Msanii wa kimataifa Mohombi Nzasi Moupondo baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere kwa ajili ya shoo kali ya Serengeti Fiesta  itakayofanyika kesho katika viwanja vya Leaders Club. Mbele yake ni Fauzia mratibu wa shughuli za Serengeti Fiesta kutoka PrimeTime Promotions.
 Msanii wa kimataifa Mohombi Nzasi Moupondo  (kulia) akifanya
interview na wanahabari baada ya kutoka nje ya uwanja wa ndege kwa ajili
ya kufanya shoo kali ya Serengeti Fiesta inayotarajiwa kufanyika kesho
katika viwanja vya leaders club. Tamasha hilo limedhaminiwa na kampuni ya
bia ya Serengeti kupitia bia ya Serengeti Laga.
 Mohombi (kulia) akisindikizwa kutoka nje ya uwanja wa ndege wa
Mwalimu Nyerere  baada ya kushuka na ndege ya Turkish Air lines na Afisa
wa ndege hiyo Ebubekir Ekici ambaye pia alifurahia ujio wake Tanzania.
Msanii wa kimataifa anaetamba na kibao chake kikali cha “Kiss Me”
akiwa amepozi na mtangazaji wa Clouds Tv baada ya kupokelewa jana katika
uwanja wa ndege wa mwalimu Nyerere.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...