Habari kutoka Dodoma zinasema Mbunge wa Kasulu Mjini kupitia chama cha NCCR-Mageuzi, Mhe. Moses Machali (pichani), amelazwa katika hospitali ya mkoa ya Dodoma kuuguza majeraha aliyoyapata baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo mjini Dodoma.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi na Mbunge wa kuteuliwa, Mhe James Mbatia, watu takriban wanane hivi walimshambulia Mhe Machali mnamo saa mbili za usiku akielekea kupumzika baada ya kuhudhuria vikao vya Bunge.

Mhe Mbatia amesema leo mjini Dodoma kwamba amemtembelea Mhe. Machali asubuhi hii na kumkuta anaendelea vyema na matibabu. 
Habari zaidi tutawaletea kwa kadri zitapopatikana.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 21, 2013

    Sitashangaa hapo tukiambiwa amejipiga mwenyewe! TUMEFIKA MAHALI YAANI HATA HAIFAHAMIKI MWENYE DHAMANA YA KULINDA WANANCHI NI NANI.
    POLE MBUNGE

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 22, 2013

    Mdau nakubaliana na wewe kabisa, baadhi ya watu wamekuwa si wakweli na hawayazungumzi ya ukweeli kabisa. Baadhi ya viongozi sikuhizi ni MAJANGAZ kabisa. visa vingi, wanapenda sifa, wanapenda kukejeli, wanapenda kusujudiwa na wana penda kuonewa huruma badala ya kuleta maendeleo nchini. POLE MBUNGE.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...