Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akisalimiana na wakazi wa mji wa Moshi waliojitokeza kwa wingi kushiriki mbio za Kilimanjaro Marathon 2016 ambapo mwaka huu zaidi ya watu elfu 8 walishiriki kutoka nchi mbali mbali ambapo kati ya hao 200 walitoka nchini Kenya.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akikimbia kwenye riadha ya Kilimanjaro Marathon 2016 ambapo alikimbia kilomita 5 pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Hai Mhe. Anthony Mtaka, mashindano hayo ya riadha yameshirikisha zaidi ya nchi 40.
Mshindi wa kwanza wa kilometa 42.2 Kiprotich Kirui akiinua mikono juu kama ishara ya kushangilia ushindi wa mbio za Kilimanjaro Marathon 2016.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...