KAMANDA WA WA MKOA WA MWANZA SACP LIBERTUS BARLOW (pichani) AMEUWAWA KWA KUPIGWA RISASI NA WATU WANAOHISIWA KUWA NI MAJAMBAZI KATIKA ENEO LA KITANGILI JIJINI HUMO USIKU WA KUAMKIA LEO.
HABARI ZINASEMA MAREHEMU ALIUWAWA MAJIRA YA SAA TISA USIKU AKIWA NJIANI KUELKEA NYUMBANI KWAKE AKITOKEA KUMRUDISHA DADA YAKE BAADA YA KUHUDHURIA KIKAO CHA HARUSI.
MKUU WA POLISI IGP SAIDI MWEMA AMETHIBITISHA TUKIO HILO NA TAYARI MKUU WA UPELELEZI WA MAKOSA YA JINAI WA JESHI HILO (DCI) ROBERT MANUMBA AKIWA NA KIKOSI CHA MAKACHERO WAMEELEKEA MWANZA KUONGEZA NGUVU KATIKA UPELELEZI MKALI AMBAO UMESHAANZA.
MKUU WA POLISI IGP SAIDI MWEMA AMETHIBITISHA TUKIO HILO NA TAYARI MKUU WA UPELELEZI WA MAKOSA YA JINAI WA JESHI HILO (DCI) ROBERT MANUMBA AKIWA NA KIKOSI CHA MAKACHERO WAMEELEKEA MWANZA KUONGEZA NGUVU KATIKA UPELELEZI MKALI AMBAO UMESHAANZA.
HABARI ZAIDI ZINAKUSANYWA NA TUTAKULETEA KWA KINA BAADA YA MUDA SI MREFU.
poleni sana familia ya kamanda,hawa makamanda wawekewe ulinzi saa zote kazi yao ni risk sana wana maadui wengi!
ReplyDeleteKama jukumu lao linazalisha maadui wengi kwa nini wasiwe na Ulinzi wa Vijana wa kazi wanapokuwa ktk misafara yao binafsi?
ReplyDeleteHii itasaidia kama isipofanyika wimbi hili litakuwa kila kukicha!
Poleni wafiwa.Hao makamanda wanatakiwa kuwa wabunifu kwanini neighbour hood watch (sungu sungu)isirudi? Au mpaka mkuu wa nchi aseme?
ReplyDeleteHii ni hatari sana. Watu wana "guts" za kumua RPC tena wa jiji kubwa kama la Mwanza? Tunakoelekea sio kuzuri. Polisi waache kuchekeana na wezi/wala-rushwa/majambazi... Msako mkali kwenda mbele 24hrs/day; 365days/year....
ReplyDeletePole sana kwa familia. Sielwei Tanzania inaelekea wapi, yaani kila iitwapo leo ni afadhali ya jana. Mara makanisa yanavunjwa, mara mwandish wa habari ameuawa, mara hiki mara kile, ni nini kinachoendelea? Ni watu wamekata tamaa ya maisha au? Wakati wa baba wa Taifa Mwl Nyerere tunaambiwa maisha yalikuwa magumu zaidi ya na sidhani hali ya matukio haya mabaya ilikuwa kama ilivyo sasa. Nafaikiri kuna tatizo mahali, inabidi tujiangalie upya.
ReplyDelete