nafsi itaonja mauti, basi hatuna budi kumshukuru Mungu kwa kutimiza ahadi yake na tuseme: Yeye (Mama Esther Nyimbo Badi) ni wa Mwenyezimungu na kwake Mungu sote tutarejea!

Mungu ampumzishe Mama Esther Nyimbo Badi Mahala Pema Peponi – Amen!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Poleni sana Badi.Bwana ametoa na ametwaa.Bwana akupe atawaongoza katika kipindi hiki kigumu.Kuweni na imani mtafika.Amen

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...