Jeshi la Polisi Nchini linamshikilia mtu mmoja ambaye jina lake linahifadhiwa kwa sababu za kiupelelezi kwa tuhuma za kueneza ujumbe wa uchochezi na chuki kwa wananchi na viongozi wa serikali kwa njia ya simu ya mkononi akituma SMS kwa lengo la kuchochea fujo, vurugu na kutoa matusi kwa viongozi hao.

Mtu huyo amekuwa akifanikisha kazi hiyo kwa kutumia Chips (sim card) 13 za simu za mkononi ambazo amekamatwa nazo. Jeshi la Polisi linaendelea kumhoji mtu huyo na ushahidi utakapokamilika atafikishwa mahakamani.

Aidha, Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wananchi wenye taarifa zingine za wahahlifu kama hao kujitokeza na kutoa taarifa hizo polisi ili wahalifu hao waweze kukamatwa na kuchukuliwa hatua stahiki, wakiwemo watu wanaowashawishi wenzao kwa njia ya fedha, kuwashauri ama kuwasaidia kwa namna yeyote ile katika kufanikisha uhalifu huo na kusababisha uvunjifu wa amani hapa nchini. Jeshi la polisi halitasita kumchukulia hatua mtu yeyote atakayebainika kuvunja sheria za nchi.

Imetolewa na:-
Advera Senso-SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...