Kongamano hilo litajikita katika vipengele vifuatavyo:-
a)
Amani na
Utulivu wa Taifa letu kwa Miaka 50 Ijayo;
b)
Elimu na
Maendeleo ya Taifa kwa Miaka 50 Ijayo;
c)
Rasilimali
zetu kwa Maendeleo ya Kiuchumi ya Taifa.
Kongamano hilo litarushwa moja kwa moja na ITV, Radio One na Capital
Radio ili wananchi wote waweze kufuatilia kongamano hilo muhimu. Watakaongoza mjadala
ni Prof. Gaudence Mpangala, Dkt Martha Qorro, Dkt Haji Semboja, Dkt. Kitila
Mkumbo, Bw. Maggid Mjengwa na Mhandisi Joshwa Raya. Watakuwepo pia wazungumzaji
waalikwa kama vile: Mzee Joseph Butiku, Dkt Aldin Mutembei, Mh. January Makamba
(Mb), Julius Mtatiro, Usu Mallya na Esther Wassira.
Kongamano linategemewa kufungwa na Mh. Bernard Membe (Mb), Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Wote mnakaribishwa
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...