Mkazi wa Kata ya Rhotia Wilaya ya Karatu mkoani Arusha, John Nando (73)akitoa maoni yake kuhusu Katiba Mpya mbele ya Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba wakati wa mkutano ulioitishwa na Tume hiyo jana jumatatu Novemba 19, 2012 katika Kata hiyo.
Akina Mama wa kijiji cha Slahhamo Kata ya Mbulumbulu Wilaya ya Karatu mkoani Arusha wakisoma nakala za Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba katika lugha nyepesi wakati wa mkutano wa kazi ya ukusanyaji wa maoni ya wananchi kuhusu Katiba Mpya ulioitishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba kijijini hapo jana jumatatu Novemba 19, 2012.
Mjumbe wa Sekretarieti ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Charles Masero (mwenye shati jeupe) akitoa ufafanuzi kuhusu ujazaji wa fomu za maoni kuhusu Katiba Mpya kwa wanafunzi wa Chuo cha Mafunzo ya Ufundi cha Audry Veldan kilichopo kijiji cha Shahhamo Kata ya Mbulumbulu Wilaya ya Karatu Mkoani Arusha wakati wa mkutano wa kukusanya maoni ya maoni ya wananchi kuhusu Katiba Mpya kijijini hapo jana jumatatu Novemba 19, 2012.
Mkazi wa kijiji cha Slahhamo Kata ya Mbulumbulu Wilaya ya Karatu mkoani Arusha, Thimos Mushi (51) akitoa maoni yake kuhusu Katiba Mpya wakati wa mkutano wa kukusanya maoni ulioitishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba kijiji hapo jana jumatatu Novemba 19, 2012.
Mjumbe wa Sekretarieti ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba, John Theobard akigawa nakala za machapisho mbalimbali yanayotolewa na Tume hiyo kwa wananchi wa Kata ya Rhotia Wilaya ya Karatu mkoani Arusha wakati wa mkutano wa kukusanya maoni ya wananchi kuhusu Katiba Mpya katika kata hiyo jana jumatatu Novemba 19, 2012.
Wajumbe wa Sekretarieti ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Charles Masero (kulia), Rebbeca Kajiru (katikati) na Mussa Kombo wakikusanya maoni ya wananchi kuhusu Katiba Mpya katika njia ya maandishi wakati wa mkutano uliotishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika Kata ya Rhotia, Wilaya ya Karatu mkoani Arusha jana jumatatu Novemba 19, 2012.
Wananchi wa Kata ya Rhotia Wilaya ya Karatu mkoani Arusha wakifuatilia mkutano wa kukusanya maoni kuhusu Katiba Mpya uliotishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika Kata hiyo jana jumatatu Novemba 19, 2012.PICHA NA TUME YA KATIBA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...