Waziri wa nchi katika ofisi ya Rais asiye na Wizara maalum Profesa Mark Mwandosya akila kiapo mbele ya Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.Wapili kushoto ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue.Na watatu kulia ni Karani wa Baraza la Mawaziri Bwana Gerson Mdemu.
Profesa Mwandosya akipokea miongozo ya kazi baada ya kula kiapo ikulu leo asubuhi.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza na kumtakia mafanikio Profesa Mwandosya muda mfupi baada ya kumuapisha ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimsaidiaWaziri wa nchi katika ofisi ya Rais asiye na Wizara maalumu Profesa Mark Mwandosya kushuka katika ngazi za ikulu baada ya kumuapisha leo asubuhi.
Waziri Profesa Mark Mwandosya akiwa katika mazungumzo na Rais Dkt.Jakaya Kikwete muda mfupi baada ya kula kiapo ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi(picha na Freddy Maro)
hatimae kakubali hongera JK...napita tu siandiki zaidi.
ReplyDeleteMr.Prez please muache huyu mzee ajiuguze taratibu.hebu muondolee hayo majukumu yasiyo na wizara!!
ReplyDeleteI see Mark Mwandosya as our Next President. Don't ask me where did i get this:) Just my opinion.
ReplyDeleteHuyo anayesaidiwa kushuka pilika za ofisi ataziweza? Vijana wakiichukia CCM wanachama wanashangaa, watawapendeje wakati mnakumbatia wazee namna hii?
ReplyDeleteNimetokwa na machozi ......
ReplyDeleteHongera sana prof naona sasa umepona
ReplyDeleteunastahili sifa mh rais utu wako umepitiliza kiwango mpende adui yako kama nafsi yako mungu akubariki mfano wa kuigwa
ReplyDeleteHivi huyu mwenye cheo cha "public" anaumwa kitu gani?
ReplyDeleteVazi la Taifa!
ReplyDeleteWanaume, vaeni ki-Mwandosya!
Halafu tukazanie la akina mama.
oooh Pole sana Mwandosya na mama Lucy tunakuombea utapona.sijaamini kushuka ngazi unasaidiwa!ila ni hatua kama umeweza kufika na kuapishwa maana yake kuna improvement.mungu akulinde
ReplyDeleteMgonjwa atawezaje kufanya kazi jamani? Badilikeni!!!!!!
ReplyDeletekwanini isipite sheria ya kuongezewa muda wa uraisi tanzania huyu mh.kikwete hakuna wa kumfikia ana uwezo mkubwa wa kuongoza nchi yetu
ReplyDeletewatanzania tukumbuke kuwa leo tutamuona hafai lakini tutakuja kumkumbuka sana mh.kikwete hakuna kama yeye kwa kila idara.
Jamani Mhe. Raisi wetu JAKAYA MRISHO KIKWETE tutamkumbuka kwa mengi sana atakapomaliza muda wake.
ReplyDeleteNi wazi kwa sasa Serikali inafikika kuliko ilivyokuwa kabla.
Ametumia ubinaadamu sana kumwacha Prof. Mwandosya Ofisini na kuwa hiyo Wizara isiyo kuwa na kazi Maalum ni kama amepewa mapumziko tu Mwandosya ili aweze kupata huduma za Mamlaka kuliko angetolewa ingesababisha ajione mpweke, engesononeka na ingeongeza kasi zaidi ya kuumwa kwake !