MBUNGE wa Mafinga Mjini Mhe.  Cosato Chumi akizindua 
gari la kubeba wagonjwa (ambulance) 

Na fredy mgunda, Iringa

MBUNGE wa Mafinga Mjini Mhe.  Cosato Chumi kwa kushirikiana na asasi ya kimataifa ya Rafiki Surgical Mission ya Australia ametoa msaada wa gari la kubeba wagonjwa (ambulance) kwa ajili ya matumizi ya hospitali ya wilaya ya Mufindi, mkoani Iringa iliyopo katika jimbo lake hilo.

Gari hilo aina ya Toyota Hiace lenye thamani ya Sh Milioni 40 lilikabidhiwa jana kwa uongozi wa halmashauri ya mji wa Mafinga inayosimamia uendeshaji wa hospitali hiyo katika mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa mashujaa, mjini Mafinga.

Akikabidhi msaada huo Chumi alisema; “napenda ifahamike kwamba gari hilo limenunuliwa na asasi hiyo ambayo mimi ni rafiki yao mkubwa. Uadilifu na uaminifu kwa taasisi hiyo umetufanya tushirikiane vyema katika mambo mengi kwa faida ya wananchi wa jimbo langu la Mafinga.”

Alisema  gari hilo la wagonjwa ni rafiki kwa wagonjwa na wajawazito kwa kuwa lina vifaa tiba vinavyoweza kutumika kutolea huduma wakati wakipelekwa hospitalini.

Baada ya kukabidhi gari hilo, Chumi ambaye ni mbunge wa kwanza wa jimbo hilo jipya, mkoani Iringa alikumbusha vipaumbele vyake kwa wapiga kura wake kuwa ni kuhakikisha linapata huduma bora ya maji, elimu, afya na miundombinu ya barabara.

Akishukuru kwa msaada huo, Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji wa Mafinga, Dk Innocent Mhagama alisema kabla ya msaada huo, hospitali hiyo ya wilaya ilikuwa na gari moja tu la kubeba wagonjwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...