Afisa Elimu Wilaya ya Mtwara Mwl.Mohamed Kahumbi,akionesha aina ya simu iliyowekewa fedha katika akaunti ya M-pesa zinazotolewa bila malipo kwa kwa akina mama wanaonyonyesha kuwawezesha kupokea fedha za kunulnuia chakula chenye lishe kupitia mradi wa Lishe bora na salama wa shirika la mpango wa chakula duniani – WFP. Mradi huo umezinduliwa juzi katika kijiji cha Nanguruwe, Mkoani Mtwara.
Mmoja wa wanufaika wa mradi wa kuwawezesha wanawake wanaonyonyesha na wajawazito mkoani Mtwara kupata chakula chenye lishe akiijaribu simu aliyopatiwa ikiwa na fedha katika akaunti ya M-pesa atakazozitumia kununulia chakula chenye lishe. Fedha na simu hizo hutolewa bila malipo na Shirika la Mpango wa Chakula Duniani – WFP kupitia mradi wake wa Lishe bora na salama.
Afisa Elimu Wilaya ya Mtwara Mwl.Mohamed Kahumbi akimkabidhi simu ya mkononi mmoja wa wanufaika wa mradi wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani – WFP wa kuwapatia fedha wanawake wanaonyonyesha na wajawazito fedha za kununulia chakula chenye lishe kupitia M-pesa wakati wa uzinduzi uliofanyika juzi katika kijiji cah Nanguruwe mkoani Mtwara.
Akina mama wa kijiji cah Nanguruwe mkaoni Mtwara ambao ni wanufaika wa mradi wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani – WFP wa kuwapatia fedha wanawake wanaonyonyesha na wajawazito fedha za kununulia chakula chenye lishe wakijumuika na maofisa wa Vodacom kufurahia simu walizopatiwa zikiwa zimeunganishwa na mtandao wa Vodacom kuwawezesha kupokea fedha za mradi kwa njia ya M-pesa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...