Mtaalamu wa Elimu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto –UNICEF Zubeida Tumbo-Masabo akitoa ufafanuzi kuhusiana na umuhimu wa kuwa na sera madhubuti za elimu zitakazopelekea kuboresha kiwango cha elimu kuanzia ngazi za chini hadi za juu.

Na Mwandishi wetu
Serikali ya Tanzania imeshauriwa kuwa na sera ya mpya ya elimu kwa kuwa sera iliyopo imepitwa na wakati na inasababisha mikanganyiko.
Mtaalamu wa Elimu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto –UNICEF Zubeida Tumbo-Masabo amesema upo umuhimu wa kuharakisha kutoa sera mpya ya elimu kwa sababu ndio itakayorahisisha utekelezaji badala ya kutokuwepo na sera inayoeleweka.
Aidha amesema sera zilizopo sasa zimepitwa na wakati, hivyo sera zitakazobuniwa upya zinapaswa kuwa na malengo ya kuendeleza elimu kwa watoto haswa motto wa kike.
Bi. Zubeida Tumbo-Masabo amesema vitendo vinavyofanyika sasa vya kumfukuza shule mtoto wa kike kwa mfano aliyebakwa na kupata ujauzito ni kumtia kitanzi cha maisha.
Ametumia fursa hiyo kuelezea kuwa katika sekta ya Elimu Umoja wa Mataifa unafanya shughuli za kuboresha elimu kitaifa, lakini pia inafanya kazi katika ngazi ya wilaya maalum katika kuangalia yale mambo ambayo wanayatilia mkazo na kuyachangia iwapo yamefanikiwa.
Katika wilaya hizo Umoja wa Mataifa unafanya vitu mbali mbali ambapo kama UNICEF imejikita katika kuangalia Masuala ya Upangaji Mipango, kwa kuwa mara nyingi shule nyingi hazina mipango.
Bi. Zubeida Tumbo-Masabo amefafanua kuwa shule zinapokuwa na mipango thabiti zinaweza hata kuuza mipango hiyo kwa mashirika mengine na kujipatia fedha za kuendesha shughuli zao nyingine za hapo shuleni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Nina unga mkono na bi Zubeida Tumbo-Masabo wa UNICF. Shule za leo zina hitaji sera mpya ya elimu hasa kwa watoto wa kike. Sera mpya ya elimu ifundishe watoto mambo ya Utumwa, vipi evil inavyo tumiwa,utapele,haki zao, na vipi mali zina pora kwenye nchi yao.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...