Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi,Ramadhani Khijjah (kulia) akimsikiliza kwa makini ofisa Mkuu wa (CMSA) Mrs Nassama Masinda wakati alipokua akichangia mada wakati wa Kongamano la siku moja la kujadili masuala ya Mitaji na Uwekezaji lililoandaliwa na NIC Capital kwa kushirikiana na DSE, IFC jijini Dar es Salaam hapo jana.
Meneja Masoko na Mawasiliano wa NIC Capital Bw.Yusuf Shenyagwa, akitoa mada katika kongamano la siku moja lililojadili masuala ya mitaji na uwekezaji,kongamano hilo liliandaliwa na NIC Capital kwa kushirikiana na IFC pamoja na Soko la hisa la Dar es Salaam (DSE)hapo jana.
Mmoja wa washiriki wa kongamano la siku moja la kujadili masuala ya mitaji na uwekezaji akichangia mada. Kongamano hilo lililofanyika jijini Dar es Salaam jana liliandaliwa na NIC Capital kwa kushirikiana na IFC pamoja na Soko la hisa la Dar es Salaam (DSE).
Baadhi ya washiriki wa kongamano la siku moja la kujadili masuala ya mitaji na uwekezaji wakifuatilia kwa makini mada iliyokuwa ikitolewa. Kongamano hilo lililofanyika jijini Dar es Salaam jana liliandaliwa na NIC Capital kwa kushirikiana na IFC pamoja na Soko la hisa la Dar wes Salaam (DSE).
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi Ramadhani Khijjah watatu toka kushoto waliokaa akiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kufungua kongamano la siku moja la kujadili masuala ya Mitaji na Uwekezaji lililoandaliwa na NIC Capital kwa kushirikiana na DSE, IFC jijini Dar es Salaam hapo jana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Wananchi wengi Tanzania bado hawajawa na uwelewa wa soko la mitaji.Tatizo ni viongozi wa siasa bado hakuna miundo mbinu mizuri ya kusapoti soko la mitaji na pia watu walio kwenye soko la mitaji hawana mipango endelevu wapo tu kwasababu wanalipwa mishahara. Kwa mfano sisi tulio huku UK tukizungumza mnasema kuwa tunasema sana, matokeo yake limekuwa kama anasa la watu wachache jaribuni kubadilika uchumi haendi hivyo soko si la watu wenye kipato cha juu tu na muongeze zaidi financial product sio share za kawaida na categories tofauti tofauti za kampuni zilizo sajiliwa.
    Mdau Mpenda maendeleo UK

    ReplyDelete
  2. Mdau wa UK mpenda maendeleo Anonymous wa kwanza hapo juu Fri Sep 07, 08:09:00 PM 2012

    Umesema ukweli mtupu,

    Hayo yamenikuta mimi mwenyewe mkazi wa Dar ambaye ninao ufahamu kiasi kuhusu masuala haya, ilitokea siku moja nilifika pale jengo la PSPF Mtaa wa Ohio ghorofa ya 14 ilipo DSE.

    Cha kushangaza nilikuwa Mfanyakazi wa Mapokezi ana mgeni mmoja pembeni, ile kuingia tu alinitazama juu hadi chini kana kwamba natokea Sayari nyingine hapo sijaulizia kupata access kufika ktk Trading Floor, nilipoona hivyo nilisita nikajua hili Soko linamilikiwa na kundi la wachache wanaofahamika ndio maana nilitazamwa sana.

    Baada ya kuona hivyo ilibidi nighairi nikauliza mambo mengine lakini nikasema ninataka kujua uwezekano wa kufika Trading Floor Mhudumu akasema haiwezekani!

    Enheee, hata Huko Wodi ya Wagonjwa Mahututi Muhimbili kunafikika kuliko Trading Floor ya DSE kitu ambacho kama utaenda Masoko ya Hisa ya nchi jirani Kigali(RSE),Uganda(USE) na Nairobi(NSE) hiyo siyo issue Soko la Hisa lipo wazi kwa yeyote yule (hata Raia wa nje ya nchi hizo) na unapokelewa kama Mwekezaji kamili hata kama umeenda kuulizia tu!

    Hivi kwa mtaji huu ali achilia mbali nchi za mbali, tutauweza Ushindani ktk Masoko ya Hisa Afrika ya Mashariki?

    ReplyDelete
  3. ndo tanzania yetu hii mtu najali kukikuza kna kujiliwaza na kitambi take na familia yake na siyo manufaa ya nchi na wananchi wake,ukiwa mjanja mjanja na mwizi ndo unastahili mapato ya wavujajasho katika nchi hii wajanja ndo wanaotawala, mlala hoi unatakiwa ulale

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...