Waziri Mkuu Mh. Mizengo Peter akipata maelekezo
ya namna ya kupiga kura yake kutoka kwa Meneja wa Tawi la Bodi ya Utalii
Tanzania(TTB) Arusha Bw. Wily Lyimo muda mfupi kabla ya kupiga kura
yake katika kituo cha Mikutano cha AICC mjini Arusha hivi karibuni.
Na Geofrey Tengeneza
Waziri Mkuu Mheshimiwa Mizengo Pinda hivi karibuni amepiga kura
yake ya kuvichagua vivutio vitatu vya Tanzana katika shindano linaloendelea
hivi sasa la kutafuta maajabu Saba ya asili ya Afrika.
Waziri Mkuu alipiga kura yake wakati wa mkutano wa tano wa wadau wa
Mfuko wa Pensheni wa LAPF uliofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa
mikutano wa AICC mjini Arusha ambapo Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) iliweka
kituo cha kupigia kura kwa njia ya mtandao wa komputa (internet).
Waziri
Mkuu alivipigia kura vivutio hivyo vitatu ambavyo ni Mlima Kilimanjaro, Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na Kreta ya Ngorongoro
ili viweze kuwa miongoni mwa maajabu Saba ya Asili barani Afrika.
Viongozi
wengine waliopiga kura zao wakati wa mkutano huo katika kituo hicho
cha Bodi ya utalii Tanzania ni pamoja na Waziri wa Kazi na Ajira
Mh.Gaudensia Kabaka, Naibu Waziri wa TAMISEMI Mh.Henry Mwanri na viongozi
mbalimbali wa LAPF.
Bodi ya Utalii Tanzania hivi sasa inaendesha kampeni kamambe ya kuwahamasisha
watanzania kuvipigia kura vivutio hivyo, na katika mkutano huo iliamua
kupiga kambi katika kituo hicho cha mikutano ya Kimataifa cha AICC kwa
lengo la kuwahamashishawajumbe wa mkutano huo na kuhakikisha wale ambao
hawajapiga kura wanapiga kura zao katika kituo hicho hapo AICC zoezi
ambalo lilifanikiwa kwa kiasi kikubwa.
Tanzania ni nchi pekee barani Afrika iliyoingiza vivutio vingi katika
shindano hilo ambapo imefanikiwa kuiongiza vivutio vitatu.
Mkitaka watu wengi wapige, kila atakayepiga apewe zawadi ndogo tu. Maana kama kivutio kimojawapo kikifanikiwa kuingia ktk orodha ya maajabu saba, pesa itarudi kupitia watalii.
ReplyDelete